AJTC VOICE FO VOICLESS

Jumanne, 7 Machi 2017

MICHEZO YA JUMANNE HII YA LEO 07/03/2017

TFF – KAMATI YA UTENDAJI MACHI 26, ROBO FAINALI MACHI 18!

PRESS RELEASE NO. 264                                      MACHI 7, 2017
KIKAO CHA KAMATI YA UTENDAJI TFF
Kikao cha kawaida cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kinatarajiwa kukaa Machi 26, mwaka huu ambako pamoja na ajenda nyingine, itaamua tarehe rasmi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Kikao hiki cha kawaida, kwa mujibu wa katiba hufanyika mara nne kwa mwaka na huamua masuala mbalimbali ya uendeshaji na usimamizi wa mpira wa miguu nchini.
Kadhalika Mkutano Mkuu wa uchaguzi kwa mujibu wa Katiba ya TFF, hufanyika kila baada ya miaka minne kwa mwaka.
ROBO FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION CUP
Mechi mbili za kwanza hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Azam (Azam Sports Sports Federation Cup 2016/2017), zitachezwa Machi 18, mwaka huu kwenye viwanja viwili tofauti.
Mechi hizo ni kati ya Kagera Sugar itakayocheza na Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani Kagera kadhalika Simba itakayosafiri hadi Arusha kucheza na Madini kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Mechi nyingine zitapangiwa tarehe za baadaye. Mechi hizo ni kati ya Azam FC na Ndanda FC kadhalika Tanzania Prisons ya Mbeya itakayocheza na mshindi kati ya Young Africans ya Dar es Salaam na Kiluvya United ya Pwani.
Bingwa wa michuano hiyo kwa mujibu wa kanuni, atazawadiwa Tsh. 50 milioni.
Pia bingwa wa michuano hiyo, ndiye atakayeiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ya Total wakati Bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ndiye ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya Total Ligi ya Mabingwa Afrika.
..…………………………………………………………………………........................
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)  

IBRAHIMOVIC, MINGS KITANZINI.

MSHAMBULIAJI wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic na beki wa Bournemouth Tyrone Mings wamefunguliwa Mashitaka na Chama Soka cha Uingereza-FA kwa kuonyesha mchezo usio wa kiungwana. Wachezaji hao walichezeana faulo mara kwa mara kwenye mechi ya Jumamosi iliyopita ya Ligi Kuu ambapo timu hizo zilitoka Sare 1-1 katika Uwanja wa Old Trafford. Mings alimchezea faulo kwa kumkanyaga kichwani Ibrahimovic aliyekuwa ameanguka chini katika dakika ya 44 na dakika 2 baadae Ibrahimovic alijibu kwa kumpiga kiwiko Mings wakati akipiga kichwa mpira wa kona. Wachezaji hao wamepewa muda hadi kufikia leo kujibu mashitaka yao, FA imeeleza Matukio hayo waliyoshitakiwa nayo hayakuonwa na mwamuzi Kevin Friend lakini yalinaswa kwenye picha za video wakati mchezo ukiendelea. Kwa mujibu wa kanuni za FA, mchezaji kumpiga kiwiko na kumkanyaga mchezaji mwezake kwa makusudi ni faulo ambazo zinastahili kutolewa kadi nyekundu na pia adhabu ya kutocheza mechi tatu.

GUARDIOLA AELEZA MIPANGO YA USAJILI KIANGAZI.

MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema klabu inajipanga kufanya usajili majira ya kiangazi na wanakusudia kusajili wachezaji chipukizi wenye vipaji. City wako kwenye hatua za katikati katika mipango yao ya kusuka kikosi chao kufuatia kuwasajili John Stones, Claudio Bravo, Leroy Sane, Ilkay Gundogan, Nolito na Gabriel Jesus kiangazi mwaka jana. Akizungumza na wanahabari kuhusiana na suala hilo, Guardiola amesema klabu inasajili kwa ajili ya mipango ya muda mrefu ndio maana wamekuwa na wachezaji kama Raheem Sterling, Jesus na Sane. Guardiola amesema wanaweza kuongeza mchezaji mmoja au wawili wenye umri mkubwa kwsababu ya uzoefu pindi dirisha la usajili likapofunguliwa Juni.

XAVI ATAMANI KUINOA BARCELONA.

NGULI wa soka wa zamani wa Barcelona, Xavi amedai ana ndoto za kuja kuinoa klabu hiyo lakini ameweka wazi kuwa hayuko katika mpango wa kuchukua nafasi ya Luis Enrique mwishoni mwa msimu huu. Enrique alibainisha wiki iliyopita kuwa taachia ngazi pindi msimu utakapokamilika baada ya kukaa Camp Nou kwa miaka mitatu huku baadhi ya watu wakimpigia chapuo Xavi kuwa mtu sahihi wa kuchukua nafasi hiyo. Hata hivyo, pamoja na kwamba nguli huyo mwneye umri wa miaka 37 anayecheza soka katika timu ya Al Sadd ya Qatar, anapenda kuja kuinoa Barcelona siku za usoni lakini ameondoa uwezekano wa kutua sasa hivi kwakuwa hana uzoefu wa kutosha bado. Xavi amesema bado kuna vingi vya kujifunza pale linapokuja suala la kuwaongoza wachezaji 25 na benchi zima la ufundi pamoja na madaktari.

CONTE AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUTOLEWA SIFA.

MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte amewataka wachezaji wake kutulia baada ya kuifunga West Ham United kwa mabao 2-1 jana na kupiga hatua kubwa kuelekea katika ubingwa wa ligi Kuu. Chelsea wanaongoza kwa tofauti ya alama 10 dhidi ya Tottenham Hotspurs wanaoshika nafasi ya pili huku kukiwa kumebaki mechi 11 kabla ya msimu kumalizika. Mashabiki wa klabu hiyo jana walikuwa wakiimba nyimbo za ubingwa katika London, lakini Conte amesema wanapaswa kufikia jinsi ya kuchukua alama 26 zilizobakia kabla ya kujitangaza mabingwa. Akizungumza na wanahabari, Conte amesema wanapaswa kufikiri kila mpinzani watakayekutana naye anataka kuwafunga kuanzia sasa mpaka mwishoni. Conte aliendelea kudai kuwa mpaka sasa walipofika ni pazuri lakini jambo la muhimu ni kutojisahau na kuhakikisha wanaendeleza makal
IBRAHIMOVIC, MINGS KITANZINI. MSHAMBULIAJI wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic na beki wa Bournemouth Tyrone Mings wamefunguliwa Mashitaka na Chama Soka cha Uingereza-FA kwa kuonyesha mchezo usio wa kiungwana. Wachezaji hao walichezeana faulo mara kwa mara kwenye mechi ya Jumamosi iliyopita ya Ligi Kuu ambapo timu hizo zilitoka Sare 1-1 katika Uwanja wa Old Trafford. Mings alimchezea faulo kwa kumkanyaga kichwani Ibrahimovic aliyekuwa ameanguka chini katika dakika ya 44 na dakika 2 baadae Ibrahimovic alijibu kwa kumpiga kiwiko Mings wakati akipiga kichwa mpira wa kona. Wachezaji hao wamepewa muda hadi kufikia leo kujibu mashitaka yao, FA imeeleza Matukio hayo waliyoshitakiwa nayo hayakuonwa na mwamuzi Kevin Friend lakini yalinaswa kwenye picha za video wakati mchezo ukiendelea. Kwa mujibu wa kanuni za FA, mchezaji kumpiga kiwiko na kumkanyaga mchezaji mwezake kwa makusudi ni faulo ambazo zinastahili kutolewa kadi nyekundu na pia adhabu ya kutocheza mechi tatu. Posted by beki3 at 4:35 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest GUARDIOLA AELEZA MIPANGO YA USAJILI KIANGAZI. MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema klabu inajipanga kufanya usajili majira ya kiangazi na wanakusudia kusajili wachezaji chipukizi wenye vipaji. City wako kwenye hatua za katikati katika mipango yao ya kusuka kikosi chao kufuatia kuwasajili John Stones, Claudio Bravo, Leroy Sane, Ilkay Gundogan, Nolito na Gabriel Jesus kiangazi mwaka jana. Akizungumza na wanahabari kuhusiana na suala hilo, Guardiola amesema klabu inasajili kwa ajili ya mipango ya muda mrefu ndio maana wamekuwa na wachezaji kama Raheem Sterling, Jesus na Sane. Guardiola amesema wanaweza kuongeza mchezaji mmoja au wawili wenye umri mkubwa kwsababu ya uzoefu pindi dirisha la usajili likapofunguliwa Juni. Posted by beki3 at 4:18 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest XAVI ATAMANI KUINOA BARCELONA. NGULI wa soka wa zamani wa Barcelona, Xavi amedai ana ndoto za kuja kuinoa klabu hiyo lakini ameweka wazi kuwa hayuko katika mpango wa kuchukua nafasi ya Luis Enrique mwishoni mwa msimu huu. Enrique alibainisha wiki iliyopita kuwa taachia ngazi pindi msimu utakapokamilika baada ya kukaa Camp Nou kwa miaka mitatu huku baadhi ya watu wakimpigia chapuo Xavi kuwa mtu sahihi wa kuchukua nafasi hiyo. Hata hivyo, pamoja na kwamba nguli huyo mwneye umri wa miaka 37 anayecheza soka katika timu ya Al Sadd ya Qatar, anapenda kuja kuinoa Barcelona siku za usoni lakini ameondoa uwezekano wa kutua sasa hivi kwakuwa hana uzoefu wa kutosha bado. Xavi amesema bado kuna vingi vya kujifunza pale linapokuja suala la kuwaongoza wachezaji 25 na benchi zima la ufundi pamoja na madaktari. Posted by beki3 at 4:15 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest CONTE AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUTOLEWA SIFA. MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte amewataka wachezaji wake kutulia baada ya kuifunga West Ham United kwa mabao 2-1 jana na kupiga hatua kubwa kuelekea katika ubingwa wa ligi Kuu. Chelsea wanaongoza kwa tofauti ya alama 10 dhidi ya Tottenham Hotspurs wanaoshika nafasi ya pili huku kukiwa kumebaki mechi 11 kabla ya msimu kumalizika. Mashabiki wa klabu hiyo jana walikuwa wakiimba nyimbo za ubingwa katika London, lakini Conte amesema wanapaswa kufikia jinsi ya kuchukua alama 26 zilizobakia kabla ya kujitangaza mabingwa. Akizungumza na wanahabari, Conte amesema wanapaswa kufikiri kila mpinzani watakayekutana naye anataka kuwafunga kuanzia sasa mpaka mwishoni. Conte aliendelea kudai kuwa mpaka sasa walipofika ni pazuri lakini jambo la muhimu ni kutojisahau na kuhakikisha wanaendeleza makali yao.

Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap

LEO ARSENAL KUIAGA RASMI ULAYA? WANAWEZA KUPINDUA KIPONDO CHA 5-1 CHA BAYERN?

KWA MARA NYINGINE tena Arsenal wanachungulia kutupwa nje ya Hatua ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, hatua ambayo mara ya mwisho waliivuka Msimu wa 2009/10.
Kibarua kigumu cha Arsenakl kinatokana na kuchapwa 5-1 na Wababe wa Germany Bayern Munich kwenye Mechi yao ya Kwanza iliyochezwa Allianz Arena huko Munich.
Ili kusonga Robo Fainali, Arsenal wanahitaji ushindi wa 4-0 au matokeo mengine ili mradi tofauti ya Magoli ibakie 4-0 kwa upande wao.
Kazi hii ngumu ipo ngumu zaidi kwao kwa vile pia watamkosa Kiungo wao Mjerumani Mesut Ozil ambae ni Mgonjwa.
Lakini Arsenal wanaweza kumtumia kwa mara ya kwanza Sentahafu wao Mjerumani Per Mertesacker ambae ni Kepteni wao baada ya kupona Goti na hii itakuwa Mechi yake ya kwanza kucheza Msimu huu ikiwa atacheza.
Pia huenda Meneja wa Arsenal Arsene Wenger huenda akamuanzisha Fowadi wao kutoka Chile Alexis Sanchez ambae hakuanza Jumamosi iliyopita walipotwangwa 3-1 na Liverpool huko Anfield kwenye Mechi ya Ligi Kuu England baada kuvumishwa kulikuwa na rabsha Mazoezini iliyomhusu yeye.
Sanchez ndie Mfungaji Bora wa Arsenal Msimu huu akiwa na Bao 20.
Kwa upande wa Bayern Munich, chini ya Kocha Mtaliano Carlo Ancelotti, itawakosa Jerome Boateng ambae ni Majeruhi na Philipp Lahm ambae yupo Kifungoni.
+++++++++
JE WAJUA?
-Arsenal na Bayern zimekutana mara 11 na 7 kati ya hizo ni katika Miaka Minne iliyopita.
-Bayern imeshinda Mechi 6 na kufungwa 3 tu kati ya hizo huku wakiipiga Arsenal 5-1 mara 2 mfululizo katika Mechi 2 zilizopita.
-Hakuna Klabu iliyowahi kupindua kipigo cha Bao 4-0 au zaidi katika Mechi ya Kwanza na kusonga kwenye UCL.
+++++++++
Pengine matumaini makubwa kwa Arsenal ni kuwa Bayern imepigwa mara 2 mfululizo kila walipotua England katika Mechi 2 zilizopita na ya mwisho ikiwa Emirates walipochapwa 2-0 na Arsenal kwa Bao za Olivier Giroud na Mesut Ozil.
Lakini Bayern watatua Emirates wakiwa hawajafungwa katika Mechi 16 huku wakishinda Mechi 14 kati ya hizo mbio zilizoanzia Novemba Mwaka Jana.
Katika Mechi zao 5 zilizopita, Bayern wamenyuka Bao 20.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
ARSENAL: Ospina; Bellerin, Koscielny, Mustafi, Gibbs; Ramsey, Xhaka, Walcott, Iwobi, Sanchez; Giroud
BAYERN MUNICH: Neuer; Rafinha, Martinez, Hummels, Alaba; Alonso, Kimmich, Ribery, Muller, Robben; Lewandowski
REFA: Tasos Sidiropoulos (Greece)
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku Saa za Bongo
Mechi za Pili
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza
Jumanne 14 Machi 2017
Juventus v FC Porto      [2-0]
Leicester City v Sevilla [1-2]           
Jumatano 15 Machi 2017
Atlético Madrid v Bayer 04 Leverkusen [4-2]              
Monaco v Manchester City [3-5]     
++++++++++++++++++++++++++++
TAREHE MUHIMU:
MECHI ZA MTOANO:
14/15 na 21/22 Feb 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Kwanza
7/8 na 14/15 Machi 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Pili
11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza
18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili
02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)

CHELSEA YAPIGA, YAELEKEA UBINGWA!

++++++++++++++++++++
CHELSEA-UBINGWA
VINARA wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea, Jana wamezidi kupaa kileleni na sasa kuwa Pointi 10 mbele ya Timu ya Pili Tottenham Hotspur baada ya kuichapa West Ham United 2-1 huko London Stadium Jijini London.
Sasa, baada ya Mechi 27, Chelsea wana Pointi 66, Tottenham na wa 3 ni Man City wenye Pointi 55 kwa Mechi 26.
Hadi Mapumziko Chelsea walikuwa mbele 1-0 kwa Bao la Dakika ya 25 la Eden Hazard baada ya N'Golo Kante kuinasa Pasi ya Mchezaji wa West Ham Robert Snodgrass upande wa Chelsea na kumpasia Hazard aliesonga mbele na kucheza moja mbili na Pedro na kisha kumchambua Kipa Darren Randolph na kufunga.
Bao la Pili la Chelsea lilifungwa na Diego Costa katika Dakika ya 50 akiunganisha Kona ya Hazard na hilo ni Bao lake la 17 la Ligi Msimu huu.
West Ham walipata Bao lao pekee Dakika za Majeruhi, Dakika ya 92, baada ya Andy Carroll kumnyang’anya Mpira Cesc Fabregas na kumlisha Andrew Ayew aliempasia Lanzini na kufunga.
Ushindi huu ni wa 21 kwa Chelsea kwenye EPL Msimu huu na kidogo kidogo wananyemelea Utepe wa kutwaa Ubingwa.EPL-MAR7
VIKOSI:
West Ham:Randolph, Kouyate, Fonte, Reid [Byram 64'], Cresswell, Obiang, Noble [Fernandes 77'], Feghouli [Ayew 64'], Lanzini, Snodgrass, Carroll
Akiba:Adrian, Collins, Masuaku, Byram, Fernandes, Ayew, Calleri.
Chelsea:Courtois, Azpilicueta, David Luiz, Cahill, Moses [Zouma 76'], Fabregas, Kante, Alonso, Pedro [Matic 65'], Costa, Hazard [Willian 75']
Akiba:Begovic, Terry, Zouma, Matic, Loftus-Cheek, Willian, Batshuayi.
REFA:Andre Marriner
EPL – Ligi Kuu England
Ratiba
Jumamosi Machi 11
1800 Bournemouth v West Ham United           
Crystal Palace v Tottenham Hotspur [IMEAHIRISHWA]
1800 Everton v West Bromwich Albion            
1800 Hull City v Swansea City     
Middlesbrough v Sunderland [IMEAHIRISHWA]
Arsenal v Leicester City [IMEAHIRISHWA]
Jumapili Machi 12
Southampton v Manchester United [IMEAHIRISHWA]
1900 Liverpool v Burnley            
Jumatatu Machi 13
Chelsea v Watford [IMEAHIRISHWA]
Jumamosi Machi 18
1530 West Bromwich Albion v Arsenal             
1800 Crystal Palace v Watford              
1800 Everton v Hull City             
1800 Stoke City v Chelsea          
1800 Sunderland v Burnley         
1800 West Ham United v Leicester City 
2030 Bournemouth v Swansea City                 
Jumapili Machi 19
1500 Middlesbrough v Manchester United                 
1715 Tottenham Hotspur v Southampton                  
1930 Manchester City v Liverpool       

CHIRWA AFUNGA NNE, YANGA YAWAJERUHI KILUVYA 6-1 KOMBE LA TFF

YANGA SC imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ushindi wa kishindo wa mabao 6-1 dhidi ya Kiluvya United ya Pwani katika mchezo wa kukamilisha hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo inayojulikana pia kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, mshambuliaji Mzambia Obrey Chirwa alifunga mabao manne peke yake, huku mengine yakifungwa na viungo Geoffrey Mwashiuya na Juma Mahadhi. 
Yanga sasa itamenyana na Prisons katika Robo Fainali Machi 18, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mzambia Obrey Chirwa amefunga mabao manne peke yake, Yanga ikiichapa Kiluvya United 6-1 

Robo fainali nyingine zitakuwa kati ya Simba SC na Madini FC Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, Azam FC na Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na Kagera Sugar na Mbao FC ya Mwanza Uwanja wa Kaitaba.  
Katika mchezo wa leo uliochezeshwa refa hodari anayechipukia nchini, Kheri Sasii, hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Winga Geoffrey Mwashiuya alianza kuwafungia Yanga bao la kwanza dakika ya 11 kwa shuti kali baada ya kuwatoka vizuri wachezaji wa Kiluvya United kuanzia katikati pembezoni mwa Uwanja kushoto kufuatia pasi ya beki wa kushoto, Oscar Joshua.
⁠⁠⁠mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa akaifungia Yanga bao la pili dakika ya 24 kwa shuti kali pia baada ya pasi nzuri ya kutanguliziwa na mshambuliaji pacha wake leo, Juma Mahadhi. 
Chipukizi Edgar Charles Mfumakule akamtoka vizuri beki Mtogo, Vincent Bossou baada ya pasi ya Shala Juma na kumtungua kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ kuipatia Kiluvya United bao la kufutia machozi.
Geoffrey Mwashiuya na Juma Mahadhi walifunga mabao mengine ya Yanga leo
Juma Mahadhi (kushoto) aliumia misuli baada ya kufunga bao la tano dakika ya 74 na hakuweza kurejea uwanjani

Chirwa akaifungia Yanga mabao mawili mfulilizo dakika za 45 akimalizia pasi ya Juma Mahadhi na dakika ya 70 akimalizia krosi ya Hassan Kessy kukamilisha hat trick yake ya kwanza tangu ajiunge na timu hiyo Julai mwaka jana kutoka FC Platinums ya Zimbabwe.
Juma Mahadhi akaifungia Yanga bao la tano dakika ya 74 kwa shuti la umbali wa mita 21 hadi misuli ikambana. Yanga ilicheza pungufu tangu dakika ya 74 baada ya Mahadhi kuumia misuli na kutoka nje, wakati wamekwishatimiza idadi ya wachezaji watatu wa kubadili.
Kikosi cha Yanga kilikuwa; Deogratias Munishi ‘Dida’, Hassan Kessy, Oscar Joshua, Vincent Bossou, Said Juma ‘Makapu’/Justin Zulu dk48, Yussuf Mhilu/Emmanuel Martin dk35, Deus Kaseke, Juma Mahadhi, Obrey Chirwa na Geoffrey Mwashiuya/Simon Msuva dk44. 
Kiluvya United: Philimoni Ramadhani, Nassor Abubakar/Hashik Fakhi dk62, Ramadhani Ally, Jagani Mvugalo, Aloyce Nkya, Mwita Emmanuel, Yohana Richard, Hassan Ayoub, Edgar Charles/Juma Mohammed dk79, Shala Juma na Mwinyi Rehani/Ramadhani Said dk79.
 
KIINGILIO CHA CHINI AZAM NA MBABANE 3,000 TU

KIINGILIO cha chini katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Afrikaa kati ya wenyeji, Azam FC na Mbabane Swallows ya Swaziland Jumapili wiki hii kitakuwa Sh. 3,000.
Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kuanzia Saa 1.15 usiku.
Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd Maganga amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba Sh. 3000 ni kwa mashabiki watakaoketi majukwaa ya mzunguko.
Maganga amesema eneo la V.I.P B kiingilio kitakuwa ni Sh. 5,000 na V.I.P A itakuwa Sh. 10,000 na mashabiki watanunua tiketi kwa njia ya mtandao kupitia kampuni ya Selcom.
Nahodha wa Azam FC, John Bocco (kulia) anatarajiwa kuwa fiti kwa mchezo dhidi ya Mbabane
Maganga amesema wameamua kuuza tiketi hizo mapema, ili kuwarahisishia mashabiki wa soka nchini kupata tiketi hizo kwa haraka na kutosumbuka watakapokuwa wamefunga safari yao kuja kushuhudia mchezo huo.
“Kama unavyojua uwanja wetu ni mdogo, hivyo kwa kuuza tiketi hizo kwa mfumo huo tutakuwa tumewapunguzia usumbufu mashabiki wa soka kwani idadi kamili ikishatimia ya mashabiki wanaotakiwa basi zoezi la uuzaji tiketi litahitimishwa,” alisema.
Aidha alitoa wito kwa mashabiki kununua tiketi zao mapema ili kujiwekea uhakika wa kushuhudia uhondo wa mchezo huo kwani hadi sasa watu wengi wamekuwa na shauku kubwa ya kujitokeza uwanjani.
Katika hatua nyingine, waamuzi watakaochezesha mchezo huo kutoka nchini Benin wanatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa hii, ambao ni Mwamuzi wa Kati Adissa Abdul Raphiou Ligali, Mwamuzi Msaidizi Namba Moja, Medegnonwa Romains Agbodjogbe huku Msaidizi Namba Mbili akiwa ni Babadjide Bienvenu Dina. 
Kikosi cha Azam FC, kinachodhaminiwa na kinywaji safi cha Azam Cola burudani kwa koo lako na Benki bora kabisa nchini ya NMB, kipo kwenye hali nzuri kuelekea mchezo huo kikiwa hakika majeruhi hata mmoja jambo ambalo linatia matumaini makubwa ya timu hiyo kupata matokeo mazuri.
Jambo pekee ambalo limebakia hivi sasa, ni mashabiki wa soka kwa ujumla wenu nchini hasa jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti Azam FC kwenye mchezo huo kwani ndio moja ya timu pamoja na Yanga, ambazo zinaiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya Afrika.

IBRAHIMOVIC, MINGS KITANZINI. MSHAMBULIAJI wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic na beki wa Bournemouth Tyrone Mings wamefunguliwa Mashitaka na Chama Soka cha Uingereza-FA kwa kuonyesha mchezo usio wa kiungwana. Wachezaji hao walichezeana faulo mara kwa mara kwenye mechi ya Jumamosi iliyopita ya Ligi Kuu ambapo timu hizo zilitoka Sare 1-1 katika Uwanja wa Old Trafford. Mings alimchezea faulo kwa kumkanyaga kichwani Ibrahimovic aliyekuwa ameanguka chini katika dakika ya 44 na dakika 2 baadae Ibrahimovic alijibu kwa kumpiga kiwiko Mings wakati akipiga kichwa mpira wa kona. Wachezaji hao wamepewa muda hadi kufikia leo kujibu mashitaka yao, FA imeeleza Matukio hayo waliyoshitakiwa nayo hayakuonwa na mwamuzi Kevin Friend lakini yalinaswa kwenye picha za video wakati mchezo ukiendelea. Kwa mujibu wa kanuni za FA, mchezaji kumpiga kiwiko na kumkanyaga mchezaji mwezake kwa makusudi ni faulo ambazo zinastahili kutolewa kadi nyekundu na pia adhabu ya kutocheza mechi tatu. Posted by beki3 at 4:35 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest GUARDIOLA AELEZA MIPANGO YA USAJILI KIANGAZI. MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema klabu inajipanga kufanya usajili majira ya kiangazi na wanakusudia kusajili wachezaji chipukizi wenye vipaji. City wako kwenye hatua za katikati katika mipango yao ya kusuka kikosi chao kufuatia kuwasajili John Stones, Claudio Bravo, Leroy Sane, Ilkay Gundogan, Nolito na Gabriel Jesus kiangazi mwaka jana. Akizungumza na wanahabari kuhusiana na suala hilo, Guardiola amesema klabu inasajili kwa ajili ya mipango ya muda mrefu ndio maana wamekuwa na wachezaji kama Raheem Sterling, Jesus na Sane. Guardiola amesema wanaweza kuongeza mchezaji mmoja au wawili wenye umri mkubwa kwsababu ya uzoefu pindi dirisha la usajili likapofunguliwa Juni. Posted by beki3 at 4:18 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest XAVI ATAMANI KUINOA BARCELONA. NGULI wa soka wa zamani wa Barcelona, Xavi amedai ana ndoto za kuja kuinoa klabu hiyo lakini ameweka wazi kuwa hayuko katika mpango wa kuchukua nafasi ya Luis Enrique mwishoni mwa msimu huu. Enrique alibainisha wiki iliyopita kuwa taachia ngazi pindi msimu utakapokamilika baada ya kukaa Camp Nou kwa miaka mitatu huku baadhi ya watu wakimpigia chapuo Xavi kuwa mtu sahihi wa kuchukua nafasi hiyo. Hata hivyo, pamoja na kwamba nguli huyo mwneye umri wa miaka 37 anayecheza soka katika timu ya Al Sadd ya Qatar, anapenda kuja kuinoa Barcelona siku za usoni lakini ameondoa uwezekano wa kutua sasa hivi kwakuwa hana uzoefu wa kutosha bado. Xavi amesema bado kuna vingi vya kujifunza pale linapokuja suala la kuwaongoza wachezaji 25 na benchi zima la ufundi pamoja na madaktari. Posted by beki3 at 4:15 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest CONTE AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUTOLEWA SIFA. MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte amewataka wachezaji wake kutulia baada ya kuifunga West Ham United kwa mabao 2-1 jana na kupiga hatua kubwa kuelekea katika ubingwa wa ligi Kuu. Chelsea wanaongoza kwa tofauti ya alama 10 dhidi ya Tottenham Hotspurs wanaoshika nafasi ya pili huku kukiwa kumebaki mechi 11 kabla ya msimu kumalizika. Mashabiki wa klabu hiyo jana walikuwa wakiimba nyimbo za ubingwa katika London, lakini Conte amesema wanapaswa kufikia jinsi ya kuchukua alama 26 zilizobakia kabla ya kujitangaza mabingwa. Akizungumza na wanahabari, Conte amesema wanapaswa kufikiri kila mpinzani watakayekutana naye anataka kuwafunga kuanzia sasa mpaka mwishoni. Conte aliendelea kudai kuwa mpaka sasa walipofika ni pazuri lakini jambo la muhimu ni kutojisahau na kuhakikisha wanaendeleza makali yao.

Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni