Katika kuongeza hamasa kwa wachezaji wa Singida United, mkuu
wa mkoa huo Dkt. Rehema Nchimbiameibuka kwenye kambi ya timu na kutoa
kiasi cha shilingi 500,000 kama hamasa ya kuhakikisha timu inapata
ushindi.
“Mimi ninawafahamu wanangu kwamba mnaweza, hiyo 500,000 niliyowapa ni
sadaka ili mtuombee kwa Mungu viongozi wenu na watendaji wote.” – Dkt.
Rehema Nchimbi
“Sasa ninatoa sadaka ili mtuombee kwa Mungu atusamehe ili uwepo wake uwepo ili tuweze kuvuka vizuri.”
Macho na masikio ya watanzania yapo kwenye mechi ambayo
itapigwa kwenye uwanja wa Namfua mkoani Singida kati ya Singida United
dhidi ya Alliance Academy ya Mwanza mchezo wa ligi daraja la kwanza
Tanzania bara Kundi C.
Kocha wa Alliance Salvatory Edward amesema vijana wake wapo vizuri na
wanataraji wakuwashangaza wakazi wote wa Singida pamoja na wananchi wa
maeneo jirani.
“Vijana wote wako tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Singida United
ambao ni mgumu ukizingatia kila timu ina nafasi ya kwenda ligi kuu,
majeruhi ni wachache sana lakini kwa ujumla vijana wako vizuri.”
Kocha wa Singina Unidted Fred Felix Minziro amsema, kila mkazi wa
Singida aende uwanjani kushuhudia timu yao inavyokata tiketi ya kufuzu
kucheza ligi kuu.
Kwa ujumla maandalizi yanakweda vizuri hakuna majeruhi yeyote,
tumejipanga kupambana kama unavyojua mechi hiyo ni kufa au kupona lakini
sisi tumejipanga kuhakikisha watu wa Singida angalau wanapata timu
inayocheza ligi kuu.
Morali ipo juu kwa sababu watu wa Singida wana hamu ya kuona timu yao inacheza ligi kuu baada ya kukosa kwa miaka 17.
Nawaheshimu Alliance ni timu nzuri lakini na sisi tumejipanga
kukabiliana na hilo kwa sababu walitufunga kwenye mchezo wa kwanza
nyumbani kwao kwa hiyo na sisi tunataka kulipa kisasi.
Mechi nyingine za Kundi C ligi daraja la kwanza
Mgambo Shooting va Polisi Dodoma
Polisi Mara vs Mvuvumwa FC
Panone FC vs Rhino Rangers
Mechi za Kundi B
Mlale JKT vs Kurugenzi FC
Njombe Mji vs Coastal Union
‘Ondoeni shaka, kila kitu kipo kwenye mstari’ – Mkwasa
Katibu Mkuu wa Young Africans Charles Boniface Mkwasa amesema tayari wameshakamilisha taratibu zote za safari kuelekea visiwani Comoro kwa ajili ya mchezo wao wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Ngaya Club.
“Maandalizi yote yamekamilika kwa upande wetu kama utawala taratibu zote tumesha zifata na mambo yote muhimu tumesha yatekeleza kwa maana tayari tickets zimeshapatikana na timu imekuwa kambini kuanzia mwanzo wa wiki hii na wamekuwa wanaendelea na mazoezi kila siku.”
“Timu itaondoka kesho alfajiri, mda wa safari utakuwa ni dakika 90 na watapata muda mrefu wa mapumziko jioni watafanya mazoezi kwenye uwanja utakaotumiwa kwa ajili ya mechi siku ya Jumapili.”
“Baada mechi timu itarejea Jumanne kwa ajili ya maandalizi kwa ajili ya mechi ya marudiano kikosi chote kipo kaminili ukiachilia mbali majeruhi wachache, watanzania wasiwe na wasiwasi mambo yote yanaendelea vizuri.”
Yanga itasafri na msafara wa jumla ya watu 30. Wachezaji 20, benchi la ufundi litakuwa na watu nane, muwakilishi mmoja kutoka TFF, na mjumbe wa kamati ya utendaji ndio atakuwa kiongozi wa msafara.
Mashabiki wa Stand United wanaokata tamaa, kocha amewapa neno…
Stand United inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Majimaji kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, kocha wa Stand Augustino Malindi amesema wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo huo.
“Tumejipanga kushinda mechi dhidi ya Majimaji, mimi nafikiri kwenye mpira huwa hakuna sababu kwamba kwa nini umepoteza inapofikia wakati unafungwa inabidi ukubali na inapotokea timu imeshinda ni sawa kwa sababu ndio mpira ulivyo ndio maana timu inafanya mazoezi.” – Augustino Malindi
“Kuna sababu nyingine ambazo hata ukiziongelea inakuwa sio, mechi yetu tuliyocheza Kagera mwamuzi hakuwa fair kwa upande wetu kwa sababu tulipata penati mbili lakini hatukupewa hali kadhalika fourth official akamtoa kocha wetu wa makipa na kuwapandisha jukwaani.”
“Tumeenda Tanga hali ikawa hivyohivyo, mechi ambazo tulikuwa tunaweza kushinda lakini tunashindwa kutokana na maamuzi ya ma-referee.”
“Mashabiki wetu wasikate tama, watupe sapoti kama walivyotupokea tulivyorudi kucheza na Yanga. Mwalimu amefanyia kazi safu ya ushambuliaji na ulinzi tunaingia kucheza na Majimaji tukiamini tutapata ushindi na kuibuka na pointi tatu.”
SAMATTA APIGA BAO MECHI YA MAHASIMU, GENK YAUA 3-0
MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amerejea uwanjani usiku
wa jana na kuifungia KRC Genk bao la pili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya
mahasimu, Sint-Truiden katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Uwanja
wa Stayen, Sint-Truiden, St.-Trond.
Samatta aliyekuwa anacheza kwa mara ya kwanza tangu aumie mgongo Februari 1, alifunga bao lake dakika ya 39 kwa kichwa akimalizia krosi ya kiungo fundi wa Kispaniola, Alejandro Pozuelo Melero.
Na Pozuelo alimsetia Samatta kufunga bao la pili, akitoka kufunga bao la kwanza yeye mwenyewe dakika ya 37, akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji chipukizi Mbelgiji, Siebe Schrijvers.
Mbwana Samatta akikimbia kushangilia baada ya kufunga bao lake jana
Bao la tatu la KRC Genk ambayo sasa inafikisha pointi 41 katika nafasi ya tano baada ya kucheza mechi 26, lilifungwa na kiungo wa kimataifa wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy dakika ya 45.
Februari 1 Samatta alicheza kwa dakika 23 tu kabla ya kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo akiiacha KRC Genk ikifungwa 1-0 na KV Oostende Uwanja Luminus Arena, Genk katika mchezo wa Kombe la Ubelgiji na kutolewa.
Jana Samatta alicheza mechi ya 41 tangu asajiliwe Genk Januari mwaka jana, 18 msimu uliopita na 23 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 22 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 11 msimu huu.
Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati 10 hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na nne msimu huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao 12, sita msimu huu na sita msimu uliopita.
Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Ryan, Uronen, Colley/Wouters dk82, Brabec, Castagne, Berge, Malinovskyi, Pozuelo/Boetius dk62 Trossard/Naranjo dk70, Writers na Samatta.
STVV:Pirard, Mechele, Peeters, Gerkens, Bagayoko/Dussaut dk63, Janssens/Boli dk45, Kotysch, Valdivia, Fernandes, Vetokele na Bolingoli/Ceballos dk45.

SIMBA KURUDI KILELENI LIGI KUU LEO?
SIMBA
SC itajaribu kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
wakati itakapomenyana na Prisons ya Mbeya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
leo.
Timu hiyo ya kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog itaingia kwenye mchezo wa leo ikihitaji ushindi tu ili kurejea kileleni mwa Ligi Kuu.
Na hiyo ni kwa sababu wapinzani wao katika mbio za ubingwa, Yanga SC hawatakuwa na mechi ya Ligi Kuu wikiendi hii kwa kuwa wamekwenda Comoro kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Na wakitoka kushinda 3-0 ugenini katika mechi iliyopita ya Ligi Kuu dhidi ya wenyeji Maji Maji mjini Songea, Simba wanajamini kabisa leo wataendeleza wimbi la ushindi.
Na bila shaka, kocha Omog anayesaidiwa na Mganda, Jackson Mayanja leo ataendelea kupanga safu kali ya ushambuliaji ya wakali watatu, Juma Luizio, Ibrahim Hajib na Mrundi Laudit Mavugo.
Kwa ujumla Omog hatarijiwi kufanya mabadiliko makubwa kutoka kikosi kilichoifunga 3-0 Maji Maji Jumamosi Uwanja wa Maji Maji, Songea.
Na bila shaka langoni ataendelea kusimama Mghana Daniel Agyei, akisaidiwa na beki Mkongo Janvier Bokungu kulia, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kushoto na katikati Mzimbabwe Method Mwanjali na Novatus Lufunga.
Viungo wanaweza kuendelea kucheza Muzamil Yassin, Said Ndemla na Shizza Kichuya. Simba SC inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 48 baada ya kucheza mechi 21, ikiwa nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga wenye poinyi 49 za mechi 21.

JORDAN AYEW AJIUNGA NA SWANSEA, AJIFUNGA MIAKA MITATU NA NUSU
Pamoja na kutofanya vizuri katika msimu uliopita, Manchester United imeshika namba moja katika mauzo ya jezi baada ya kuuza zaidi ya jezi milioni 2.8.
Mauzo ya jezi kwa mwaka 2016 yameshikwa na Man United huku wakifuatiwa na Real Madrid ya Hispania iliyouza zaidi ya jezi milioni 2.2.
FC Barcelona ya Hispania pia, imeuza jezi milioni 1.9 na kufuatiwa na Chelsea Chelsea iliyouza jezi milioni 1.6.
LISTI YA KLABU ZILIZOUZA SANA
1) Manchester United (2,850,000)
2) Real Madrid (2,290,000)
3) Barcelona (1,980,000)
4) Chelsea (1,650,000)
5) Bayern Munich (1,500,000)
6) Arsenal (1,225,000)
7) Juventus (850,000)
8) Liverpool (705,000)
9) Paris Saint-Germain (685,000)
10) AC Milan (650,000)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni