JAMII YETU NI BAHARI YA HABARI MBALIMBALI
PATA HABARI KWA KINA NA UNDANI ZAIDI .
Jumatatu, 3 Aprili 2017
Jumanne, 7 Machi 2017
MICHEZO YA JUMANNE HII YA LEO 07/03/2017
TFF – KAMATI YA UTENDAJI MACHI 26, ROBO FAINALI MACHI 18!
PRESS RELEASE NO. 264 MACHI 7, 2017
KIKAO CHA KAMATI YA UTENDAJI TFF
Kikao
cha kawaida cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), kinatarajiwa kukaa Machi 26, mwaka huu ambako pamoja na
ajenda nyingine, itaamua tarehe rasmi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika
baadaye mwaka huu.
Kikao
hiki cha kawaida, kwa mujibu wa katiba hufanyika mara nne kwa mwaka na
huamua masuala mbalimbali ya uendeshaji na usimamizi wa mpira wa miguu
nchini.
Kadhalika Mkutano Mkuu wa uchaguzi kwa mujibu wa Katiba ya TFF, hufanyika kila baada ya miaka minne kwa mwaka.
ROBO FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION CUP
Mechi
mbili za kwanza hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Azam (Azam
Sports Sports Federation Cup 2016/2017), zitachezwa Machi 18, mwaka huu
kwenye viwanja viwili tofauti.
Mechi
hizo ni kati ya Kagera Sugar itakayocheza na Mbao FC ya Mwanza kwenye
Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani Kagera kadhalika Simba
itakayosafiri hadi Arusha kucheza na Madini kwenye Uwanja wa Sheikh Amri
Abeid jijini Arusha.
Mechi
nyingine zitapangiwa tarehe za baadaye. Mechi hizo ni kati ya Azam FC
na Ndanda FC kadhalika Tanzania Prisons ya Mbeya itakayocheza na mshindi
kati ya Young Africans ya Dar es Salaam na Kiluvya United ya Pwani.
Bingwa wa michuano hiyo kwa mujibu wa kanuni, atazawadiwa Tsh. 50 milioni.
Pia
bingwa wa michuano hiyo, ndiye atakayeiwakilisha nchi kwenye michuano
ya Kombe la Shirikisho Afrika ya Total wakati Bingwa wa Ligi Kuu
Tanzania Bara ndiye ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya Total Ligi ya
Mabingwa Afrika.
..…………………………………………………………………………........................
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
IBRAHIMOVIC, MINGS KITANZINI.
MSHAMBULIAJI wa
Manchester United Zlatan Ibrahimovic na beki wa Bournemouth Tyrone Mings
wamefunguliwa Mashitaka na Chama Soka cha Uingereza-FA kwa kuonyesha
mchezo usio wa kiungwana. Wachezaji hao walichezeana faulo mara kwa mara
kwenye mechi ya Jumamosi iliyopita ya Ligi Kuu ambapo timu hizo
zilitoka Sare 1-1 katika Uwanja wa Old Trafford. Mings alimchezea faulo
kwa kumkanyaga kichwani Ibrahimovic aliyekuwa ameanguka chini katika
dakika ya 44 na dakika 2 baadae Ibrahimovic alijibu kwa kumpiga kiwiko
Mings wakati akipiga kichwa mpira wa kona. Wachezaji hao wamepewa muda
hadi kufikia leo kujibu mashitaka yao, FA imeeleza Matukio hayo
waliyoshitakiwa nayo hayakuonwa na mwamuzi Kevin Friend lakini yalinaswa
kwenye picha za video wakati mchezo ukiendelea. Kwa mujibu wa kanuni za
FA, mchezaji kumpiga kiwiko na kumkanyaga mchezaji mwezake kwa makusudi
ni faulo ambazo zinastahili kutolewa kadi nyekundu na pia adhabu ya
kutocheza mechi tatu.
GUARDIOLA AELEZA MIPANGO YA USAJILI KIANGAZI.
MENEJA wa Manchester
City, Pep Guardiola amesema klabu inajipanga kufanya usajili majira ya
kiangazi na wanakusudia kusajili wachezaji chipukizi wenye vipaji. City
wako kwenye hatua za katikati katika mipango yao ya kusuka kikosi chao
kufuatia kuwasajili John Stones, Claudio Bravo, Leroy Sane, Ilkay
Gundogan, Nolito na Gabriel Jesus kiangazi mwaka jana. Akizungumza na
wanahabari kuhusiana na suala hilo, Guardiola amesema klabu inasajili
kwa ajili ya mipango ya muda mrefu ndio maana wamekuwa na wachezaji kama
Raheem Sterling, Jesus na Sane. Guardiola amesema wanaweza kuongeza
mchezaji mmoja au wawili wenye umri mkubwa kwsababu ya uzoefu pindi
dirisha la usajili likapofunguliwa Juni.
XAVI ATAMANI KUINOA BARCELONA.
NGULI wa soka wa zamani
wa Barcelona, Xavi amedai ana ndoto za kuja kuinoa klabu hiyo lakini
ameweka wazi kuwa hayuko katika mpango wa kuchukua nafasi ya Luis
Enrique mwishoni mwa msimu huu. Enrique alibainisha wiki iliyopita kuwa
taachia ngazi pindi msimu utakapokamilika baada ya kukaa Camp Nou kwa
miaka mitatu huku baadhi ya watu wakimpigia chapuo Xavi kuwa mtu sahihi
wa kuchukua nafasi hiyo. Hata hivyo, pamoja na kwamba nguli huyo mwneye
umri wa miaka 37 anayecheza soka katika timu ya Al Sadd ya Qatar,
anapenda kuja kuinoa Barcelona siku za usoni lakini ameondoa uwezekano
wa kutua sasa hivi kwakuwa hana uzoefu wa kutosha bado. Xavi amesema
bado kuna vingi vya kujifunza pale linapokuja suala la kuwaongoza
wachezaji 25 na benchi zima la ufundi pamoja na madaktari.
CONTE AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUTOLEWA SIFA.
MENEJA wa Chelsea,
Antonio Conte amewataka wachezaji wake kutulia baada ya kuifunga West
Ham United kwa mabao 2-1 jana na kupiga hatua kubwa kuelekea katika
ubingwa wa ligi Kuu. Chelsea wanaongoza kwa tofauti ya alama 10 dhidi ya
Tottenham Hotspurs wanaoshika nafasi ya pili huku kukiwa kumebaki mechi
11 kabla ya msimu kumalizika. Mashabiki wa klabu hiyo jana walikuwa
wakiimba nyimbo za ubingwa katika London, lakini Conte amesema wanapaswa
kufikia jinsi ya kuchukua alama 26 zilizobakia kabla ya kujitangaza
mabingwa. Akizungumza na wanahabari, Conte amesema wanapaswa kufikiri
kila mpinzani watakayekutana naye anataka kuwafunga kuanzia sasa mpaka
mwishoni. Conte aliendelea kudai kuwa mpaka sasa walipofika ni pazuri
lakini jambo la muhimu ni kutojisahau na kuhakikisha wanaendeleza makal
IBRAHIMOVIC, MINGS
KITANZINI.
MSHAMBULIAJI wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic na beki wa
Bournemouth Tyrone Mings wamefunguliwa Mashitaka na Chama Soka cha
Uingereza-FA kwa kuonyesha mchezo usio wa kiungwana. Wachezaji hao
walichezeana faulo mara kwa mara kwenye mechi ya Jumamosi iliyopita ya
Ligi Kuu ambapo timu hizo zilitoka Sare 1-1 katika Uwanja wa Old
Trafford. Mings alimchezea faulo kwa kumkanyaga kichwani Ibrahimovic
aliyekuwa ameanguka chini katika dakika ya 44 na dakika 2 baadae
Ibrahimovic alijibu kwa kumpiga kiwiko Mings wakati akipiga kichwa mpira
wa kona. Wachezaji hao wamepewa muda hadi kufikia leo kujibu mashitaka
yao, FA imeeleza Matukio hayo waliyoshitakiwa nayo hayakuonwa na mwamuzi
Kevin Friend lakini yalinaswa kwenye picha za video wakati mchezo
ukiendelea. Kwa mujibu wa kanuni za FA, mchezaji kumpiga kiwiko na
kumkanyaga mchezaji mwezake kwa makusudi ni faulo ambazo zinastahili
kutolewa kadi nyekundu na pia adhabu ya kutocheza mechi tatu.
Posted by beki3 at 4:35 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to
TwitterShare to FacebookShare to Pinterest
GUARDIOLA AELEZA MIPANGO YA USAJILI KIANGAZI.
MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema klabu inajipanga
kufanya usajili majira ya kiangazi na wanakusudia kusajili wachezaji
chipukizi wenye vipaji. City wako kwenye hatua za katikati katika
mipango yao ya kusuka kikosi chao kufuatia kuwasajili John Stones,
Claudio Bravo, Leroy Sane, Ilkay Gundogan, Nolito na Gabriel Jesus
kiangazi mwaka jana. Akizungumza na wanahabari kuhusiana na suala hilo,
Guardiola amesema klabu inasajili kwa ajili ya mipango ya muda mrefu
ndio maana wamekuwa na wachezaji kama Raheem Sterling, Jesus na Sane.
Guardiola amesema wanaweza kuongeza mchezaji mmoja au wawili wenye umri
mkubwa kwsababu ya uzoefu pindi dirisha la usajili likapofunguliwa Juni.
Posted by beki3 at 4:18 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to
TwitterShare to FacebookShare to Pinterest
XAVI ATAMANI KUINOA BARCELONA.
NGULI wa soka wa zamani wa Barcelona, Xavi amedai ana ndoto za kuja
kuinoa klabu hiyo lakini ameweka wazi kuwa hayuko katika mpango wa
kuchukua nafasi ya Luis Enrique mwishoni mwa msimu huu. Enrique
alibainisha wiki iliyopita kuwa taachia ngazi pindi msimu
utakapokamilika baada ya kukaa Camp Nou kwa miaka mitatu huku baadhi ya
watu wakimpigia chapuo Xavi kuwa mtu sahihi wa kuchukua nafasi hiyo.
Hata hivyo, pamoja na kwamba nguli huyo mwneye umri wa miaka 37
anayecheza soka katika timu ya Al Sadd ya Qatar, anapenda kuja kuinoa
Barcelona siku za usoni lakini ameondoa uwezekano wa kutua sasa hivi
kwakuwa hana uzoefu wa kutosha bado. Xavi amesema bado kuna vingi vya
kujifunza pale linapokuja suala la kuwaongoza wachezaji 25 na benchi
zima la ufundi pamoja na madaktari.
Posted by beki3 at 4:15 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to
TwitterShare to FacebookShare to Pinterest
CONTE AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUTOLEWA SIFA.
MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte amewataka wachezaji wake kutulia baada
ya kuifunga West Ham United kwa mabao 2-1 jana na kupiga hatua kubwa
kuelekea katika ubingwa wa ligi Kuu. Chelsea wanaongoza kwa tofauti ya
alama 10 dhidi ya Tottenham Hotspurs wanaoshika nafasi ya pili huku
kukiwa kumebaki mechi 11 kabla ya msimu kumalizika. Mashabiki wa klabu
hiyo jana walikuwa wakiimba nyimbo za ubingwa katika London, lakini
Conte amesema wanapaswa kufikia jinsi ya kuchukua alama 26 zilizobakia
kabla ya kujitangaza mabingwa. Akizungumza na wanahabari, Conte amesema
wanapaswa kufikiri kila mpinzani watakayekutana naye anataka kuwafunga
kuanzia sasa mpaka mwishoni. Conte aliendelea kudai kuwa mpaka sasa
walipofika ni pazuri lakini jambo la muhimu ni kutojisahau na
kuhakikisha wanaendeleza makali yao.
Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap

LEO ARSENAL KUIAGA RASMI ULAYA? WANAWEZA KUPINDUA KIPONDO CHA 5-1 CHA BAYERN?
KWA
MARA NYINGINE tena Arsenal wanachungulia kutupwa nje ya Hatua ya Raundi
ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, hatua ambayo mara ya
mwisho waliivuka Msimu wa 2009/10.
Kibarua
kigumu cha Arsenakl kinatokana na kuchapwa 5-1 na Wababe wa Germany
Bayern Munich kwenye Mechi yao ya Kwanza iliyochezwa Allianz Arena huko
Munich.
Ili
kusonga Robo Fainali, Arsenal wanahitaji ushindi wa 4-0 au matokeo
mengine ili mradi tofauti ya Magoli ibakie 4-0 kwa upande wao.
Kazi hii ngumu ipo ngumu zaidi kwao kwa vile pia watamkosa Kiungo wao Mjerumani Mesut Ozil ambae ni Mgonjwa.
Lakini
Arsenal wanaweza kumtumia kwa mara ya kwanza Sentahafu wao Mjerumani
Per Mertesacker ambae ni Kepteni wao baada ya kupona Goti na hii itakuwa
Mechi yake ya kwanza kucheza Msimu huu ikiwa atacheza.
Pia
huenda Meneja wa Arsenal Arsene Wenger huenda akamuanzisha Fowadi wao
kutoka Chile Alexis Sanchez ambae hakuanza Jumamosi iliyopita
walipotwangwa 3-1 na Liverpool huko Anfield kwenye Mechi ya Ligi Kuu
England baada kuvumishwa kulikuwa na rabsha Mazoezini iliyomhusu yeye.
Sanchez ndie Mfungaji Bora wa Arsenal Msimu huu akiwa na Bao 20.
Kwa
upande wa Bayern Munich, chini ya Kocha Mtaliano Carlo Ancelotti,
itawakosa Jerome Boateng ambae ni Majeruhi na Philipp Lahm ambae yupo
Kifungoni.
+++++++++
JE WAJUA?
-Arsenal na Bayern zimekutana mara 11 na 7 kati ya hizo ni katika Miaka Minne iliyopita.
-Bayern imeshinda Mechi 6 na kufungwa 3 tu kati ya hizo huku wakiipiga Arsenal 5-1 mara 2 mfululizo katika Mechi 2 zilizopita.
-Hakuna Klabu iliyowahi kupindua kipigo cha Bao 4-0 au zaidi katika Mechi ya Kwanza na kusonga kwenye UCL.
+++++++++
Pengine
matumaini makubwa kwa Arsenal ni kuwa Bayern imepigwa mara 2 mfululizo
kila walipotua England katika Mechi 2 zilizopita na ya mwisho ikiwa Emirates walipochapwa 2-0 na Arsenal kwa Bao za Olivier Giroud na Mesut Ozil.
Lakini
Bayern watatua Emirates wakiwa hawajafungwa katika Mechi 16 huku
wakishinda Mechi 14 kati ya hizo mbio zilizoanzia Novemba Mwaka Jana.
Katika Mechi zao 5 zilizopita, Bayern wamenyuka Bao 20.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
ARSENAL: Ospina; Bellerin, Koscielny, Mustafi, Gibbs; Ramsey, Xhaka, Walcott, Iwobi, Sanchez; Giroud
BAYERN MUNICH: Neuer; Rafinha, Martinez, Hummels, Alaba; Alonso, Kimmich, Ribery, Muller, Robben; Lewandowski
REFA: Tasos Sidiropoulos (Greece)
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku Saa za Bongo
Mechi za Pili
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza
Jumanne 14 Machi 2017
Juventus v FC Porto [2-0]
Leicester City v Sevilla [1-2]
Jumatano 15 Machi 2017
Atlético Madrid v Bayer 04 Leverkusen [4-2]
Monaco v Manchester City [3-5]
++++++++++++++++++++++++++++
TAREHE MUHIMU:
MECHI ZA MTOANO:
14/15 na 21/22 Feb 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Kwanza
7/8 na 14/15 Machi 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Pili
11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza
18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili
02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)
CHELSEA YAPIGA, YAELEKEA UBINGWA!
++++++++++++++++++++
VINARA
wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea, Jana wamezidi kupaa kileleni na sasa
kuwa Pointi 10 mbele ya Timu ya Pili Tottenham Hotspur baada ya
kuichapa West Ham United 2-1 huko London Stadium Jijini London.
Sasa, baada ya Mechi 27, Chelsea wana Pointi 66, Tottenham na wa 3 ni Man City wenye Pointi 55 kwa Mechi 26.
Hadi
Mapumziko Chelsea walikuwa mbele 1-0 kwa Bao la Dakika ya 25 la Eden
Hazard baada ya N'Golo Kante kuinasa Pasi ya Mchezaji wa West Ham Robert
Snodgrass upande wa Chelsea na kumpasia Hazard aliesonga mbele na
kucheza moja mbili na Pedro na kisha kumchambua Kipa Darren Randolph na
kufunga.
Bao
la Pili la Chelsea lilifungwa na Diego Costa katika Dakika ya 50
akiunganisha Kona ya Hazard na hilo ni Bao lake la 17 la Ligi Msimu huu.
West
Ham walipata Bao lao pekee Dakika za Majeruhi, Dakika ya 92, baada ya
Andy Carroll kumnyang’anya Mpira Cesc Fabregas na kumlisha Andrew Ayew
aliempasia Lanzini na kufunga.
Ushindi huu ni wa 21 kwa Chelsea kwenye EPL Msimu huu na kidogo kidogo wananyemelea Utepe wa kutwaa Ubingwa.
VIKOSI:
West Ham:Randolph,
Kouyate, Fonte, Reid [Byram 64'], Cresswell, Obiang, Noble [Fernandes
77'], Feghouli [Ayew 64'], Lanzini, Snodgrass, Carroll
Akiba:Adrian, Collins, Masuaku, Byram, Fernandes, Ayew, Calleri.
Chelsea:Courtois,
Azpilicueta, David Luiz, Cahill, Moses [Zouma 76'], Fabregas, Kante,
Alonso, Pedro [Matic 65'], Costa, Hazard [Willian 75']
Akiba:Begovic, Terry, Zouma, Matic, Loftus-Cheek, Willian, Batshuayi.
REFA:Andre Marriner
EPL – Ligi Kuu England
Ratiba
Jumamosi Machi 11
1800 Bournemouth v West Ham United
Crystal Palace v Tottenham Hotspur [IMEAHIRISHWA]
1800 Everton v West Bromwich Albion
1800 Hull City v Swansea City
Middlesbrough v Sunderland [IMEAHIRISHWA]
Arsenal v Leicester City [IMEAHIRISHWA]
Jumapili Machi 12
Southampton v Manchester United [IMEAHIRISHWA]
1900 Liverpool v Burnley
Jumatatu Machi 13
Chelsea v Watford [IMEAHIRISHWA]
Jumamosi Machi 18
1530 West Bromwich Albion v Arsenal
1800 Crystal Palace v Watford
1800 Everton v Hull City
1800 Stoke City v Chelsea
1800 Sunderland v Burnley
1800 West Ham United v Leicester City
2030 Bournemouth v Swansea City
Jumapili Machi 19
1500 Middlesbrough v Manchester United
1715 Tottenham Hotspur v Southampton
1930 Manchester City v Liverpool
CHIRWA AFUNGA NNE, YANGA YAWAJERUHI KILUVYA 6-1 KOMBE LA TFF
YANGA SC imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ushindi wa kishindo wa mabao 6-1 dhidi ya Kiluvya United ya Pwani katika mchezo wa kukamilisha hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo inayojulikana pia kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, mshambuliaji Mzambia Obrey Chirwa alifunga mabao manne peke yake, huku mengine yakifungwa na viungo Geoffrey Mwashiuya na Juma Mahadhi.
Yanga sasa itamenyana na Prisons katika Robo Fainali Machi 18, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mzambia Obrey Chirwa amefunga mabao manne peke yake, Yanga ikiichapa Kiluvya United 6-1
Robo fainali nyingine zitakuwa kati ya Simba SC na Madini FC Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, Azam FC na Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na Kagera Sugar na Mbao FC ya Mwanza Uwanja wa Kaitaba.
Katika mchezo wa leo uliochezeshwa refa hodari anayechipukia nchini, Kheri Sasii, hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Winga Geoffrey Mwashiuya alianza kuwafungia Yanga bao la kwanza dakika ya 11 kwa shuti kali baada ya kuwatoka vizuri wachezaji wa Kiluvya United kuanzia katikati pembezoni mwa Uwanja kushoto kufuatia pasi ya beki wa kushoto, Oscar Joshua.
mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa akaifungia Yanga bao la pili dakika ya 24 kwa shuti kali pia baada ya pasi nzuri ya kutanguliziwa na mshambuliaji pacha wake leo, Juma Mahadhi.
Chipukizi Edgar Charles Mfumakule akamtoka vizuri beki Mtogo, Vincent Bossou baada ya pasi ya Shala Juma na kumtungua kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ kuipatia Kiluvya United bao la kufutia machozi.
Geoffrey Mwashiuya na Juma Mahadhi walifunga mabao mengine ya Yanga leo

Chirwa akaifungia Yanga mabao mawili mfulilizo dakika za 45 akimalizia pasi ya Juma Mahadhi na dakika ya 70 akimalizia krosi ya Hassan Kessy kukamilisha hat trick yake ya kwanza tangu ajiunge na timu hiyo Julai mwaka jana kutoka FC Platinums ya Zimbabwe.
Juma Mahadhi akaifungia Yanga bao la tano dakika ya 74 kwa shuti la umbali wa mita 21 hadi misuli ikambana. Yanga ilicheza pungufu tangu dakika ya 74 baada ya Mahadhi kuumia misuli na kutoka nje, wakati wamekwishatimiza idadi ya wachezaji watatu wa kubadili.
Kikosi cha Yanga kilikuwa; Deogratias Munishi ‘Dida’, Hassan Kessy, Oscar Joshua, Vincent Bossou, Said Juma ‘Makapu’/Justin Zulu dk48, Yussuf Mhilu/Emmanuel Martin dk35, Deus Kaseke, Juma Mahadhi, Obrey Chirwa na Geoffrey Mwashiuya/Simon Msuva dk44.
Kiluvya United: Philimoni Ramadhani, Nassor Abubakar/Hashik Fakhi dk62, Ramadhani Ally, Jagani Mvugalo, Aloyce Nkya, Mwita Emmanuel, Yohana Richard, Hassan Ayoub, Edgar Charles/Juma Mohammed dk79, Shala Juma na Mwinyi Rehani/Ramadhani Said dk79.
KIINGILIO CHA CHINI AZAM NA MBABANE 3,000 TU
KIINGILIO cha chini katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Afrikaa kati ya wenyeji, Azam FC na Mbabane Swallows ya Swaziland Jumapili wiki hii kitakuwa Sh. 3,000.
Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kuanzia Saa 1.15 usiku.
Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd Maganga amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba Sh. 3000 ni kwa mashabiki watakaoketi majukwaa ya mzunguko.
Maganga amesema eneo la V.I.P B kiingilio kitakuwa ni Sh. 5,000 na V.I.P A itakuwa Sh. 10,000 na mashabiki watanunua tiketi kwa njia ya mtandao kupitia kampuni ya Selcom.
![]() |
| Nahodha wa Azam FC, John Bocco (kulia) anatarajiwa kuwa fiti kwa mchezo dhidi ya Mbabane |
“Kama unavyojua uwanja wetu ni mdogo, hivyo kwa kuuza tiketi hizo kwa mfumo huo tutakuwa tumewapunguzia usumbufu mashabiki wa soka kwani idadi kamili ikishatimia ya mashabiki wanaotakiwa basi zoezi la uuzaji tiketi litahitimishwa,” alisema.
Aidha alitoa wito kwa mashabiki kununua tiketi zao mapema ili kujiwekea uhakika wa kushuhudia uhondo wa mchezo huo kwani hadi sasa watu wengi wamekuwa na shauku kubwa ya kujitokeza uwanjani.
Katika hatua nyingine, waamuzi watakaochezesha mchezo huo kutoka nchini Benin wanatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa hii, ambao ni Mwamuzi wa Kati Adissa Abdul Raphiou Ligali, Mwamuzi Msaidizi Namba Moja, Medegnonwa Romains Agbodjogbe huku Msaidizi Namba Mbili akiwa ni Babadjide Bienvenu Dina.
Kikosi cha Azam FC, kinachodhaminiwa na kinywaji safi cha Azam Cola burudani kwa koo lako na Benki bora kabisa nchini ya NMB, kipo kwenye hali nzuri kuelekea mchezo huo kikiwa hakika majeruhi hata mmoja jambo ambalo linatia matumaini makubwa ya timu hiyo kupata matokeo mazuri.
Jambo pekee ambalo limebakia hivi sasa, ni mashabiki wa soka kwa ujumla wenu nchini hasa jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti Azam FC kwenye mchezo huo kwani ndio moja ya timu pamoja na Yanga, ambazo zinaiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya Afrika.
IBRAHIMOVIC, MINGS
KITANZINI.
MSHAMBULIAJI wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic na beki wa
Bournemouth Tyrone Mings wamefunguliwa Mashitaka na Chama Soka cha
Uingereza-FA kwa kuonyesha mchezo usio wa kiungwana. Wachezaji hao
walichezeana faulo mara kwa mara kwenye mechi ya Jumamosi iliyopita ya
Ligi Kuu ambapo timu hizo zilitoka Sare 1-1 katika Uwanja wa Old
Trafford. Mings alimchezea faulo kwa kumkanyaga kichwani Ibrahimovic
aliyekuwa ameanguka chini katika dakika ya 44 na dakika 2 baadae
Ibrahimovic alijibu kwa kumpiga kiwiko Mings wakati akipiga kichwa mpira
wa kona. Wachezaji hao wamepewa muda hadi kufikia leo kujibu mashitaka
yao, FA imeeleza Matukio hayo waliyoshitakiwa nayo hayakuonwa na mwamuzi
Kevin Friend lakini yalinaswa kwenye picha za video wakati mchezo
ukiendelea. Kwa mujibu wa kanuni za FA, mchezaji kumpiga kiwiko na
kumkanyaga mchezaji mwezake kwa makusudi ni faulo ambazo zinastahili
kutolewa kadi nyekundu na pia adhabu ya kutocheza mechi tatu.
Posted by beki3 at 4:35 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to
TwitterShare to FacebookShare to Pinterest
GUARDIOLA AELEZA MIPANGO YA USAJILI KIANGAZI.
MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema klabu inajipanga
kufanya usajili majira ya kiangazi na wanakusudia kusajili wachezaji
chipukizi wenye vipaji. City wako kwenye hatua za katikati katika
mipango yao ya kusuka kikosi chao kufuatia kuwasajili John Stones,
Claudio Bravo, Leroy Sane, Ilkay Gundogan, Nolito na Gabriel Jesus
kiangazi mwaka jana. Akizungumza na wanahabari kuhusiana na suala hilo,
Guardiola amesema klabu inasajili kwa ajili ya mipango ya muda mrefu
ndio maana wamekuwa na wachezaji kama Raheem Sterling, Jesus na Sane.
Guardiola amesema wanaweza kuongeza mchezaji mmoja au wawili wenye umri
mkubwa kwsababu ya uzoefu pindi dirisha la usajili likapofunguliwa Juni.
Posted by beki3 at 4:18 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to
TwitterShare to FacebookShare to Pinterest
XAVI ATAMANI KUINOA BARCELONA.
NGULI wa soka wa zamani wa Barcelona, Xavi amedai ana ndoto za kuja
kuinoa klabu hiyo lakini ameweka wazi kuwa hayuko katika mpango wa
kuchukua nafasi ya Luis Enrique mwishoni mwa msimu huu. Enrique
alibainisha wiki iliyopita kuwa taachia ngazi pindi msimu
utakapokamilika baada ya kukaa Camp Nou kwa miaka mitatu huku baadhi ya
watu wakimpigia chapuo Xavi kuwa mtu sahihi wa kuchukua nafasi hiyo.
Hata hivyo, pamoja na kwamba nguli huyo mwneye umri wa miaka 37
anayecheza soka katika timu ya Al Sadd ya Qatar, anapenda kuja kuinoa
Barcelona siku za usoni lakini ameondoa uwezekano wa kutua sasa hivi
kwakuwa hana uzoefu wa kutosha bado. Xavi amesema bado kuna vingi vya
kujifunza pale linapokuja suala la kuwaongoza wachezaji 25 na benchi
zima la ufundi pamoja na madaktari.
Posted by beki3 at 4:15 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to
TwitterShare to FacebookShare to Pinterest
CONTE AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUTOLEWA SIFA.
MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte amewataka wachezaji wake kutulia baada
ya kuifunga West Ham United kwa mabao 2-1 jana na kupiga hatua kubwa
kuelekea katika ubingwa wa ligi Kuu. Chelsea wanaongoza kwa tofauti ya
alama 10 dhidi ya Tottenham Hotspurs wanaoshika nafasi ya pili huku
kukiwa kumebaki mechi 11 kabla ya msimu kumalizika. Mashabiki wa klabu
hiyo jana walikuwa wakiimba nyimbo za ubingwa katika London, lakini
Conte amesema wanapaswa kufikia jinsi ya kuchukua alama 26 zilizobakia
kabla ya kujitangaza mabingwa. Akizungumza na wanahabari, Conte amesema
wanapaswa kufikiri kila mpinzani watakayekutana naye anataka kuwafunga
kuanzia sasa mpaka mwishoni. Conte aliendelea kudai kuwa mpaka sasa
walipofika ni pazuri lakini jambo la muhimu ni kutojisahau na
kuhakikisha wanaendeleza makali yao.
Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap
Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap
Ijumaa, 10 Februari 2017
HABARI ZA MICHEZO JUAMOSI YA TAREHE 11/02/2017
Katika kuongeza hamasa kwa wachezaji wa Singida United, mkuu
wa mkoa huo Dkt. Rehema Nchimbiameibuka kwenye kambi ya timu na kutoa
kiasi cha shilingi 500,000 kama hamasa ya kuhakikisha timu inapata
ushindi.
“Mimi ninawafahamu wanangu kwamba mnaweza, hiyo 500,000 niliyowapa ni
sadaka ili mtuombee kwa Mungu viongozi wenu na watendaji wote.” – Dkt.
Rehema Nchimbi
“Sasa ninatoa sadaka ili mtuombee kwa Mungu atusamehe ili uwepo wake uwepo ili tuweze kuvuka vizuri.”
Macho na masikio ya watanzania yapo kwenye mechi ambayo
itapigwa kwenye uwanja wa Namfua mkoani Singida kati ya Singida United
dhidi ya Alliance Academy ya Mwanza mchezo wa ligi daraja la kwanza
Tanzania bara Kundi C.
Kocha wa Alliance Salvatory Edward amesema vijana wake wapo vizuri na
wanataraji wakuwashangaza wakazi wote wa Singida pamoja na wananchi wa
maeneo jirani.
“Vijana wote wako tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Singida United
ambao ni mgumu ukizingatia kila timu ina nafasi ya kwenda ligi kuu,
majeruhi ni wachache sana lakini kwa ujumla vijana wako vizuri.”
Kocha wa Singina Unidted Fred Felix Minziro amsema, kila mkazi wa
Singida aende uwanjani kushuhudia timu yao inavyokata tiketi ya kufuzu
kucheza ligi kuu.
Kwa ujumla maandalizi yanakweda vizuri hakuna majeruhi yeyote,
tumejipanga kupambana kama unavyojua mechi hiyo ni kufa au kupona lakini
sisi tumejipanga kuhakikisha watu wa Singida angalau wanapata timu
inayocheza ligi kuu.
Morali ipo juu kwa sababu watu wa Singida wana hamu ya kuona timu yao inacheza ligi kuu baada ya kukosa kwa miaka 17.
Nawaheshimu Alliance ni timu nzuri lakini na sisi tumejipanga
kukabiliana na hilo kwa sababu walitufunga kwenye mchezo wa kwanza
nyumbani kwao kwa hiyo na sisi tunataka kulipa kisasi.
Mechi nyingine za Kundi C ligi daraja la kwanza
Mgambo Shooting va Polisi Dodoma
Polisi Mara vs Mvuvumwa FC
Panone FC vs Rhino Rangers
Mechi za Kundi B
Mlale JKT vs Kurugenzi FC
Njombe Mji vs Coastal Union
‘Ondoeni shaka, kila kitu kipo kwenye mstari’ – Mkwasa
Katibu Mkuu wa Young Africans Charles Boniface Mkwasa amesema tayari wameshakamilisha taratibu zote za safari kuelekea visiwani Comoro kwa ajili ya mchezo wao wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Ngaya Club.
“Maandalizi yote yamekamilika kwa upande wetu kama utawala taratibu zote tumesha zifata na mambo yote muhimu tumesha yatekeleza kwa maana tayari tickets zimeshapatikana na timu imekuwa kambini kuanzia mwanzo wa wiki hii na wamekuwa wanaendelea na mazoezi kila siku.”
“Timu itaondoka kesho alfajiri, mda wa safari utakuwa ni dakika 90 na watapata muda mrefu wa mapumziko jioni watafanya mazoezi kwenye uwanja utakaotumiwa kwa ajili ya mechi siku ya Jumapili.”
“Baada mechi timu itarejea Jumanne kwa ajili ya maandalizi kwa ajili ya mechi ya marudiano kikosi chote kipo kaminili ukiachilia mbali majeruhi wachache, watanzania wasiwe na wasiwasi mambo yote yanaendelea vizuri.”
Yanga itasafri na msafara wa jumla ya watu 30. Wachezaji 20, benchi la ufundi litakuwa na watu nane, muwakilishi mmoja kutoka TFF, na mjumbe wa kamati ya utendaji ndio atakuwa kiongozi wa msafara.
Mashabiki wa Stand United wanaokata tamaa, kocha amewapa neno…
Stand United inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Majimaji kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, kocha wa Stand Augustino Malindi amesema wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo huo.
“Tumejipanga kushinda mechi dhidi ya Majimaji, mimi nafikiri kwenye mpira huwa hakuna sababu kwamba kwa nini umepoteza inapofikia wakati unafungwa inabidi ukubali na inapotokea timu imeshinda ni sawa kwa sababu ndio mpira ulivyo ndio maana timu inafanya mazoezi.” – Augustino Malindi
“Kuna sababu nyingine ambazo hata ukiziongelea inakuwa sio, mechi yetu tuliyocheza Kagera mwamuzi hakuwa fair kwa upande wetu kwa sababu tulipata penati mbili lakini hatukupewa hali kadhalika fourth official akamtoa kocha wetu wa makipa na kuwapandisha jukwaani.”
“Tumeenda Tanga hali ikawa hivyohivyo, mechi ambazo tulikuwa tunaweza kushinda lakini tunashindwa kutokana na maamuzi ya ma-referee.”
“Mashabiki wetu wasikate tama, watupe sapoti kama walivyotupokea tulivyorudi kucheza na Yanga. Mwalimu amefanyia kazi safu ya ushambuliaji na ulinzi tunaingia kucheza na Majimaji tukiamini tutapata ushindi na kuibuka na pointi tatu.”
SAMATTA APIGA BAO MECHI YA MAHASIMU, GENK YAUA 3-0
MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amerejea uwanjani usiku
wa jana na kuifungia KRC Genk bao la pili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya
mahasimu, Sint-Truiden katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Uwanja
wa Stayen, Sint-Truiden, St.-Trond.
Samatta aliyekuwa anacheza kwa mara ya kwanza tangu aumie mgongo Februari 1, alifunga bao lake dakika ya 39 kwa kichwa akimalizia krosi ya kiungo fundi wa Kispaniola, Alejandro Pozuelo Melero.
Na Pozuelo alimsetia Samatta kufunga bao la pili, akitoka kufunga bao la kwanza yeye mwenyewe dakika ya 37, akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji chipukizi Mbelgiji, Siebe Schrijvers.
Mbwana Samatta akikimbia kushangilia baada ya kufunga bao lake jana
Bao la tatu la KRC Genk ambayo sasa inafikisha pointi 41 katika nafasi ya tano baada ya kucheza mechi 26, lilifungwa na kiungo wa kimataifa wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy dakika ya 45.
Februari 1 Samatta alicheza kwa dakika 23 tu kabla ya kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo akiiacha KRC Genk ikifungwa 1-0 na KV Oostende Uwanja Luminus Arena, Genk katika mchezo wa Kombe la Ubelgiji na kutolewa.
Jana Samatta alicheza mechi ya 41 tangu asajiliwe Genk Januari mwaka jana, 18 msimu uliopita na 23 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 22 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 11 msimu huu.
Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati 10 hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na nne msimu huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao 12, sita msimu huu na sita msimu uliopita.
Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Ryan, Uronen, Colley/Wouters dk82, Brabec, Castagne, Berge, Malinovskyi, Pozuelo/Boetius dk62 Trossard/Naranjo dk70, Writers na Samatta.
STVV:Pirard, Mechele, Peeters, Gerkens, Bagayoko/Dussaut dk63, Janssens/Boli dk45, Kotysch, Valdivia, Fernandes, Vetokele na Bolingoli/Ceballos dk45.

SIMBA KURUDI KILELENI LIGI KUU LEO?
SIMBA
SC itajaribu kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
wakati itakapomenyana na Prisons ya Mbeya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
leo.
Timu hiyo ya kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog itaingia kwenye mchezo wa leo ikihitaji ushindi tu ili kurejea kileleni mwa Ligi Kuu.
Na hiyo ni kwa sababu wapinzani wao katika mbio za ubingwa, Yanga SC hawatakuwa na mechi ya Ligi Kuu wikiendi hii kwa kuwa wamekwenda Comoro kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Na wakitoka kushinda 3-0 ugenini katika mechi iliyopita ya Ligi Kuu dhidi ya wenyeji Maji Maji mjini Songea, Simba wanajamini kabisa leo wataendeleza wimbi la ushindi.
Na bila shaka, kocha Omog anayesaidiwa na Mganda, Jackson Mayanja leo ataendelea kupanga safu kali ya ushambuliaji ya wakali watatu, Juma Luizio, Ibrahim Hajib na Mrundi Laudit Mavugo.
Kwa ujumla Omog hatarijiwi kufanya mabadiliko makubwa kutoka kikosi kilichoifunga 3-0 Maji Maji Jumamosi Uwanja wa Maji Maji, Songea.
Na bila shaka langoni ataendelea kusimama Mghana Daniel Agyei, akisaidiwa na beki Mkongo Janvier Bokungu kulia, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kushoto na katikati Mzimbabwe Method Mwanjali na Novatus Lufunga.
Viungo wanaweza kuendelea kucheza Muzamil Yassin, Said Ndemla na Shizza Kichuya. Simba SC inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 48 baada ya kucheza mechi 21, ikiwa nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga wenye poinyi 49 za mechi 21.

Pamoja na kutofanya vizuri katika msimu uliopita, Manchester United imeshika namba moja katika mauzo ya jezi baada ya kuuza zaidi ya jezi milioni 2.8.
Mauzo ya jezi kwa mwaka 2016 yameshikwa na Man United huku wakifuatiwa na Real Madrid ya Hispania iliyouza zaidi ya jezi milioni 2.2.
FC Barcelona ya Hispania pia, imeuza jezi milioni 1.9 na kufuatiwa na Chelsea Chelsea iliyouza jezi milioni 1.6.
LISTI YA KLABU ZILIZOUZA SANA
1) Manchester United (2,850,000)
2) Real Madrid (2,290,000)
3) Barcelona (1,980,000)
4) Chelsea (1,650,000)
5) Bayern Munich (1,500,000)
6) Arsenal (1,225,000)
7) Juventus (850,000)
8) Liverpool (705,000)
9) Paris Saint-Germain (685,000)
10) AC Milan (650,000)
Jumatano, 18 Januari 2017
november 30/12
MAFUNZO YA VITENDO YAWA FURAHA KWA WANAFUNZI VYUONI
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha,wakiwa katika mafunzo ya vitendo wakiwa darasani.
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wametakiwa kujifunza masomo yao kwa vitendo ili kuongeza maarifa zaidi na kuleta ushindani katika soko la ajira pindi watakapoajiriwa.
Hayo yamesemwa na mkufunzi wa chuo hicho Bw;Steven Mulaki alipokuwa akihojiwa na SPIRITMWAMBA mapema leo mchana alipokuwa akiwafundisha wanafunzi wa darasa la Mt Ordizungwa.
Bw Mulaki ameongeza kwa kusema kuwa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wa vyuoni ni muhimu kwa kuwa watakapohitimu masomo yao itawasaidia kupata uzoefu watakapoajiriwa na taasisi au makampuni mbalimbali
Kwa upande wa wanafunzi wamefurahishwa na mafunzo hayo ambapo wengi wao wamemsifu mkufunzi huyo kwa kufundisha vizuri.

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Singida Afariki Dunia, Mwili Kuagwa Leo Saa 11 Jioni Muhimbili
Aliyekuwa
Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi (SACP) EX Peter Kakamba amefariki dunia alfajiri ya tarehe
30/11/2016 katika hospital ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa
matibabu.
Kakamba
alizaliwa mwaka 1963 katika kijiji cha Kawajense Wilayani Mpanda, mkoa
wa Katavi. Alisoma shule ya msingi Shanwe Kawajense mwaka 1973 hadi
1980, Kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari
Kantalamba mwaka 1981 hadi 1984 ambapo kidato cha tano na sita alisoma
katika shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro mwaka 1985 hadi 1987.
Mwaka 1992 hadi 1994 alisoma Astashahada ya Sheria katika Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam.
Marehemu
alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1988 ambapo katika utumishi wake
alipandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Konstable wa Polisi (1989), Sagenti
wa Polisi (1991), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1997), Mkaguzi wa Polisi
(2003), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (2006), Mrakibu wa Polisi (2008),
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2011), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2015)
na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2016).
Baadhi
ya nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa Mwendesha Mashtaka wa
Polisi katika mkoa wa Iringa, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, Afisa
mnadhimu wa Polisi katika Mikoa ya Iringa na Geita, Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Iringa na mpaka anafariki alikuwa Kamanda wa Polisi katika mkoa
wa Singida.
Kufuatia
kifo hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu anatoa pole
kwa Maofisa, Wakaguzi,Askari, ndugu, jamaa na marafiki kwa Msiba huo.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa,
Jina la Bwana lihimidiwe - Amen.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
Alhamisi, 12 Januari 2017
michezo alhamisi hii
TIMU YA BARCELONA YATINGA ROBO FAINALI YA COPA DEL REY
Luis Suarez amefunga goli la 100
katika michezo 120 akiwa na Barcelona wakati timu hiyo ikitinga robo
fainali ya Copa del Rey kwa kuifunga Athletic Bilbao magoli 3-1.
Suarez alifunga goli katika kipindi
cha kwanza kufuatia krosi ya Neymar, na katika kipindi cha pili
Neymar akafunga goli la pili kwa mkwaju wa penati.
Athletico Bilbao walipata goli pekee
lililofungwa na kichwa na mshambulia Saborit, hata hivyo Lionel Messi
aliipatia Barcelona goli la tatu kwa shuti la mpira wa adhabu.
Luis Suarez akimalizia vyema mpira wa krosi iliyopigwa na Neymar
Lionel Messi akipiga mpira wa adhabu ulioenda kujaa wavuni na kuipatia ushindi Barcelona
SOUTHAMPTON YAITUNGUA LIVERPOOL GOLI MOJA BILA MAJIBU
Timu ya Southampton imeanza vyema
mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya kombe la EFL, kwa kupata ushindi
inaostahili wa goli 1-0 didi ya Liverpool katika dimba la St Mary.
Goli la Southampton lilimaliziwa
vyena na Nathan Redmond akipokea pasi ya Jay Rodriguez, na kuipatia
ushindi muhimu kabla ya mchezo wa marudiano Anfield Januari 25.
Nathan Redmond akijipinda na kuachia shuti lililojaa wavuni
Nathan Redmond akishika kichwa baada ya kukosa nafasi ya kufunga goli la pili
Diamond akabidhiwa bendera ya taifa kuliwakilisha taifa AFCON 2017 nchini Gabon
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye
(kushoto) akimkabidhi bendera ya Taifa Mwanamuziki wa bongo fleva Nasib
Abdul maarufu kama Diamond Platinumz kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha
Tanzania kwenye Ufunguzi wa Mashindano ya AFCON 2017 yanayotarajiwa
kufanyika nchini Gabon.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye akiongea
na wageni waalikwa pamoja na Waandishi wa Habari wakati wa hafla ya
kumkabidhi bendera ya Taifa mwanamuziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul
maarufu kama Diamond Platinumz anayekwenda kushiriki katika Ufunguzi wa
Mashindano ya AFCON 2017 yanayotarajiwa kufanyika nchini Gabon. Hafla
hiyo imefanyika leo 11 Januari, 2017 Hoteli ya Serena Jijini Dar es
Salaam.
Wageni
waalikwa pamoja na Waandishi wa Habari wakifuatilia hotuba ya Waziri
Nape Nnauye wakati wa hafla ya kukabidhi bendera ya Taifa kwa
mwanamuziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz
iliyofanyika leo 11 Januari, 2017 Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa DSTV Multi Choice Tanzania Bw. Salum Salum akiongea na Waandishi wa
Habari pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kukabidhi bendera ya
Taifa kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond
Platinumz anayekwenda kushiriki katika Ufunguzi wa Mashindano ya AFCON
2017 yanayotarajiwa kufanyika nchini Gabon.
Balozi
wa DSTV Bomba Bw. Lucas Mhuvile maarufu kama Joti akiongea na Waandishi
wa Habari pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kukabidhi
bendera ya Taifa kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul maarufu kama
Diamond Platinumz iliyofanyika leo 11 Januari, 2017 Hoteli ya Serena
Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye,
Mkurugenzi wa DSTV Multi Choice Tanzania Bw. Salum Salum pamoja na
mwanamuziki wa bongo fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz
wakiteta jambo kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhi bendera ya Taifa
kwa mwanamuziki huyo anayekwenda kushiriki katika Ufunguzi wa Mashindano
ya AFCON 2017 yanayotarajiwa kufanyika nchini Gabon.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye
(katikati) akimpongeza mwanamuziki wa bongo fleva Nasib Abdul maarufu
kama Diamond Platinumz wakiteta jambo kabla ya kuanza kwa hafla ya
kukabidhi bendera ya Taifa kwa mwanamuziki huyo anayekwenda kushiriki
katika Ufunguzi wa Mashindano ya AFCON 2017 yanayotarajiwa kufanyika
nchini Gabon. Anayeshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa DSTV Multi Choice
Tanzania Bw. Salum Salum
Mwanamuziki
wa bongo fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz akimshukuru
Waziri Nape Nnauye pamoja na Serikali kwa ujumla kwa mchango mkubwa
inaotoa katika kukuza sekta ya Sanaa nchini wakati wa hafla ya kukabidhi
bendera ya Taifa kwa mwanamuziki huyo anayekwenda kuiwakilisha Tanzania
kwenye Ufunguzi wa Mashindano ya AFCON 2017 yanayotarajiwa kufanyika
nchini Gabon.iliyofanyika leo 11 Januari, 2017 Hoteli ya Serena Jijini
Dar es Salaam.
Jisajili kwenye:
Maoni (Atom)