AJTC VOICE FO VOICLESS

Jumatano, 18 Januari 2017

november 30/12



MAFUNZO YA VITENDO YAWA FURAHA KWA WANAFUNZI VYUONI

Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha,wakiwa katika mafunzo ya vitendo wakiwa darasani.


Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wametakiwa kujifunza masomo yao kwa vitendo ili kuongeza maarifa zaidi na kuleta ushindani katika soko la ajira pindi watakapoajiriwa.



Hayo yamesemwa na mkufunzi wa chuo hicho Bw;Steven Mulaki alipokuwa akihojiwa na SPIRITMWAMBA mapema leo mchana alipokuwa akiwafundisha wanafunzi wa darasa la Mt Ordizungwa.



Bw Mulaki ameongeza kwa kusema kuwa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wa vyuoni ni muhimu kwa kuwa watakapohitimu masomo yao itawasaidia kupata uzoefu watakapoajiriwa na taasisi au makampuni mbalimbali



Kwa upande wa wanafunzi wamefurahishwa na mafunzo hayo ambapo wengi wao wamemsifu mkufunzi huyo kwa kufundisha vizuri.




Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Singida Afariki Dunia, Mwili Kuagwa Leo Saa 11 Jioni Muhimbili

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) EX Peter Kakamba amefariki dunia alfajiri ya tarehe 30/11/2016 katika hospital ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kakamba alizaliwa mwaka 1963 katika kijiji cha Kawajense Wilayani Mpanda, mkoa wa Katavi. Alisoma shule ya msingi Shanwe Kawajense  mwaka 1973 hadi 1980, Kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari Kantalamba mwaka 1981 hadi 1984 ambapo kidato cha tano na sita alisoma katika shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro mwaka 1985 hadi 1987. Mwaka 1992 hadi 1994 alisoma Astashahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Marehemu alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1988 ambapo katika utumishi wake alipandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Konstable wa Polisi (1989), Sagenti wa Polisi (1991), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1997), Mkaguzi wa Polisi (2003), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (2006), Mrakibu wa Polisi (2008), Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2011), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2015) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2016).
 
Baadhi ya nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa  Mwendesha Mashtaka wa Polisi katika mkoa wa Iringa, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, Afisa mnadhimu wa Polisi katika Mikoa ya Iringa na Geita, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa na mpaka anafariki alikuwa Kamanda wa Polisi katika mkoa wa Singida.
 
Kufuatia kifo hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu anatoa pole kwa Maofisa, Wakaguzi,Askari, ndugu, jamaa na marafiki kwa Msiba huo.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa,
Jina la Bwana lihimidiwe - Amen.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.        

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni