AJTC VOICE FO VOICLESS

Jumanne, 27 Desemba 2016

JUMANNE

jumanne hii

...... PLAZA.jpgJEMBE1.jpg

 

Jumanne, 27 Desemba 2016

JOSE MOURINHO ASIFIA GOLI TAMU LA HENRIKH MKHITARYAN

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amepongeza goli zuri lililofungwa kwa mpira wa kisigino kwa nyuma na Henrikh Mkhitaryan katika mchezo walioibuka na ushindi dhidi ya Sunderland katika dimba la Old Trafford.

Mkhitaryan alifunga goli hilo lililozua utata kutokana na kuwa alikuwa ameotea akipokea pasi kutoka kwa Zlatan Ibrahimovic na kufanya matokeo ya mchezo huo kuwa Manchester 3-1 Sunderland.

Mkhitaryan mwenyewe amesema goli hilo ni goli zuri kuwahi kufunga katika maisha yake ya soko, na kuongeza kuwa hayo yalikuwa ni mazingaumbwe madogo ya kipindi cha Sikukuu ya Krismasi.

MANCHESTER CITY YAKWEA HADI KATIKA NAFASI YA PILI KATIKA LIGI KUU YA UINGEREZA

Timu ya Manchester City imekwea hadi nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Hull City wakiwa ugenini katika dimba la KCOM.

Kikosi cha Pep Guardiola kilipata ushindi wake wa 12 katika msimu huu, na kuwa nyuma kwa pointi saba dhidi ya vinara timu ya Chelsea.

Yaya Toure alifunga goli la kwanza kwa mkwju wa penati katika kipindi cha pili, baada ya Raheem Sterling kuchezewa rafu, Kelechi Iheanacho akafunga la pili na Curtis Davies kujifunga la tatu.
                                                          Yaya Toure akifunga goli kwa mkwaju wa penati
                                       Kelechi Iheanacho akifunga goli la pili la Manchester City 
    Curtis Davies akijifunga wakati akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na Raheem Sterling 
 
 

NAHODHA YANGA ASEMA SIMBA WANAONGOZA TU LIGI, UBINGWA BADO SANA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannaavaro’ amesema kwamba ni mapema mno kuiondoa Yanga kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online juzi, Cannavaro alisema kwamba baada ya Yanga kulazimishwa sare ya 1-1 African Lyon watu wengi wanaelekea kukata tamaa kama timu hiyo inaweza kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu. Cannavaro alisema watu wanaoikatia tamaa Yanga wakati huu lazima watakuwa wageni wa Ligi, kwani kwa uzoefu anaamini ligi bado mchichi.
“Simba wametupita pointi nne, ambazo ni sawa na wastani wa mechi mbili na bado hawajacheza na sisi. Wakicheza na sisi tukawafunga, inabaki pointi moja, na wakitoa hata sare mechi nyingine watapoteza pointi mbili na sisi tutawapita,”alisema. Cannavaro alisema kwamba wachezaji wa Yanga kwa ujumla waliumizwa na sare ambayo hawakuitarajia dhidi ya Lyon, lakini sasa wanaelekeza nguvu zao katika mechi zijazo. “Kwa sasa hivi tunaelekeza nguvu zetu kwenye mchezo wetu ujao na Ndanda, tunahitaji kushinda kwanza ili kurejesha imani za mashabiki wetu na baada ya hapo tuendelee kupambana huku tukitazam na spidi ya wapinzani wetu (Simba) katika mbio za ubingwa,”alisema Cannavaro. Aidha, Nahodha huyo amewataka mashabiki, wapenzi na wanachama wa Yanga kuwa wavumilivu na wenye subira katika kipindi hiki na kushikamana na wachezaji wao ili kuwatia moyo wafanye vizuri.
 

SAMATTA ASIKITIKA KUFUKUZWA KWA KOCHA ALIYEMSAJILI GENK

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amesikitishwa na klabu yake, KRC Genk kumfukuza kocha Mbelgiji Peter Maes. Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online leo kwa simu kutoka Ubelgiji, Samatta amesema kwamba amesikitishwa na taarifa hizo, lakini hana namna nyingine zaidi ya kukubali matokeo. "Siyo taarifa nzuri kwa mtu ambaye alitokea kuniamini kwa muda mfupi, lakini hakuna chaguo zaidi ya kuendelea kujituma na kuwa bora zaidi, ili kumpendeza kocha atakayekuja,"amesema Samatta.
Akimzungumzia zaidi Maes, Nahodha huyo wa Tanzania alisema; "Alikuwa kocha kocha mzuri, aina ya ufundishaji wake ulikuwa wa moja kwa moja na alikuwa rafiki kwa kila mchazaji,". Genk imemfukuza rasmi Maes leo baada ya matokeo mabaya ya hivi karibuni na kuelekea mchezo wa kesho, aliyekuwa Msaidizi wake, Rudi Cossey ataiandaa timu.  Maes ndiye aliyemsajili Samatta Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na akamuamini haraka na kumpa nafasi kwenye kikosi cha kwanza. Chini ya Maes, Samatta amecheza mechi 35 Genk,18 msimu uliopita na 17 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 17 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na saba msimu huu. Mechi 18 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 10 msimu huu, wakati nane hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na mbili msimu huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao tisa, manne msimu huu na matano msimu uliopita. Maes alijiunga na Genk msimu wa 2015-2016 kutoka KSC Lokeren na ameiongoza timu hiyo katika mechi 81 rasmi. Genk kesho itacheza na KAA Gent ikiwa chini ya kocha wa muda, Mbelgiji pia, Rudi Cossey na klabu imemshukuru Peter Maes kwa kazi yake nzuri kwa kipindi chote alichokuwa na timu na kumtakia kila la heri aendako.
 
 

SIMBA KUMALIZANA NA NDUSHA, ANGBAN JUMATANO

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM SIMBA SC imesema kwamba hadi kesho itakuwa imekwishawalipa kipa Vincent Angban na kiungo Mussa Ndusha ili waondoke Alhamisi kuerejea kwao. Angban kutoka Ivory Coast na Ndusha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wote wameachwa Simba SC katika dirisha dogo mwezi huu, kufuatia kusajili kwa Waghana, kipa Daniel Agyei na kiungo James Kotei. Baada ya kusitishiwa mikataba, wawili hao wanapaswa kulipwa na Simba SC kulingana na vipengeel vya mikataba yao. Na akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online leo, Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele amesema kwamba klabu haina tatizo na wachezaji hao na tayari wamefikia makubaliano juu yaa namna ya kumalizana.
Mussa Ndusha (kushoto) aliichezea Simba mara ya mwisho ikifungwa na Mtibwa Sugar 2-1 Desemba 12, mwaka huu
Kahemele alisema kwamba wachezaji wote hao wana uelewa mzuri na wanaielewa vizuri mikataba waliyosaini kujiunga na Simba, hivyo hakuna tatizo lolote baina yao. “Hatuna tatizo nao kabisa, tumezungumza nao vizuri na tumefikia makubaliano kwamba tutakuwa tumekwishamalizana nao hadi kufika Jumatano (kesho) ili Alhamisi waondoke,”alisema. Aidha, Kahemele alisema wanauheshimu na kuuthamini mchango wa wachezaji hao kwa kipindi cha kuitumikia Simba na wanawatakia kila laa heri waendako. Wakati huo huo: Kikosi cha Simba jana kimeendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting Alhamisi wiki hii. Kahemele alisema kwamba timu imeweka kambi hoteli ya Spiece, Mnazi Mmoja mjini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo huo.  “Tangu tutoke Mtwara tuliweka kambi Spiece na tutaendelea kuwa hapo hadi baada ya mchezo huu na Ruvu Shooting tutakapokwenda Zanzibar kwenye Kombe la Mapinduzi,”alisema Kahemele. Simba SC imeuanza vyema mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kushinda mechi mbili mfululizo za mwanzo na kuzidi kupaa kileleni. Wekundu hao wa Msimbazi walianza kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara kabla ya kuilaza 1-0 JKT Ruvu katikaa mchezo uliofuata Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Matokeo hayo yanawafanya Wekundu wa Msimbazi wafikishe pointi 41 baada ya mechi 17, wakiwazidi kwa pointi nne, mabingwa watetezi, Yanga wanaofuatia katika nafasi ya pili kwa pointi zao 37. 

Jumatatu, 26 Desemba 2016

JUM,ATATU

umatatu, 26 Desemba 2016

HABARI ZA JUMATATU HII


Seebait.com 2016

.
.

Monday, 26 December 2016


Magufuli awataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Misa ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.
Hapa wakiwa katika sala.
Rais Magufuli na mkewe wakisilkiliza neno

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo mkoani Singida

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda akimuombea na kumbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakisalimiana na waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya ibada ya Krismasi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipunga mkono wakati wakitoka kwenye Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii kama ilivyokuwa kwa Yesu Kristo ambaye alikuwa chini ya malezi ya fundi seremala.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
Rais Magufuli ametoa rai hiyo (jana) katika Kanisa la Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu mjini Singida katika kuadhimisha Sikukuu ya Krismasi ambayo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
“Katika kipindi cha maisha yake Yesu Kristo hapa duniani, mbali ya kwamba alizaliwa na mfanyakazi, Joseph seremala, lakini na yeye alishiriki katika kufanya kazi, basi niwaombe watanzania wote tuchape kazi kwelikweli kwa sababu hakuna cha bure,” alisema Rais Magufuli. 
Pia amewataka watanzania kuimarisha upendo, kuvumiliana, na kutobaguana, kwani upendo utalisaidia taifa kupata maendeleo huku akiwakumbusha waumini kuwa Yesu Kristo hakuwa CHADEMA wala CCM bali alikuwa ni wa watu wote.
Rais Magufuli ambaye aliambatana na mkewe Mama Janeth Magufuli, katika ibada hiyo amesema, kusali ni moja ya nguzo muhimu ambayo Wakristo wote wanapaswa kutekeleza ili kuhakikisha taifa linaendelea kubakia katika hali ya amani na utulivu ambayo ndiyo msingi wa maendeleo.
Aidha, Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wakulima kote nchini kuhakikisha wanazitumia vizuri mvua za sasa katika shughuli za kilimo pamoja na kulima mazao yanayostahimili ukame

Monday, December 26, 2016


Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu ya Disemba 26



Monday, December 26, 2016


Picha 15: Vodacom Wasafi Festival Ilivyofanyika Dec 25 Mkoani Iringa

Usiku wa Dec 25, 2016  wakali wa Bongo Fleva akiwemo Diamond Platnumz, Harmonize, Rayvanny, Queen Darleen, Q Boy, Chege pamoja na msanii kutoka Nigeria Kcee wameandika historia katika mkoa wa Iringa.


Show hiyo iliyopewa jina la Vodacom Wasafi Festival imefanyika katika uwanja wa Samora Stadium, hizi ni baadhi ya picha kutoka mahali palipofanyika tamasha hilo.

Monday, December 26, 2016


Michezo: Haji Manara Amuombea Msamaha Jerry Muro Kwa Rais Wa TFF

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Sunday Manara amejitokeza kwa mara ya kwanza kumuombea msamaha mtani wake Jerry Muro ili kuifufua upya hamasa na kuongeza ushindani katika ulimwengu wa soka la Bongo.

Jerry Muro ambaye ni Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga amefungiwa na TFF kwa muda wa mwaka mmoja kutojihusisha na soka kutokana na matumizi mabaya ya kauli zake kupitia vyombo vya habari mwezi Julai mwaka huu.

Manara katika ujumbe aliouweka kwenye mtandao wake wa Instagram akiuelekeza kwa Rais wa TFF Jamal Malinzi, amesema katika kuadhimisha sikukuu ya Krismasi anaona ni wakati muafaka sasa kwa Rais Malinzi kutumia mamlaka yake kumfungulia Jerry kwa kuwa amekwishatumikia takriban nusu ya kifungo chake na kwamba soka la Bongo linamuhitaji sana kwa sasa.

"Nimekaa nimetafakari sana,nimeamua kumuombea msamaha mtani wangu Jerry Muro ambaye TFF mlimfungia mwaka mmoja kujihusisha na mpira wa miguu, ninafanya hivi nikijua kabisa Jerry alikosea na tayari ameshatumikia karibia nusu ya kifungo chake, ninajua kwa kufanya hivyo atakuwa keshajifunza lugha za kutumia na pia itakuwa fundisho kwetu sisi wasemaji na viongozi wa vilabu kwa ujumla. "Ameandika Manara

Manara pia hakusita kukumbushia jinsi ambavyo Jerry Muro amewahi kumtolea hata yeye mwenye lugha za kuudhi "
Nnafahamu pia Jerry aliwahi kunitolea lugha zisizostahili mimi bnafsi, lakini yale yashapita na binafasi amenihakikishia kutorudia tena, na nnaamini viongozi na washabiki wa Simba watanielewa dhamira yangu hii njema, ambayo inathibitisha uungwana tulio nao wanasimba".

manara amemaliza kwa kusema kuwa soka la Tanzania linammis sana Jerry Muro na kuomuomba Rais Malinzi kutumia mamlaka yake kumfungulia kwa kuwa Jerry bado alikuwa hajawa na uzoefu wa kutosha katika siasa za mpira.

Kwa upande wake Jerry Muro amefurahi na kushukuru kuona mtani wake Haji Manara anamkumbuka na kutumia fursa hiyo kuomba msamaha kwa shirikisho la soka Tanzania ili aendeleze hamasa ya soka aliyokuwa ameiweka nchini yeye na Haji Manara.

Monday, December 26, 2016


Rais Magufuli Atoboa Siri ya Kula Christmass Mkoani Singida

Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli,amefichua siri ya kusali Krismasi kwenye kanisa la Parokia ya Moyo wa Yesu, mjini Singida mwaka huu.

Ametaja siri hiyo kuwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, aliwahi kusali kwenye kanisa hilo na wakati akitoka, alikutana na sista mmoja (hamkumbuki jina) ambaye alimzawadia rozali, na kumwahidi kuwa itamsadia kushinda uchaguzi huo.

Rais Magufuli ametoa siri hiyo jana  wakati akizungumza kwenye sherehe ya Krismasi iliyofanyika kwenye kanisa la Porokia ya Moyo wa Yesu, na kuhudhuriwa pia na mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli.

Akifafanua, alisema kuwa rozali hiyo amezunguka nayo kwenye kampeni yake, na mwisho wa siku, alifanikiwa kupata kura za kutosha na hivyo kuwa mshindi.

“Hiyo ndio sababu kubwa au siri ya mimi kufika mjini Singida, na kuungana na wakazi wa mkoa wa Singida na Watanzania kwa ujumla, kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu kristo,” alisema na kusababisha mamia ya waumini kushangilia kwa nguvu.

Rais Magufuli alitumia fursa hiyo kuwataka Watanzania wote kutumia sikukuu hii ya Krismasi kuimarisha upendo, kuvumiliana na wala wasibaguane ,na kwa njia hiyo,Tanzania itaendelea kupaa kimaendeleo.

Katika hatua nyingine, alisema kuwa Watanzania na hususani wakulima, wahakikishe wanazitumia vizuri mvua zinazonyesha kwa sasa nchini kwa kuchapa kazi ya kilimo kwa nguvu zote na kulima mazao yanayostahimili ukame.

“Ndugu zangu waumini na Watanzania kwa ujumla, acheni kulialia kuwa fedha zimepotea … fedha hazijapotea isipokuwa ninyi wenyewe hamfanyi kazi. Vitabu vyote vya madhehebu ya dini vinasisitiza wajibu wa kuchapa kazi … na vinasema asiyefanya kazi na asile,” alisisitiza.

Akiijengea nguvu hoja yake ya hapa ni kazi tu, alisema kuwa Yesu kristo amezaliwa na fundi mchapa kazi kweli kweli seremala, na hivyo tunaposherehekea Krismasi Watanzania wote wenye uwezo wa kufanya kazi, wafanye kazi huku wakijua hakuna cha bure.

Aidha, Rais Magufuli, aliwataka wakazi wa mkoa wa Singida, kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti, ili kukiwezesha kiwanda kikubwa cha kukamua mafuta ya alizeti cha Mount Meru kupata mbegu za kikudhi mahitaji ya kiwanda.

Awali askofu wa kanisa katoliki jimbo la Singida, Edward Mapunda, alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wakazi wa mkoa wa Singida, kutunza mazingira, ili yaweze kuwatunza na wao.

Alisema hivi sasa hali ni mbaya kutokana na binadamu kuongeza kasi ya kuharibu mazingira, kitendo kinachochangia madhara mengi ikiwemo uhaba wa mvua.

“Mimi nashangaa sana, watu wanaendelea kuzaa huku wakiendelea kuharibu mazingira na kutishia nchi kuwa jangwa. Tuna zaa watoto waje wateseke kutokana na uharibifu wa mazingira. Kama tunaendelea kuharibu mazingira, ni vema tuache kuzaa”, alisema Mapunda.

Monday, December 26, 2016


Michezo: Ratiba ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza Disemba 30

Pazia la Mashindano ya Kombe la Mapinduzi linatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake Disemba 30, 2016 katika uwanja wa Amaan saa 2:15 Usiku ambapo kutakuwa na mchezo wa Derby ya Jangombe kati ya Taifa ya Jangombe na Jangombe Boys ambapo mashindano ya msimu huu yameshirikisha vilabu 9, vitano vikitokea Zanzibar, vitatu Tanzania bara na kimoja kutaka Uganda ambao ndio mabingwa watetezi timu ya URA.
 
KUNDI A: Simba, URA, KVZ, Taifa ya Jangombe na Jangombe Boys.
 
KUNDI B: Yanga, Azam, Zimamoto na Jamhuri.
 
RATIBA KAMILI YA MAPINDUZI CUP
30/12/2016 Taifa ya Jang’ombe vs Jang’ombe boys saa 2:30 usiku.
 
1/1/2017 KVZ VS URA Saa 10:00 alasiri, Simba vs Taifa ya Jang’ombe saa 2:30 usiku.
 
2/1/2017 Azam vs Zimamoto saa 10:00 alasiri, Yanga vs Jamhuri saa 2:30 usiku.
 
3/1/2017 Jang’ombe boys vs URA saa 10:00 alasiri, KVZ vs Simba saa 2:30 usiku.
 
4/1/2017 Zimamoto vs Yanga saa 10:00 alasiri, Jamhuri vs Azam saa 2:30 usiku.
 
5/1/2017 KVZ vs Jang’ombe boys saa 10:00 alasiri, Simba vs URA saa 2:30 usiku.
 
6/1/2017 Taifa ya Jang’ombe vs KVZ saa 2:30 usiku.
 
7/1/2017 Jamhuri vs Zimamoto saa 10:00 alasiri, Yanga vs Azam saa 2:30 usiku.
 
8/1/2017 Simba vs Jang’ombe boys saa 10:00 alasiri ,Taifa ya jang’ombe vs URA 2:30 usiku.
 
10/1/2017 Saa 10: 00 nusu fainali ya kwanza , Saa 2:30 nusu fainali ya pili.
 
13/1/2017 Fainali saa 2: 30 usiku.



Monday, December 26, 2016


Michezo: TFF Yasema Mechi ya Simba na Yanga iko palepale

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa mechi ya ligi kuu Tanzania Bara ya mzunguko wa pili kati ya Simba na Yanga iliyokuwa imepangwa kuchezwa Februari 18 mwaka 2017 iko palepale kwa kuwa bado halijafikiria kuibadili tarehe hiyo.

Hatua hiyo inatokana na tarehe hiyo kugongana na kalenda ya CAF ya michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika iliyotolewa hivi karibuni na kuipanga Yanga kucheza mchezo wa marudiano kati yake na Ngaya de Mbe ya Comoro kati ya tarehe 17, 18 na 19 mwezi Februari 2017.

Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas amesema kuwa hadi sasa shirikisho hilo kupitia Bodi ya Ligi halijafikiria kufanya mabadiliko yoyote kwenye ratiba hiyo, na kwamba ratiba itaendelea kubaki kama ilivyo hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.

"Ratiba imeshapangwa na haitabadilika, kila timu inajua itacheza lini, kuhusu ratiba ya CAF haiwezi kutuzuia kufanya mashindano yetu, kama kuna timu inacheza CAF inatakiwa ijipange, kila timu inatakiwa kuwa tayari wakati wowote ndiyo maana zinafanya matayarisho, zinaajiri makocha, zinasajili wachezaji , hiyo yote ni matayarisho kwahiyo sidhani kama watahitaji kupumzika na kutuharibia ratiba" Amesema Lucas

Jumatatu iliyopita Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi Boniface Wambura akiwa kwenye kipindi cha 5Sports cha EATV, alisisitiza kuwa katika mzunguko wa pili wa ligi, ratiba haitakuwa tatizo, na kwamba haitabadilishwa badilishwa kwa kuwa katika upangaji wake kila kitu kilizingatiwa ikiwemo kalenda ya CAF.

Jumatatu, 26 Desemba 2016


MAN UNITED YAPATA USHINDI WA NNE MFULULIZO LIGI KUU YA UINGEREZA

Manchester United imepata ushindi wa nne mfululizo wa Ligi Kuu ya Uingereza katika mchezo walioutawala dhidi ya Sunderland inayobakia katika mstari wa kushuka daraja baada ya kulala kwa magoli 3-1.

Manchester United iliyostahili ushindi iliutawala mchezo huo kwa asilimia 63, ilipiga mashuti 25 kwenye goli, lakini zilikuwa jitihada za beki Daley Blind zilizozaa matunda na kuipatia goli la kwanza kufuatia pasi ya Zlatan Ibrahimovic.

Katika kipindi cha pili Zlatan Ibrahimovic aliongeza goli la pili akinasa pasi ya Paul Pogba huku Henrikh Mkhitaryan aliyetokea benchi akifunga goli la kisigino licha ya kuonekana ameotea.
                     Zlatan Ibrahimovic akianza kushangilia goli wakati mpira ukielekea wavuni
                          Mchezaji raia wa Armenia Henrikh Mkhitaryan akifunga goli kwa kisigino

OLIVER GIROUD AIPATIA ARSENAL USHINDI KATIKA DAKIKA ZA MWISHO

Mshambuliaji wa Arsenal Oliveir Giroud amefunga goli la ushindi katika dakika za mwisho na kumaliza gundu la kufungwa michezo miwili ya Ligi Kuu ya Uingereza kwa ushindi dhidi ya West Brom.

Giroud alianza kwa mara ya kwanza katika kikosi cha kwanza katika msimu huu, na alifanikiwa kufunga kwa mpira wa kichwa akiunganisha krosi ya Mesut Ozil katika dakika ya 86 ya mchezo huo.

Hadi Arsenal inapata goli hilo ilikuwa inaongoza kwa kumiliki mpira kwa asilimia 80, lakini ilikuwa na wakati mgumu kufanikiwa kutikisa nyavu za West Brom kazi kubwa akifanya kipa Ben Foster.
                     Olivier Giroud akiwa ameupiga mpira kwa kichwa uliozaa goli pekee 
Aaron Ramsey akishangilia kuona mpira wa kichwa uliopigwa na Giroud ukitinga wavuni

RC GAMBO AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI ARUSHA



Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa wa Arushaa ofisini kwake juzi kutoka vyombo mbalimba vya habari kuhusu sakata la kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha ITV Halfani Liundi ambapo amehaidi kulishughulikia huku akiwataka waandishi kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari


Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu mwandishi wa kituo cha ITV Halfani Liundi aliyekamatwa hivi karibuni na jeshi la polisi, ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa anatambua umuhimu wa vyombo vya habari na hivyo mwandishi anauhuru wa kwenda popote kupata taarifa yeyote kwa kuzingatia misingi ya uandishi wa habari


Mwandishi wa habari wa kituo cha channel Ten Aristrides Dotto akichangia katika mkutano huo wa waandishi wa habari na mkuu wa Mkoa juzi ofisinii kwake jijini Arusha


                                         Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia mkutano huo


Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Mosses Mashalla akichangia katika mkutano huo wa mkuu wa Mkoa na waandishi wa habari mkoa wa Arusha. (Picha zote na Pamela Mollel)

Jumatatu, 26 Desemba 2016


MWANAFUNZI ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUCHALANGWA MAPANGA NA MWALIMU

Mwanafunzi Marco Limbe akiwa amelazwa baada ya kushambuliwa kwa panga na Mwalimu Pendo Gabriel
Mwalimu Pendo Gabriel akiwa naye amelazwa baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira


Na Shushu Joel, BUSEGA



MWANAFUNZI Marco Limbe(14) aliyemaliza darasa la saba mwaka huu katika shule ya msingi Yitwimila iliyoko kata ya kiloleli wilaya ya Busega mkoani Simiyu amelazwa katika kituo cha afya Busega mara baada ya kuchalangwa mapanga kichwani na mdomoni na mwalimu wake.



Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11.30 jioni wakati mwanafunzi huyo alipokuwa akirejea nyumbani kwao akitokea katika malisho ya mifugo ndipo alipokaribia katika shamba la mwalimu Pendo Gabriel ndipo mwalimu huyo alimkamata kijana huyo na kuanza kumchalanga kwa panga na kupelekea kijana limbe kupoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 mara baada ya kufikishwa katika kituo cha afya Busega.



Shuhuda wa tulio hilo aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Manoga anaeleza kuwa ilikuwa kama mchezo lakini kumbe ni kweli kwani niliona mifugo ya limbe iliyokuwa ikielekea nyumbani na huku limbe akiwa nyuma ya mifugo hiyo katika barabara ambalo liko karibu na maeneo ya shule ghafla nilimuona mwalimu pendo wakishikana na kijana huyo na ndipo nikamuona akiwa na panga na kuanza kumchalanga”



Nilikimbia katika tukio na kutoa msaada kwa wote lakini mara watu walijaa na kuanza kumshambua mwalimu Pendo kwa kumpiga ingawa jaribio hilo lilikwama mara baada ya mwenyekiti wa kijiji hicho mshemas bahai.



Mwandishi alikwenda katika kituo cha afya cha Nyashimo na kujionea hali mbaya kwa kijana Limbe ambaye alikuwa amepoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 bila kujitambua na huku akiwa anaongezewa drip na kwa pembeni mwalimu Gabriel naye akipata matibabu ya jeraha lake kichwani amabolo alishambuliwa na wananchi na huku akiwa chini ya ulinzi wa jeshi la piolisi.



Akithibitisha kutokea kwa tukio mwenyekiti wa Sogesca Bahai Mshemas alisema kuwa sikukuu ya kuzaliwa kwa yesu imekuwa ni mbaya katika kijiji chake mara baada ya wananchi walio na hasira kali kufanya shambulio la kumshambulia mwalimu Pendo kwa kosa la kumchalanga na panga mwanafunzi wake aliyekuwa akitokea kwenye malisho na kupita karibu na shamba lake la mahindi.



Aliongeza kuwa alifanikiwa kuwatuliza wananchi wa kijiji chake na kuanza kufanya mikakati ya kuwapeleka kituo cha afya ili wapate huduma za matibabu.



Aidha Mshemasi aliongeza kuwa walifika polisi na kuandikiwa barua ya kwenda kutibiwa wote wawili mwalimu pamoja na mwanafunzi.



Kwa upande wake kaimu mganga mfawidhi wa kituo hicho cha afya Dk Ayubu Ismail alithibitisha kuwapokea kwa majeruhi hao na kudai kuwa kijana limbe ndiye aliyekuwa na hali mbaya zaidi kuliko mwalimu pendo.



Aliongeza kuwa kijana ameshonwa nyuzi 9 katika sehemu zake zote alizopatwa na majeraha na huku mwalimu yeye akiwa ameshonwa nyuzi 6.



ni kweli Limbe alikuwa ametokwa na damu nyingi sana na hivyo kumpelekea kupoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 lakini hali yake inaendelea vizuri alisema Dk Ismail”

NYOTA WA POP GEORGE MICHAEL AFARIKI DUNIA



Mwanamuziki nyota wa muziki wa Pop George Michael amefariki dunia jana baada ya moyo wake kushindwa kufanya kazi akiwa nyumbani kwake huko Oxfordshire Uingereza.
Mwanamuziki huyo aliyeanza muziki katika miaka 80, na kupata mafanikio zaidi akiimaba peke yake nje ya bendi, amefariki dunia kwa amani jana siku ya Krismasi, kwa mujibu wa msemaji wake.


Mwanamuziki mwenzake wa zamani wa bendi ya Wham! Andrew Ridgeley amesema amevunjika moyo kuwa kumpoteza rafiki yake kipenzi.
           George Michael akiwa na Andrew Ridgeley wakiimba pamoja na bendi ya Wham !
Picha hii inaaminika kuwa ni picha ya mwisho kupiga George Michael hii ilikuwa Septemba mwaka huu akipata mlo wa usiku na rafiki yake
                                  Pata wimbo maarufu wa George Michael wa Careless Whisper

 
https://youtu.be/izGwDsrQ1eQ

habari za kimataifa


Wazamiaji wa Urusi wamepata mabaki ya ndege ya kijeshi iliyoanguka katika bahari nyeusi ikiwa na watu 92. Mabaki ya ndege hiyo yako katika kina cha mita 27 sawa na maili moja kutoka usawa wa bahari , amesema Rimma Chernova , msemaji wa operesheni ya msako na uokozi iliyoko mjini Sochi ikiongozwa na wizara ya masuala ya dharura ya Urusi. Mashirika ya habari ya Urusi hapo kabla yalimnukuu afisa ambaye hakutajwa akisema kwamba sehemu ya mbele ya ndege hiyo imepatikana, taarifa ambayo maafisa wa mji huo hawakuithibitisha wakati walipozungumza na shirika la habari la afp.Chernova aliongeza kusema kwamba wazamiaji wanapanga kutumia mashine maalum kuangalia ukubwa wa mabaki hayo na mahali yalipo ili kuweza kufahamu hatua zinazopaswa kuchukuliwa.
Mwanadiplomasia wa zamani wa Marekani Dan Kurtzer ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Israel amesema lugha chafu ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu baada ya azimio la Umoja wa mataifa kushutumu ujenzi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi , haikubaliki. Dan Kurtzer ambaye alikuwa balozi wa Marekani nchini Israel wakati wa utawala wa rais George W Bush ameiambia redio ya Israel kwamba lugha inayotumiwa dhidi ya rais wa Marekani haikubaliki na haipaswi kutumiwa na mshirika hata kama amekasirika. Netanyahu amemshutumu rais anayeondoka madarakani Barack Obama jana usiku kwa kuwa nyuma ya azimio hilo , akiongeza kwamba Israel haina shaka kwamba utawala wa Obama ulianzisha , kusimamia ,na kuratibu juu ya maelezo yake na kutaka azimio hilo lipitishwe. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa liliidhinisha azimio ambalo linashutumu ujenzi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo ya Wapalestina na kuitaka Israel kusitisha hatua hiyo.
Maafisa nchini Syria wamewashutumu wapiganaji waasi kwa kuwauwa raia 21 , ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto, kwa kuwapiga risasi wakati wakiondoka kutoka mji wa Aleppo wiki iliyopita. Miili ya watu hao ilipatikana katika vitongoji viwili mashariki mwa Aleppo. Mkuu wa kitengo cha kuchunguza ushahidi wa maeneo yanayotokea uhalifu mjini Aleppo zaher Hajjo aliliambia shirika la habari la Syria SANA kwamba miili ya raia 21 , ikiwa ni pamoja na watoto watano na wanawake wanne , waliouliwa na makundi ya magaidi, ilifukuliwa.Hajjo alinukuliwa akisema kwamba miili hiyo ilipatikana katika jela iliyokuwa ikiendeshwa na makundi ya kigaidi katika maeneo ya Sukkari na al-Kalasseh , na ilionekana kwamba watu hao walipigwa risasi kwa karibu.
Mshambuliaji wa kujitoa muhanga ameshambulia soko la kuuza ng'ombe leo mjini Maiduguri kaskazini mashariki mwa Nigeria , mji ambao umekumbwa na mashambulio mengi zaidi katika mapambano ya miaka saba yanayofanywa na wanamgambo wa Kiislamu wa kundi la Boko Haram. Polisi wamesema mshambuliaji huyo ambaye alikuwa ni mwanamke , ambaye alishambulia soko la Kasuwan Shanu katika wilaya ya kati ya kasuwa, alikuwa mtu pekee aliyeuwawa katika mripuko huo leo.Katika taarifa , polisi ilisema mwanamke wa pili ambaye alikuwa na bomu aliuwawa na kundi la watu karibu na eneo hilo, na majeshi ya usalama yalifanikiwa baadaye kuripua bomu hilo. Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo, lakini lina alama zote za kundi la Boko Haram na linakuja siku chache baada ya rais Muhammadu Buhari kusema kambi muhimu ya kundi hilo katika ngome yao kuu iliyobakia imekamatwa.