jumanne hii

Jumanne, 27 Desemba 2016
JOSE MOURINHO ASIFIA GOLI TAMU LA HENRIKH MKHITARYAN
Kocha wa Manchester United Jose
Mourinho amepongeza goli zuri lililofungwa kwa mpira wa kisigino kwa
nyuma na Henrikh Mkhitaryan katika mchezo walioibuka na ushindi dhidi
ya Sunderland katika dimba la Old Trafford.
Mkhitaryan alifunga goli hilo
lililozua utata kutokana na kuwa alikuwa ameotea akipokea pasi kutoka
kwa Zlatan Ibrahimovic na kufanya matokeo ya mchezo huo kuwa
Manchester 3-1 Sunderland.
Mkhitaryan mwenyewe amesema goli
hilo ni goli zuri kuwahi kufunga katika maisha yake ya soko, na
kuongeza kuwa hayo yalikuwa ni mazingaumbwe madogo ya kipindi cha
Sikukuu ya Krismasi.
MANCHESTER CITY YAKWEA HADI KATIKA NAFASI YA PILI KATIKA LIGI KUU YA UINGEREZA
Timu ya Manchester City imekwea hadi
nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuibuka
na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Hull City wakiwa ugenini katika
dimba la KCOM.
Kikosi cha Pep Guardiola kilipata
ushindi wake wa 12 katika msimu huu, na kuwa nyuma kwa pointi saba
dhidi ya vinara timu ya Chelsea.
Yaya Toure alifunga goli la kwanza
kwa mkwju wa penati katika kipindi cha pili, baada ya Raheem Sterling
kuchezewa rafu, Kelechi Iheanacho akafunga la pili na Curtis Davies
kujifunga la tatu.
Yaya Toure akifunga goli kwa mkwaju wa penati
Kelechi Iheanacho akifunga goli la pili la Manchester City
Curtis Davies akijifunga wakati akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na Raheem Sterling
NAHODHA YANGA ASEMA SIMBA WANAONGOZA TU LIGI, UBINGWA BADO SANA
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
NAHODHA
wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannaavaro’ amesema kwamba ni mapema mno
kuiondoa Yanga kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara.
Akizungumza
na Bin Zubeiry Sports - Online juzi, Cannavaro alisema kwamba baada ya
Yanga kulazimishwa sare ya 1-1 African Lyon watu wengi wanaelekea kukata
tamaa kama timu hiyo inaweza kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu.
Cannavaro
alisema watu wanaoikatia tamaa Yanga wakati huu lazima watakuwa wageni
wa Ligi, kwani kwa uzoefu anaamini ligi bado mchichi.
“Simba
wametupita pointi nne, ambazo ni sawa na wastani wa mechi mbili na bado
hawajacheza na sisi. Wakicheza na sisi tukawafunga, inabaki pointi
moja, na wakitoa hata sare mechi nyingine watapoteza pointi mbili na
sisi tutawapita,”alisema.
Cannavaro
alisema kwamba wachezaji wa Yanga kwa ujumla waliumizwa na sare ambayo
hawakuitarajia dhidi ya Lyon, lakini sasa wanaelekeza nguvu zao katika
mechi zijazo.
“Kwa
sasa hivi tunaelekeza nguvu zetu kwenye mchezo wetu ujao na Ndanda,
tunahitaji kushinda kwanza ili kurejesha imani za mashabiki wetu na
baada ya hapo tuendelee kupambana huku tukitazam na spidi ya wapinzani
wetu (Simba) katika mbio za ubingwa,”alisema Cannavaro.
Aidha,
Nahodha huyo amewataka mashabiki, wapenzi na wanachama wa Yanga kuwa
wavumilivu na wenye subira katika kipindi hiki na kushikamana na
wachezaji wao ili kuwatia moyo wafanye vizuri.
SAMATTA ASIKITIKA KUFUKUZWA KWA KOCHA ALIYEMSAJILI GENK
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amesikitishwa na klabu
yake, KRC Genk kumfukuza kocha Mbelgiji Peter Maes.
Akizungumza
na Bin Zubeiry Sports - Online leo kwa simu kutoka Ubelgiji, Samatta
amesema kwamba amesikitishwa na taarifa hizo, lakini hana namna nyingine
zaidi ya kukubali matokeo.
"Siyo
taarifa nzuri kwa mtu ambaye alitokea kuniamini kwa muda mfupi, lakini
hakuna chaguo zaidi ya kuendelea kujituma na kuwa bora zaidi, ili
kumpendeza kocha atakayekuja,"amesema Samatta.
Akimzungumzia
zaidi Maes, Nahodha huyo wa Tanzania alisema; "Alikuwa kocha kocha
mzuri, aina ya ufundishaji wake ulikuwa wa moja kwa moja na alikuwa
rafiki kwa kila mchazaji,".
Genk
imemfukuza rasmi Maes leo baada ya matokeo mabaya ya hivi karibuni na
kuelekea mchezo wa kesho, aliyekuwa Msaidizi wake, Rudi Cossey ataiandaa
timu.
Maes
ndiye aliyemsajili Samatta Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na akamuamini haraka na kumpa
nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
Chini ya Maes, Samatta amecheza mechi 35 Genk,18 msimu uliopita na 17 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 17 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na saba msimu huu.
Mechi
18 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 10 msimu huu,
wakati nane hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na mbili
msimu huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao tisa, manne msimu huu na
matano msimu uliopita.
Maes alijiunga na Genk msimu wa 2015-2016 kutoka KSC Lokeren na ameiongoza timu hiyo katika mechi 81 rasmi.
Genk
kesho itacheza na KAA Gent ikiwa chini ya kocha wa muda, Mbelgiji pia,
Rudi Cossey na klabu imemshukuru Peter Maes kwa kazi yake nzuri kwa
kipindi chote alichokuwa na timu na kumtakia kila la heri aendako.
SIMBA KUMALIZANA NA NDUSHA, ANGBAN JUMATANO
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
SIMBA
SC imesema kwamba hadi kesho itakuwa imekwishawalipa kipa Vincent
Angban na kiungo Mussa Ndusha ili waondoke Alhamisi kuerejea kwao.
Angban
kutoka Ivory Coast na Ndusha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC), wote wameachwa Simba SC katika dirisha dogo mwezi huu, kufuatia
kusajili kwa Waghana, kipa Daniel Agyei na kiungo James Kotei.
Baada ya kusitishiwa mikataba, wawili hao wanapaswa kulipwa na Simba SC kulingana na vipengeel vya mikataba yao.
Na
akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online leo, Katibu Mkuu wa Simba,
Patrick Kahemele amesema kwamba klabu haina tatizo na wachezaji hao na
tayari wamefikia makubaliano juu yaa namna ya kumalizana.
Mussa Ndusha (kushoto) aliichezea Simba mara ya mwisho ikifungwa na Mtibwa Sugar 2-1 Desemba 12, mwaka huu
Kahemele alisema kwamba wachezaji wote hao wana uelewa mzuri na wanaielewa vizuri mikataba waliyosaini kujiunga na Simba, hivyo hakuna tatizo lolote baina yao. “Hatuna tatizo nao kabisa, tumezungumza nao vizuri na tumefikia makubaliano kwamba tutakuwa tumekwishamalizana nao hadi kufika Jumatano (kesho) ili Alhamisi waondoke,”alisema. Aidha, Kahemele alisema wanauheshimu na kuuthamini mchango wa wachezaji hao kwa kipindi cha kuitumikia Simba na wanawatakia kila laa heri waendako. Wakati huo huo: Kikosi cha Simba jana kimeendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting Alhamisi wiki hii. Kahemele alisema kwamba timu imeweka kambi hoteli ya Spiece, Mnazi Mmoja mjini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo huo. “Tangu tutoke Mtwara tuliweka kambi Spiece na tutaendelea kuwa hapo hadi baada ya mchezo huu na Ruvu Shooting tutakapokwenda Zanzibar kwenye Kombe la Mapinduzi,”alisema Kahemele. Simba SC imeuanza vyema mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kushinda mechi mbili mfululizo za mwanzo na kuzidi kupaa kileleni. Wekundu hao wa Msimbazi walianza kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara kabla ya kuilaza 1-0 JKT Ruvu katikaa mchezo uliofuata Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Matokeo hayo yanawafanya Wekundu wa Msimbazi wafikishe pointi 41 baada ya mechi 17, wakiwazidi kwa pointi nne, mabingwa watetezi, Yanga wanaofuatia katika nafasi ya pili kwa pointi zao 37.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni