FARID SASA ANGOJA LESENI TU YA RFEF AANZE KAZI SEGUNDA
WINGA chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Farid Malik Mussa amesema kwamba anasubiri leseni ya Mamlaka ya Shirikisho la Soka Hispania (RFEF) aanze kuchezea klabu yake, Club Deportivo Tenerife. Farid amejiunga na klabu hiyo ya Santa Cruz de Tenerife, Tenerife, visiwa vya Canary mwezi huu kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu kutoka Azam FC ya Dar es Salaam. Na tangu afike wiki iliyopita amekuwa akifanya mazoezi tu na timu hiyo ya Daraja la Kwanza, maarufu kama Segunda Division, inayotumia Uwanja wa Heliodoro Rodriguez Lopez wenye kuchukua mashabiki 23,660.
Farid Mussa Malik akiwa na vifaa vya michezo alivyopatiwa baada ya kuwasili Tenerife
Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online kwa simu jana usiku, Farid alisema anaendelea vizuri tangu afike na amekuwa akifanya mazoezi na wenzake, lakini hajaanza kicheza Ligi kwa sababu ya leseni. “Nadhani leseni itatoka wakati wowote. Sitarajii kama itachelewa,”alisema Farid. Azam FC imemtoa kwa mkopo Farid kwenda CD Tenerife kwa makubaliano maalum baada ya winga huyo kufuzu majaribio katika klabu hiyo Aprili mwaka jana alipokwenda na Mkurugenzi wa klabu yake, Yussuf Bakhresa. Farid alitua Hispania Aprili 21 baada ya kuichezea Azam FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance mjini Tunis, Tunisia ikifungwa 3-0 na kutolewa kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya awali kushinda 2-1 Dar es Salaam. Na ilimchukua wiki moja tu Farid kuwakuna kwa kipaji chake makocha wa Tenerife na kutaka kumnunua, lakini Azam ikakataa na kuamua kumtoa kwa mkopo
SIMBA YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI
Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
SIMBA
SC imekwenda Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa bao
1-0 dhidi ya KVZ usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Ushindi
huo uliotokana na bao pekee la kiungo Muzamil Yassin dakika ya 43,
unaifanya Simba SC ifikishe pointi sita baada ya kucheza mechi mbili.
Sifa
zaidi zimuendee beki Abdi Hassan Banda aliyeyafanikiwa kuvunja mtego wa
kuotea wa KVZ ma kumchomea pasi nzuri Muzamil aliyekwenda kufunga.
Huu unakuwa ushindi wa pili mfululizo kwa Simba katika michuano hii, baada ya juzi kuilaza Taifa Jang’ombe 2-1. KVZ ilimaliza pungufu mchezo huo baada ya beki wake, Rashid Omar Rashid kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kumkwatua mshambuliaji wa Simba, Pastory Athanas nje kidogo ya boksi akiwa anakwenda kufunga. Katika mchezo wa Kundi A uliotangulia leo, Jang’ombe Boys iliwalaza mabingwa watetezi, URA ya Uganda 2-1. Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi za Kundi B, kati ya Zimamoto na Yanga kuanzia Saa 10:00 jioni na Jamhuri dhidi ya Azam kuanzia Saa 2:30 usiku. Kikosi cha Simba leo kilikuwa; Daniel Agyei, Janvier Besala Bokungu, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Method Mwanjali, Abdi Banda, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, James Kotei, Athanas Pastory, Juma Luizio na Muzamil Yassin. KVZ; Abdallah Bakari, Saleh Nassor, Makarani Mluchu, Rashid Omar, Said Mohammed, Suleiman Ali, Suleiman Hassan, Suleiman Juma, Sultan Kasikasi, Mohammed Maulid na Masoud Abdllah.

LALA SALAMA LIGI YA WANAWAKE YAANZA KESHO KARUME
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
DURU
la Pili la Ligi Kuu soka ya Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), linatarajiwa kuanza kesho Jumatano Januari 4, 2017 kwa
michezo minne itakayofanyika kwenye viwanja mbalimbali.
Kwa
mujibu wa ratiba, katika kundi ‘A’ pekee litakuwa na mchezo mmoja
wakati kundi ‘B’ litakuwa na michezo mitatu kwa siku ya kesho Jumatano.
Mchezo
pekee wa kesho wa kundi ‘A’ utakuwa kati ya Mburahati Queens ya
Kinondoni, Dar es Salaam na Viva Queens ya Mtwara – mchezo utakaofanyika
Uwanja wa Karume jijini katika mzunguko wa sita wa ligi hiyo.
Michezo mingine mitatu itakuwa ni ya Kundi B ambako Mejengo FC itacheza na Marsh Academy ya Mwanza kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida wakati Panama ya Iringa inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Sisterz ya Kigoma kwenye Uwanja wa Samora huku Victoria Queens ikiikaribisha Baobab ya Dodoma kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera. Kabla ya michezo ya juma lijalo, upande wa Kundi A michezo yake miwili ya mzunguko wa sita itafanyika Alhamisi Januari 5, mwaka huu ambako Evergreen ya Temeke, Dar es Salaam itacheza na Fair Play ya Tanga kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam. Mlandizi ya Pwani inatarajiwa kuikaribisha JKT Queens ya Dar es Salaam, katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Mabatini.

DILI LA HAJIB MISRI LAINGIWA UKAKASI
BIASHARA ya mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Hajib kwenda Haras El Hodoud ya Misri inaelekea kama kutokamilika kwa sasa. Dirisha la usajili la Misri lilifungwa juzi na Haras El Hodoud hawakuwa wamefanya mawasiliano yoyote na Simba SC hadi jana jioni. Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Hajji Sunday Manara alisema jana katika mazungumzo na Bin Zubeiry Sports - Online kwamba klabu yake haijapokea ofa yoyote kutoka kwa Haras El Hodoud. “Sijui wanategemea nini, maana dirisha la usajili la kwao linafungwa leo (jana). Sasa sijui wana mpango gani,”alisema Manara.
Ibrahim Hajib (kushoto) akiwa na wachezaji wa Haras El Hodoud nchini Misri
Juzi Hajib alisema kwamba amefanya mazungumzo ya awali na Haras El Hodoud na kufikia makubaliano, lakini kwanza wanatakiwa kumalizana na klabu yake ya sasa, Simba SC. “Ninamshukuru Mungu nimefurahia siku zangu chache za kuwa Alexandria, nilikuwa katika klabu nzuri, mazingira mazuri na wachezaji wenzangu kule wamenikubali mapema sana. Sasa baada ya yote, ninawasikilizia wao tu ni jinsi gani watalimalizia hili suala,”alisema. Hajib alirejea nchini juzi na kusema kwamba atajiunga na timu itakayompa ofa nzuri kati ya Haras El Hodoud ya Misri na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini inayomtaka pia. Pamoja na kufuzu majaribio na vipimo vya afya Haras El Hodoud, lakini imeripotiwa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini pia inatamaka mchezaji huyo wa Simba kwa kusaini naye mkataba moja kwa moja bila majaribio. “Ni kweli nimesikia hizo habari, na si Kaizer tu, timu nyingine kama mbili za Afrika Kusini nazo zimetangaza ofa. Kwanza ninamshukuru Mungu. Mungu ni mkubwa, sasa tusubiri haya maneno yawe vitendo ndiyo tufanye maamuzi,” alisema Hajib. Wakala anayeshughulikia mipango ya Hajib nchini Afrika Kusini, Rodgers Mathaba kwa upande wake alikiri juu ya mchezaji huyo kutakiwa na Kaizer Chiefs. “Ni kweli, Kaizer wanamtaka Hajib. Najua alikuwa Misri, nasubiri arejee Dar es Salaam nimpigie simu nizungumze naye. Tayari nimekwishazungumza na kocha Steve Khompela wa Kaizer,”alisema. Hajib alikuwa ana wiki nzuri ya majaribio Haras El Hodoud ikiwemo kufunga bao moja katika ushindi wa 4-0 kwenye mchezo wa kirafiki Ijumaa. Mathaba ndiye aliyempeleka Hajib Afrika Kusini kwa majaribio pia, klabu ya Lamontville Golden Arrows FC ya Ligi Kuu ya ABSA nchini humo na pamoja na kufuzu, wakamtaka arejee Simba kumalizia Mkataba ili baadaye aende kama mchezaji huru.
YANGA YAANZA NA MOTO KOMBE LA MAPINDUZI, JAMHURI YAFA 6-0
YANGA SC imeanza kwa kishindo michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar baada ya kuichapa mabao 6-0 Jamhuri ya Pemba usiku huu Uwanja wa Amaan. Ushindi huo, unaifanya Yanga iongoze Kundi B, kwa pointi zake tatu sawa na Azam iliyoshinda 1-0 dhidi ya Zimamoto katika mchezo wa kwanza jioni ya leo. Winga Simon Msuva alifungua biashara nzuri dakika ya 19 akiifungia Yanga bao la kwanza kwa kumalizia kona maridadi ya Nahodha, kiungo Haruna Niyonzima kutoka Rwanda. Mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Ngoma akaifungia Yanga mabao mawili mfululizo daakika ya 23 akimalizia krosi ya Mwinyi Hajji Mngwali na dakika ya 37 baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa, Omary Said kufuatia shuti la Msuva.
Donald Ngoma (kushoto) akikimbia kushangilia baada ya kufunga, huku mabeki wa Jamhuri wakiwa wameduwaa
Msuva tena akawainua vitini mashabiki wa Yanga baada ya kufunga baola nne dakika ya 40 akitumia makosa ya kiopa kutoka langoni bila mahesabu. Baada ya kumaliza kipindi cha kwanza na mtaji wa mabao 4-0, kocha wa Yanga, George Lwandamina akakianza kipindi cha pili kwa mabadiliko, akimpumzisha kiungo Mzambai mwenzake, Justin Zulu na nafasi yake kuchukuliwa na mzalendo, Said Juma ‘Makapu’. Kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko akaifungia Yanga bao la tano dakika ya 59 akimalizia krosi ya Juma Abdul, kabla ya kiungo Juma Mahadhi aliyetokea benchi pia kipindi cha pili kuhitisha tafrija za mabao kwa kufunga la sita dakika ya 85 kwa shuti la karibu. Katika mchezo huo, nafasi pekee nzuri ambayo Jamhuri walipoteza ilikuwa ni mapema atu dakika ya 13 baada ya krosi ya Ahmed Ali kuokolewa na beki wa Yanga Andrew Vincent ‘Dante’ na kuwa kona iliyochongwa na Mohamed omary ambayo haikuza matunda baada ya beki huyo kuokoa tena. Kikosi cha Yanga kilikuwa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Kelvin Yondan/Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dk72, Vincent Andrew ‘Dante’, Justin Zulu, Simoni Msuva/Geoffrey Mwashiuya dk77, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma/Juma Mahadhi dk66, Haruna Niyonzima/Deus Kaseke dk66 na Emmanuel Martin. Jamhuri: Omary Said, Mohammed Mgau, Mohammed Omary, Mohammed Juma, Yussuf Makame, Greyson Gerald, Umry Bagaseka, Mbarouk Suleiman, Mwalimu Mohammed, Ahmed Ally na Mussa Mbarouk.
TFF YAACHANA NA MKWASA, MAYANGA KOCHA MPYA STARS
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtangaza Salum Mayanga kuwa kocha mpya wa muda wa timu ya taifa, Taifa Stars. Malinzi amesema leo kwamba hiyo inafuatia aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa kumaliza Mkataba wake leo. Majukumu ya Mayanga yatakuwa ni kuandaa kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo mechi za awali zitanza mapema mwaka huu. Mayanga atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya mechi za kufuzu CHAN. TFF inamshukuru Kocha Charles Boniface Mkwasa kwa utumishi katika nafasi hiyo ulioanza Julai, 2015 akimrithi Mholanzi, Mart Nooij na kumtakia mafanikio katika mipango yake inayofuata. Katika kipindi chake cha kuwa Taifa Stars, Mkwasa ameiongoza timu katika mechi 13, ikishinda mbili, kufungwa sita na sare tano.
Chini ya Charles Boniface Mkwasa (kulia) Taifa Stars, imeshinda mechi mbili tu kati ya 13, ikifungwa sita na sare tano
REKODI YA MKWASA TAIFA STARS Tanzania 1-1 Uganda (Kufuzu CHAN, Kampala) Tanzania 1-2 Libya (Kirafiki Uturuki) Tanzania 0-0 Nigeria (Kufuzu AFCON Dar) Tanzania 2-0 Malawi (Kufuzu Kombe la Dunia Dar) Tanzania 0-1 Malawi (Kufuzu Kombe la Dunia Blantyre) Tanzania 0-2 Afrika Kusini U23 (Kirafiki Johannesburg) Tanzania 2-2 Afrika Kusini U23 (Kufuzu Kombe la Dunia Dar) Tanzania 2-2 Afrika Kusini U23 (Kufuzu Kombe la Dunia Dar) Algeria 7-0 Tanzania (Kufuzu kombe la Dunia Blida) Tanzania 1-0 Chad (Kufuzu AFCON D’jamena) Tanzania 0-2 Misri (Kufuzu AFCON Taifa) Tanzania 1-1 Kenya (Kirafiki Nairobi) Tanzania 0-3 Zimbabwe (Kirafiki Harare)
AZAM YAANZA VYEMA KOMBE LA MAPINDUZI
BAO pekee la mshambuliaji chipukizi, Shaaban Iddi Chilunda limetosha kuipa Azam FC ya Dar es Salaam ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Zimamoto katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mapinduzi. Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar jioni ya leo, Chilunda alifunga bao hilo dakika ya 79 akimvisha kanzu kipa baada ya kuipokea kiufundi kwa kifua pasi ya juu ya kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’. Ushindi huo unaifanya Azam FC kuongoza Kundi B ikiwa na pointi tatu, ambapo hivi sasa itasubiria mchezo wa pili wa kundi hilo utakazoihusisha Yanga na Jamhuri ili kujua kama itaendelea kukaa kileleni. Winga wa kushoto wa Azam FC kutoka Ghana, Enock Atta Agyei, alianza kuichezea mechi ya kwanza ya mashindano timu hiyo tokea aliposajiliwa, hii ni baada ya kushindwa kuitumikia kwenye Ligi Kuu kufuatia kutotimiza umri wa miaka 18, ambapo kwenye ligi ataanza kuonekana baada ya kutimiza umri huo Januari 5 mwaka huu.
Shaaban Iddi (katikati) akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga jana
Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii walianza mchezo huo kwa kasi ya chini kabla ya kubadilika dakika 20 za mwisho za kipindi cha pili, ambapo mshambuliaji Samuel Afful, alikaribia kuiandikia bao la uongozi Azam FC dakika ya 30 baada ya kuwatoka mabeki wa Zimamoto lakini shuti alilopiga lilimbabatiza kipa na kuokolewa na mabeki. Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, timu zote ziliweza kutoka nguvu sawa ya bila kufungana, katika dakika 10 za mwanzo za kipindi cha pili Azam FC ilifanya mabadiliko ya kumtoa Afful na kuingia Shaaban ambaye alienda kufunga bao la ushindi. Kabla ya kufunga bao hilo, Shaaban huenda angetangalia kufunga jingine kama angekuwa makini kutumia pasi safi ya Enock Atta Agyei dakika ya 59, lakini aliukosa mpira wakati kiwa kwenye harakati za kuupiga mpira. Azam FC iliweza kuulinda ushindi huo hadi dakika 90 zinamalizika, ambapo itashuka tena dimbani Keshokutwa Jumatano kucheza dhidi ya Jamhuri mchezo utakaofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar saa 2.15 usiku. Kikosi cha Azam FC kilikuwa: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Yakubu Mohammed, Stephan Kingue, Salum Abubakar, Frank Domayo/Mudathir Yahya dk 77, Yahaya Mohammed, Samuel Afful/Shaaban Idd dk 50, Enock Atta/Ramadhan Singano dk 67.
Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
SIMBA
SC imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Taifa
Jang’ombe mabao 2-1 katika mchezo wa Kundi A usiku huu Uwanja wa Amaan,
Zanzibar.
Hadi
mapumziko, Simba walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na wachezaji
wa zamani wa Mtibwa Sugar, Muzamil Yassin na Juma Luizio.
Kiungo
Muzamil Yassin alianza kuifungia Simba dakika ya 27 baada ya kuwahi
mpira uliogonga mwamba na kurudi kufuatia shuti la beki Mzimbabwe,
Method Mwanjali ambalo lilimshinda kipa Ahmed Suleiman.
Mshambuliaji Juma Luizio akafunga kwa shuti la umbali wa mita 17 baada ya kuwatoka mabeki wawili wa Taifa, kufuatia pasi ya Muzamil Yassin. Luizio anayecheza kwa mkopo kutoka Zesco United ya Zambia akiichezea kwa mara ya pili Simba leo, alidumu uwanjani kwa dakika 60 tu kabla ya kumpisha Mrundi, Laudit Mavugo. Beki wa kati wa Simba, Novaty Lufunga akajifunga kwa kichwa katika harakati za kuokoa mpira wa kona uliochongwa na Hassan Bakari dakika ya 76 kuipatia Taifa bao la kufutia machozi. Katika mchezo uliotangulia, URA iliichapa 2-0 KVZ. Simba sasa inalingana kwa pointi na URA na Taifa iliyoifunga Jang’ombe Boys 1-0 katika mchezo wa kwanza Ijumaa. Kikosi cha Simba leo kilikuwa; Daniel Agyei, Hamad Juma, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, James Kotei, Shiza Kichuya/Mwinyi Kazimoto, Muzamil Yassin, Juma Luizio/Laudit Mavgugo dk60, Said Ndemla na Jamal Mnyate/Moses Kitundu dk66. Taifa Jang’ombe; Ahmed Suleiman, Adam Hamad, Saleh Mgeni/Hassan Bakari dk59, Abdallah Shaibu, Samir Yahya, Khatib Simai, Ally Mlanga, Baraka Ushindi/Mohmed Salum ‘Messi’ dk56, Seif Hassan, Adam Ibrahim/Method Apigi dk62 na Yahya Tumbo/Nelson Gabriel dk72.

SIMBA YAANZA VYEMA KOMBE LA MAPINDUZI, LUIZIO AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO

KOMBE LA MAPINDUZI, LUIZIO AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO

Wednesday, January 4, 2017
TUZO ZA CAF KUTOLEWA KESHO.
SHIRIKISHO la Soka la
Afrika-CAF kesho linatarajia kufanya sherehe ya kutoa tuzo kwa wachezaji
mbalimbali wa soka waliofanya vizuri katika kipindi cha mwaka mzima
uliopita. Sherehe hizo zinakuwa ni za 25 toka kuanzishwa kwake na
zinatarajiwa kufanyika jijini Abuja, Nigeria kwa mara ya pili mfululizo.
Kwenye sherehe hizo atapatikana mfalme wa soka Afrika ambapo miongoni
mwao ni pamoja na mshindi wa tuzo ya mwaka jana Pierre-Emerick
Aubameyang wa Gabon, Riyad Mahrez wa Algeria na Sadio Mane anayetoka
Senegal. Kuanzia mwaka 1992 zilipoanzishwa tuzo hizo ambapo ilikwenda
kwa nguli wa zamani wa Ghana Abeid Ayew Pele mpaka mwaka jana alipotwaa
Aubameyang ni jumla ya wachezaji 15 waliofanikiwa kutwaa hiyo. Nyota wa
Cameroon Samuel Eto’o ndio mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo hiyo mara nne
mfululizo mwaka 2003, 2004, 2005 na 2010 kabla ya Yaya Toure wa Ivory
Coast hajaivunja rekodi hiyo kwa kutwaa kuanzia mwaka 2011 mpaka 2014.
HULL CITY YAMTIMUA MENEJA WAKE.
KLABU ya Hull City
imeamua kumtimua meneja wake Mike Phelan kufuatia kuendelea kuvurunda
kwa timu hiyo katika Ligi Kuu. Phelan mwenye umri wa miaka 54 alichukua
mikoba kama kocha wa muda kufuatia kuondoka kwa Steve Bruce majira ya
kiangazi na kufanikiwa kuteuliwa kuchukua nafasi hiyo moja kwa moja
Octoba mwaka jana. Lakini kufuatia Hull City kuburuza mkia katika
msimamo wa ligi huku wakiwa wameambulia alama tatu pekee katika mechi
tisa za mwisho, klabu imeamua kuachana na kocha huyo. Katika taarifa
yake klabu hiyo imedai kuwa kwasasa wanatafuta mbadala wa Phelan na
watamtangaza hivi karibuni.
CONTE AWAPASHA WANAOSEMA TIMU YAKE INAPENDELEWA.
MENEJA wa Chelsea,
Antonio Conte amedai kuwa ratiba yao ya msimu wa sikukuu inakosolewa
kwasababu wako kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu. Chelsea wana nafasi
kubwa ya mapumziko katika ratiba yao kuliko timu yeyote kwenye kipindi
hiki huku meneja wa Manchester United Jose Mourinho naye akitoa kauli
kuhusiana na faida inayopata klabu yake hiyo ya zamani. Chelsea
wameshinda mechi 13 mfululizo katika ligi na wanaweza kufikia rekodi
iliyowekwa na Arsenal mwaka 2002 kama wakifanikiwa kuichapa Tottenham
Hotspurs baadae leo. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Conte alikiri
kuwa ni kweli wana faida kidogo kwani wamepata muda wa kupumzika siku
moja zaidi ya wapinzani wao Spurs lakini sio wao waliopanga ratiba.
Conte aliendelea kudai kuwa anadhani malalamiko yamekuwa makubwa zaidi
kwao kwasababu wanaongoza msimamo wa ligi.
WACHEZAJI WANGU WALIGOMBA KUFUNGWA - WENGER.
MENEJA wa Arsenal,
Arsene Wenger amesema kikosi chake kiligoma kupoteza mchezo kufuatia
kutoka nyuma wakiwa wamefungwa mabao 3-0 na kutoa sare ya mabao 3-3
dhidi ya Bournemouth. Hiyo ni mara ya kwanza kwa Arsenal kufanikiwa
kupata alama baada ya kufungwa mabao matatu katika mchezo wa Ligi Kuu.
Akihojiwa Wenger amesema mchezo huo ulikuwa ni jaribio tosha la kimwili
na kiakili, lakini mwishoni wamehuzunishwa kwa kutoshinda. Wenger
aliendelea kudai kuwa walihitaji kushinda mchezo huo lakini haikuwa
rahisi kwani timu kubwa zingine nazo zilipoteza mechi zao kwa
Bournemouth ikiwemo Liverpool.
CHAPECOENSE KUSAJILI 20 WAPYA KWA AJILI YA MSIMU MPYA.
MKURUGENZI wa michezo wa
Chapecoense, Rui Costa amedai kuwa klabu hiyo inatarajia kusaini
wachezaji wapya 20 kwa ajili ya msimu mpya huku fulana mbili za
wachezaji walionusurika katika ajali zikituzwa bila kwa matumaini kuwa
wanaweza kurejea uwanjani tena. Klabu hiyo ilipoteza karibu wachezaji
wote waliofariki katika ajali ya ndege nchini Colombia Novemba 28 mwaka
huu. Klabu hiyo ndogo inayotoka kusini wa Brazil ilikuwa njiani kuelekea
Medelin kucheza na Atletico Nacional katika mchezo wa fainali ya Copa
Sudamericana kabla ya kupata ajali hiyo milimani na kuua watu 71. Mabeki
Neto na Alan Ruschel walisalimika katika ajali hiyo sambamba na kipa wa
akiba Jackson Follmann ambaye mguu wake umekatwa kutokana na ajali
hiyo. Costa amesema wachezaji wote watatu waliopona ajalini bado wana
nafasi ya kucheza na hakuna mchezaji yeyote atakayevaa jezi zao na
pamoja na kwamba Follmann hataweza lakini anaweza kushiriki kwa upande
mwingine. Costa aliendelea kudai kuwa klabu hiyo itasajili wachezaji 18
mpaka 20 wapya kabla ya kuanza kwa msimu Januari 26 kwa mchezo wa
nyumbani dhidi ya Joinville.
Monday, January 2, 2017
WENGER ALISIFIA BAO LA GIROUD.
MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amedai kuwa bao murua la Olivier Giroud alilofunga katika ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Crystal Palace ni moja kati ya mabao yake tano bora aliyopata kushuhudia katika kipindi cha miaka 21 akiwa na klabu hiyo.
Mabao ya kina Thierry Henry na Dennis Bergkamp nayo yapo katika orodha yake lakini amesema bao hilo la jana milele litakuwa la Giroud pekee.
Wenger amesema kiufundi sio jambo lisilowezekana lakini unatakiwa na uwezo tofauti kwani mpira wa krosi haukuja kama ilivyotakiwa na Giroud alifanya jambo la kipekee.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amesema ilikuwa kama bahati kwani mpira haukuja kama ilivyotakiwa.
Friday, December 30, 2016
MAPINDUZI CUP YANG'OA NANGA.
Timu zitakazoshiriki
kombe la Mapinduzi msimu huu zinatarajiwa kupata asilimia kumi ya mapato
ya uwanjani baada ya kulipiwa gharama zote za siku ya mchezo. Kila
klabu itapatiwa asilimia hizo 10 baada ya kulipiwa gharama zote ya siku
ya mchezo na kinachobakia watapatiwa asilimia hizo. Akizungumza na
Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa kamati inayosimamia kombe la Mapinduzi
Sharifa Khamis amesema msimu huu wanatarajia kuwapatia kila timu
asilimia 10 ya mapato ya uwanjani baada ya kulimia gharama zote za
mchezo. “Vilabu vimelalamika hasa vya Zanzibar hali zao ni mbaya sana,
kwaiyo kwa pamoja tumekubaliana kwa kila timu tutaipatia asilimia 10 ya
mapato ya uwanjani baada ya kulimia gharama zote za mchezo.” Aidha
kamati ya kombe la Mapinduzi msimu huu imepanga kila timu kuwapatia
nafasi 35 kwa wachezaji pamoja na viongozi kuingia bure uwanjani katika
mashindano hayo. “Tumekubaliana na vilabu kila timu tutaipatia nafasi
35 za kuingia bure uwanjani kuangalia mashindano hayo.” Pazia la
Mashindano ya Kombe la Mapinduzi linatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake
Disemba 30, 2016 katika uwanja wa Amaan saa 2:15 Usiku ambapo kutakuwa
na mchezo wa Derby ya Jangombe kati ya Taifa ya Jangombe na Jangombe
boys ambapo mashindano ya msimu huu yameshirikisha vilabu 9, vitano
vikitokea Zanzibar, vitatu Tanzania bara na kimoja kutaka Uganda ambao
ndio mabingwa watetezi timu ya URA.
KUNDI A: Simba, URA, KVZ, Taifa ya Jangombe na Jangombe Boys.
KUNDI B: Yanga, Azam, Zimamoto na Jamhuri.
RATIBA KAMILI YA MAPINDUZI CUP
30/12/2016 Taifa ya jang’ombe vs Jang’ombe boys saa 2:30 usiku.
1/1/2017 KVZ VS URA Saa 10:00 alasiri, Simba vs Taifa ya Jang’ombe saa 2:30 usiku.
2/1/2017 Azam vs Zimamoto saa 10:00 alasiri, Yanga vs Jamhuri saa 2:30 usiku.
3/1/2017 Jang’ombe boys vs URA saa 10:00 alasiri, KVZ vs Simba saa 2:30 usiku.
4/1/2017 Zimamoto vs Yanga saa 10:00 alasiri, Jamhuri vs Azam saa 2:30 usiku.
5/1/2017 KVZ vs Jang’ombe boys saa 10:00 alasiri, Simba vs URA saa 2:30 usiku.
6/1/2017 Taifa ya jang’ombe vs KVZ saa 2:30 usiku.
7/1/2017 Jamhuri vs Zimamoto saa 10:00 alasiri, Yanga vs Azam saa 2:30 usiku.
8/1/2017 Simba vs Jang’ombe boys saa 10:00 alasiri ,Taifa ya jang’ombe vs URA 2:30 usiku.
10/1/2017 Saa 10: 00 nusu fainal ya kwanza , Saa 2:30 nusu fainal ya pili.
13/1/2017 FAINAL saa 2: 30 usiku.

CHANZO NI BEKI 3
BIN ZUBERY
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni