AJTC VOICE FO VOICLESS

Jumatano, 18 Januari 2017

november 30/12



MAFUNZO YA VITENDO YAWA FURAHA KWA WANAFUNZI VYUONI

Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha,wakiwa katika mafunzo ya vitendo wakiwa darasani.


Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wametakiwa kujifunza masomo yao kwa vitendo ili kuongeza maarifa zaidi na kuleta ushindani katika soko la ajira pindi watakapoajiriwa.



Hayo yamesemwa na mkufunzi wa chuo hicho Bw;Steven Mulaki alipokuwa akihojiwa na SPIRITMWAMBA mapema leo mchana alipokuwa akiwafundisha wanafunzi wa darasa la Mt Ordizungwa.



Bw Mulaki ameongeza kwa kusema kuwa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wa vyuoni ni muhimu kwa kuwa watakapohitimu masomo yao itawasaidia kupata uzoefu watakapoajiriwa na taasisi au makampuni mbalimbali



Kwa upande wa wanafunzi wamefurahishwa na mafunzo hayo ambapo wengi wao wamemsifu mkufunzi huyo kwa kufundisha vizuri.




Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Singida Afariki Dunia, Mwili Kuagwa Leo Saa 11 Jioni Muhimbili

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) EX Peter Kakamba amefariki dunia alfajiri ya tarehe 30/11/2016 katika hospital ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kakamba alizaliwa mwaka 1963 katika kijiji cha Kawajense Wilayani Mpanda, mkoa wa Katavi. Alisoma shule ya msingi Shanwe Kawajense  mwaka 1973 hadi 1980, Kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari Kantalamba mwaka 1981 hadi 1984 ambapo kidato cha tano na sita alisoma katika shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro mwaka 1985 hadi 1987. Mwaka 1992 hadi 1994 alisoma Astashahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Marehemu alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1988 ambapo katika utumishi wake alipandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Konstable wa Polisi (1989), Sagenti wa Polisi (1991), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1997), Mkaguzi wa Polisi (2003), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (2006), Mrakibu wa Polisi (2008), Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2011), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2015) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2016).
 
Baadhi ya nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa  Mwendesha Mashtaka wa Polisi katika mkoa wa Iringa, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, Afisa mnadhimu wa Polisi katika Mikoa ya Iringa na Geita, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa na mpaka anafariki alikuwa Kamanda wa Polisi katika mkoa wa Singida.
 
Kufuatia kifo hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu anatoa pole kwa Maofisa, Wakaguzi,Askari, ndugu, jamaa na marafiki kwa Msiba huo.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa,
Jina la Bwana lihimidiwe - Amen.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.        

Alhamisi, 12 Januari 2017

michezo alhamisi hii

 

 

 BPL-FUATILIA HAPA

TIMU YA BARCELONA YATINGA ROBO FAINALI YA COPA DEL REY

Luis Suarez amefunga goli la 100 katika michezo 120 akiwa na Barcelona wakati timu hiyo ikitinga robo fainali ya Copa del Rey kwa kuifunga Athletic Bilbao magoli 3-1.

Suarez alifunga goli katika kipindi cha kwanza kufuatia krosi ya Neymar, na katika kipindi cha pili Neymar akafunga goli la pili kwa mkwaju wa penati.

Athletico Bilbao walipata goli pekee lililofungwa na kichwa na mshambulia Saborit, hata hivyo Lionel Messi aliipatia Barcelona goli la tatu kwa shuti la mpira wa adhabu.
                       Luis Suarez akimalizia vyema mpira wa krosi iliyopigwa na Neymar
   Lionel Messi akipiga mpira wa adhabu ulioenda kujaa wavuni na kuipatia ushindi Barcelona
 

SOUTHAMPTON YAITUNGUA LIVERPOOL GOLI MOJA BILA MAJIBU

Timu ya Southampton imeanza vyema mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya kombe la EFL, kwa kupata ushindi inaostahili wa goli 1-0 didi ya Liverpool katika dimba la St Mary.

Goli la Southampton lilimaliziwa vyena na Nathan Redmond akipokea pasi ya Jay Rodriguez, na kuipatia ushindi muhimu kabla ya mchezo wa marudiano Anfield Januari 25.
                                   Nathan Redmond akijipinda na kuachia shuti lililojaa wavuni 
       Nathan Redmond akishika kichwa baada ya kukosa nafasi ya kufunga goli la pili 
 

Diamond akabidhiwa bendera ya taifa kuliwakilisha taifa AFCON 2017 nchini Gabon

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akimkabidhi bendera ya Taifa Mwanamuziki wa bongo fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye Ufunguzi wa Mashindano ya AFCON 2017 yanayotarajiwa kufanyika nchini Gabon.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye akiongea na wageni waalikwa pamoja na Waandishi wa Habari wakati wa hafla ya kumkabidhi bendera ya Taifa mwanamuziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz anayekwenda kushiriki katika Ufunguzi wa Mashindano ya AFCON 2017 yanayotarajiwa kufanyika nchini Gabon. Hafla hiyo imefanyika leo 11 Januari, 2017 Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa pamoja na Waandishi wa Habari wakifuatilia hotuba ya Waziri Nape Nnauye wakati wa hafla ya kukabidhi bendera ya Taifa kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz iliyofanyika leo 11 Januari, 2017 Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa DSTV Multi Choice Tanzania Bw. Salum Salum akiongea na Waandishi wa Habari pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kukabidhi bendera ya Taifa kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz anayekwenda kushiriki katika Ufunguzi wa Mashindano ya AFCON 2017 yanayotarajiwa kufanyika nchini Gabon.
Balozi wa DSTV Bomba Bw. Lucas Mhuvile maarufu kama Joti akiongea na Waandishi wa Habari pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kukabidhi bendera ya Taifa kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz iliyofanyika leo 11 Januari, 2017 Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye, Mkurugenzi wa DSTV Multi Choice Tanzania Bw. Salum Salum pamoja na mwanamuziki wa bongo fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz wakiteta jambo kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhi bendera ya Taifa kwa mwanamuziki huyo anayekwenda kushiriki katika Ufunguzi wa Mashindano ya AFCON 2017 yanayotarajiwa kufanyika nchini Gabon.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati)  akimpongeza mwanamuziki wa bongo fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz wakiteta jambo kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhi bendera ya Taifa kwa mwanamuziki huyo anayekwenda kushiriki katika Ufunguzi wa Mashindano ya AFCON 2017 yanayotarajiwa kufanyika nchini Gabon. Anayeshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa DSTV Multi Choice Tanzania Bw. Salum Salum
Mwanamuziki wa bongo fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz akimshukuru Waziri Nape Nnauye pamoja na Serikali kwa ujumla kwa mchango mkubwa inaotoa katika kukuza sekta ya Sanaa nchini wakati wa hafla ya kukabidhi bendera ya Taifa kwa mwanamuziki huyo anayekwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye Ufunguzi wa Mashindano ya AFCON 2017 yanayotarajiwa kufanyika nchini Gabon.iliyofanyika leo 11 Januari, 2017 Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.


Jumatatu, 9 Januari 2017

JUMATATU 09/01/2017

YANGA KUWAKOSA TAMBWE, NGOMA, ZULU NA CHIRWA KESHO DHIDI YA SIMBA

Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR KOCHA wa Yanga, Mzambia George Lwandamina amesema kwamba ataingia kwenye mchezo wa kesho dhidi ya mahasimu, Simba hali ya kikosi chake ikiwa si nzuri sana. Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online leo, Lwandamina amesema kwamba wachezaji wake wanne tegemeo wote ni majeruhi na hawawezi kucheza kesho. Lwandamina aliwataja wachezaji majeruhi ni Wazambia wenzake, viungo Justin Zulu na Obrey Chirwa na washambuliaji Mrundi Amissi Tambwe na Mzimbabwe Donald Ngoma.
George Lwandamina amesema wachezaji wake tegemeo wanne ni majeruhi kuelekea mchezo wa kesho
Pamoja na hao, Lwandamina alisema beki Pato Ngonyani na mshambuliaji Matheo Anthony nao wote ni wagonjwa na hawana uhakika wa kucheza kesho. Kwa ujumla Lwandamina ambaye timu yake ilifungwa 4-0 na Azam FC Jumamosi kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi A, alisema ataingia kwenye mchezo wa kesho katika mazingira magumu ya kukatisha tamaa. “Lakini hatuna namna nyingine, lazima tuingize timu tukapambane,”alisema. Yanga inakutana na mahasimu, Simba katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku wa leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
 
 

MKUDE: MECHI NA YANGA ITAKUWA NGUMU KESHO

Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR NAHODHA wa Simba, Jonas Mkude amesema kwamba mechi dhidi ya Yanga itakuwa ngumu kwa sababu kila timu imejiandaa vizuri. Akizugumza jana baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Jang’ombe Boys kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi A, Mkude alisema kwamba hawana wasiwasi wowote kuelekea Nusu Fainali dhidi ya mahasimu, Yanga. “Sisi tumejiandaa vizuri, ni matumaini yetu na wao wamejiandaa vizuri, mchezo wa mpira wa miguu ni maandalizi, baada ya maandalizi tutakutana tutacheza, utakuwa mchezo mzuri, kipimo kizuri kwetu na kwao, dakika 90 zitaamua,”.
Jonas Mkude (kushoto) amesema mechi dhidi ya Yanga itakuwa ngumu kesho
Simba na Yanga zitakutana katika Nusu Fainali ya Pili ya Kombe la Mapinduzi kesho Saa 2:15 usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar.  Hiyo inafuatia Simba kumaliza kileleni mwa Kundi A kwa pointi zake 10, ikifuatiwa na Taifa Jang’ombe pointi tisa, Jang’ombe Boys pointi sita na URA pointi nne.  Ikumbukwe Yanga imeshika nafasi ya pili Kundi B nyuma ya Azam walioongoza kwa wastani wa mabao baada ya kufungana kwa pinti saba kila timu. Mabao yote ya Simba SC jana yalifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo moja kila kipindi. Nusu Fainali ya kwanza kesho itazikutanisha Azam FC na Taifa Jang’ombe Saa 10:30 jioni. Hiyo inafuatia Taifa kuwalaza waliokuwa mabingwa watetezi, URA ya Uganda 1-0 katika mchezo wa mwisho wa Kundi A usiku wa jana Uwanja wa Amaan. Bao pekee la Taifa Jang’ombe limefungwa na Mohammed Said kwa penalti, baada ya Ally Badru kuangushwa kwenye boksi. Mapema URA nao walipoteza penalti baada ya Bogota Labama kuangushwa kwene boksi.
 
 

MA DJ WA SAUZI WAUFAGILIA MUZIKI WA BONGO

Na Mwandishi Wetu,  DAR ES SALAAM WACHEZESHA disko ‘ma DJ’ maarufu Afrika Kusini Siyabonga Sibeko ‘DJ Capital’ na Lutendo Kungoane ‘Dj Sliqe’ wamesema kwamba muziki wa Tanzania uko juu kwa sasa. Wakizungumza na Waandishi wa Habari jana katika hoteli ya New Africa, Dar es Salaam ma DJ hao wa Redio na Telesheni nchini Afrika Kusini walisema Tanzania imepiga hatua kubwa kimuziki. “Kwa sasa huwezi kuzungumzia nchi zinazofanya vizuri kwa kiwango cha juu kimuziki Afrika bila kuitaja


Tanzanja,”alisema Dj Capital na kuongeza; “Afrika Kusini, Nigeria, Ghana, Tanzania na Kenya hizo ndizo nchi za Afrika zinazofanya vizuri katika muziki wa kisasa,”alisema. Kwa upande wake DJ Sliqe’ alisema kwamba anavutiwa zaidi na wasanii wawili wa Tanzania kwa sasa, ambao ni Diamond Platnumz na Vanessa Mdee. “Ni wasanii wengi wa Tanzania wanaofanya vizuri kwa sasa, lakini mimi upande wangu nawapenda zaidi hao wawili,”alisema.  Wawili hao, wote ni Ma DJ wa kituo cha Redio cha Touch Central cha Johannesburg, Afrika Kusini wakati DJ Capital pia anafanya kipindi cha Club 808 cha Televisheni ya ETV nchini humo. Wawili ambao wamekuja nchini kwa ziara ya wiki moja kujifunza zaidi kuhusu muziki wa Tanzania, pia ni Ma DJ wa kumbi za disko nchin kwao.  “Tumekuja hapa kujigunza na kukutana na wasnaii kwa sababu sisi pia ni watayarishaji wa muziki,”alisema Capital.
 

AZAM KUMENYANA NA TAIFA JANG’OMBE NUSU FAINALI MAPINDUZI

Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR TIMU ya Azam FC itamenyana na Taifa Jang’ombe katika Nusu Fainali ya kwanza Kombe la Mapinduzi Jumanne jioni Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Hiyo inafuatia Taifa kuwalaza waliokuwa mabingwa watetezi, URA ya Uganda 1-0 katika mchezo wa mwisho wa Kundi A usiku huu Uwanja wa Amaan. Bao pekee la Taifa Jang’ombe limefungwa na Mohammed Said kwa penalti, baada ya Ally Badru kuangushwa kwenye boksi. Mapema URA nao walipoteza penalti baada ya Bogota Labama kuangushwa kwene boksi.

Nusu Fainali ya Pili itawakutanisha watani wa jadi, Simba na Yanga Jumanne Saa 2:15 usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar.  Hiyo inafuatia Simba SC kushinda 2-0 dhidi ya Jang’ombe Boys jioni ya leo katika mchezo wa mwingine wa Kundi A. Matokeo hayo yanaifanya Simba imalize kileleni mwa Kundi A kwa pointi zake 10, ikifuatiwa na Taifa Jang’ombe pointi tisa, Jang’ombe Boys pointi sita na URA pointi nne.  Ikumbukwe Yanga imeshika nafasi ya pili Kundi B nyuma ya Azam walioongoza kwa wastani wa mabao baada ya kufungana kwa pinti saba kila timu. Mabao yote ya Simba SC leo yamefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo moja kila kipindi.
 

FA CUP: DROO YA RAUNDI YA 4 LEO, MABINGWA MAN UNITED KUWAKWAA NANI?


DROO YA RAUNDI YA 4 ya EMIRATES FA CUP itafanyika Leo Usiku kabla kuanza kwa Mechi ya mwisho ya Raundi ya 3 kati ya Cambridge and Leeds United.
Droo hiyo itafanyika huko BT Tower Mjini London na kuendeshwa na Wachezaji wa zamani wa Kimataifa wa England Michael Owen na Martin Keown.
Mechi 16 za Raundi ya 4 zitapangwa na kutakiwa kuchezwa Wikiendi ya Januari 28 na 29.
++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-FA CUP 2016/17, ambalo pia hujulikana kama FA Challenge Cup, ni mara ya 136 kushindaniwa kila Mwaka tangu lilipoanzishwe na linatambuliwa kama ndio Mashindano ya kale kupita yote Duniani.
-Kombe hili linadhaminiwa na Kampuni ya Ndege8k ya Emirates na kwa sababu za kiudhamini linaitwa Emirates FA Cup.
-Timu 736 zilikubaliwa kushiriki Mashindano haya Msimu huu na yalianza kwa Raundi ya Awali na yatafikia Tamati kwa Fainali itakayochezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Mei 27, 2017.
-Mshindi wa FA CUP ataingizwa Hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI Msimu wa 2017/18.
-Bingwa Mtetezi ni Manchester United.
+++++++++++++++++++
Mabingwa Watetezi Manchester United wamepewa Kipira Namba 3 ambacho kitawekwa ndani ya Mtungi pamoja na Vipira vingine 31ambavyo vitatolewa Mtungini na Owen na Keown kupambanisha Timu.
 NAMBA ZA VIPIRA KWA KILA TIMU:
1 Ipswich Town au Lincoln City
2 Rochdale
3 Manchester United 
4 Hull City 
5 Sunderland au Burnley
6 Blackburn Rovers
7 Millwall
8 Manchester City
9 Brighton & Hove Albion
10 Blackpool au Barnsley
11 Wigan Athletic au Nottingham Forest
12 Birmingham City au Newcastle United
13 Chelsea 
14 Middlesbrough 
15 Derby County 
16 Leicester City 
17 Liverpool au Plymouth Argyle 
18 Wycombe Wanderers
19 Watford
20 Arsenal
21 Fulham
22 Wolverhampton Wanderers
23 Cambridge United au Leeds United 
24 Bristol City au Fleetwood Town
25 Huddersfield Town
26 Tottenham Hotspur
27 Brentford
28 Bolton Wanderers au Crystal Palace
29 Norwich City au Southampton
30 Sutton United au AFC Wimbledon
31 Accrington Stanley
32 Oxford United
 

EFL CUP - NUSU FAINALI: JUMANNE KUANZA OLD TRAFFORD MAN UNITED v HULL CITY!


EFL CUP
Nusu Fainali
**Saa za Bongo
Jumanne Januari 10
2300 Manchester United v Hull City
Jumatano Januari 11
2245 Southampton V Liverpool
=============================
IMG-20170109-WA0000NUSU FAINALI za Kombe la Ligi hukoEngland ambalo sasa huitwa EFL CUP (English Football League Cup) zitaanza Jumanne Januari 10 huko Old Trafford kwa Manchester
 United kucheza na Hull City.
Siku ya Pili, Jumatano Januari 11, itachezwa Nusu Fainali ya Pili huko Saint Mary kwa Southampton kucheza na Liverpool.
Nusu Fainali hizi huchezwa kwa Mikondo Miwili ya Nyumbani na Ugenini na hivyo Marudiano ya Mechi hizi yatakuwa hapo Januari 25 na 26 huko Anfield na KCOM Stadium.
Kwenye Mechi ya Old Trafford, Meneja wa Man United Jose Mourinho amedokeza atabadili Kikosi chake toka kile kilichoichapa Reading 4-0 Jumamosi katika Raundi ya 3 ya FA CUP.
Akiongea baada ya Mechi hiyo, Mourinho alieleza: "Jumamosi tumecheza na Wachezaji freshi. Ila sitaki ieleweke tuna Timu ya Kwanza au ya Pili! Wachezaji ambao hawakucheza Mechi hii watacheza na Hull..hivyo ni rahisi kujua Zlatan, Pogba, Herrera, Valencia watarudi Mechi na Hull."
+++++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-Msimu huu hili Kombe la Ligi halina Mdhamini na limebatizwa English Football League Cup, EFL CUP.
-Huko nyuma Kombe la Ligi, kwa sababu za kiudhamini, liliwahi kubatizwa Coca-Cola Cup, Worthington Cup, Carling Cup na Capital One Cup.
+++++++++++++++++
Hull City, chini ya Meneja Mpya Marco Silva kutoka Ureno alietwaa mikoba ya Mike Phelan alietimuliwa Wiki iliyopita, itatinga Old Trafford ikiwa na Difensi ya kuungaunga kutokana na Majeruhi kadhaa.
Sentahafu wao Michael Dawson aliumia na kutolewa Kipindi cha Pili Juzi kwenye FA CUP walipoifunga Swansea City na nafasi hiyo kushikwa na Kiungo Tom Huddlestone alishirikiana na Kiungo mwingine Jake Livermore.
Beki mwingine Majeruhi wa Hull ni Curtis Davis na hivyo kuwaacha Hull kutumia Viungo Watatu kwenye Nafasi 4 za Difensi yao.
Nafasi ya Fulbeki wa Kulia imelazimika kuzibwa na David Meyler baada kumpoteza Ahmed Elmohamady ambae ameenda Egypt kujiunga na Timu ya Taifa kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2017, yanayoanza huko Gabon Januari 14.
EFL CUP
Nusu Fainali
MARUDIANO
**Saa za Bongo
Jumatano Januari 25
2300 Liverpool v Southampton
Alhamisi Januari 26
2245 Hull City v Manchester United

Alhamisi, 5 Januari 2017

ALHAMISI KATIKA MICHEZO TAEHE 05/01/2017


MKEKA.jpg




Mfumo wa Kocha George Lwandamina umeanza kuwashitua baadhi ya wapinzani wa Yanga katika michuano ya Mapinduzi.
Yanga imekuwa ikitumia pasi ndefu za katikati ya uwanja kutengeneza mabao na inaonekana Thabani Kamusoko na Haruna Niyonzima ndiyo wamepewa jukumu hilo.

Wawili hao, wamekuwa wakipiga pasi ndefu kwa Amissi Tambwe, Donald Ngoma au Simon Msuva ambao wamekuwa wakimalizia pasi hizo.

Taarifa zinaeleza, ndani ya vikosi vya Simba na Azam FC, gumzo la mabao ya Yanga na pasi zinazopigwa limekuwa gumzo.

"Ni kweli, unaona kabisa kuna aina fulani ya kitu kinafundishwa. Tunajua na tunafuatilia. Haina maana tutacheza kama Yanga lakini lazima uwajue wapinzani wako mapema," alisema mmoja ya wahusika ndani ya Simba lakini akaomba kutotajwa jina.

"Kama mwenzako anafanya kazi vizuri, basi lazima ujifunze au uangalie unafanyaje vizuri zaidi yake au unaweza kumshinda."
Lakini upande wa Azam FC, John Bocco ambaye ni nahodha alisema wanaona kila kitu na wanajiandaa.

"Kweli kuna mambo mengi ya kujifunza kila unapocheza. Yanga ni timu kubwa, wamefunga mabao mengi lakini sisi tuna kikosi bora. Kina uwezo wa kupambana na kila mfumo," alisema.

Tayari Yanga imefuzu katika hatua ya mtoano baada ya ushindi mara mbili mfululizo
 



Kiungo mwenye kasi wa Yanga, Simon Msuva wa Yanga, amesema anautaka ufungaji bora na uchezaji bora wa Kombe la Mapinduzi.

Msuva amesema angependa kupata ufungaji bora wa michuano hiyo kwa mara ya pili. Kwa sasa anaongoza kwa kuwa na mabao manne ya kufunga.

“Kweli nataka ufungaji bora, niliwahi kuwa mfungaji bora wa Mapinduzi,” alisema.

“Kwa ushirikiano na wenzangu kwenye timu, ningependa kwua mfungaji bora. Kawaida ushirikiano unamsaidia mtu kuwa bora zaidi,” alisema.


Katika mechi mbili dhidi ya Jamhuri ambayo Yanga ilishinda kwa mabao 6-0 na ule dhidi ya Zimamoto, ikishinda mabao 2-0. Msuva alifunga mabao mawili kila mechi
 

DIAMOND KUTUMBIZA TUZO ZA MWANASOKA BORA AFRIKA LEO ABUJA

Na Mahmoud Zubeiry, DAR E SALAAM MWANAMUZIKI nyota Tanzania, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ na wasanii wengine wakubwa barani, wanatarajiwa kutumbuiza usiku wa leo katika sherehe za tuzo Mwanasoka Bora Afrika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano mjini Abuja, Nigeria. Diamond anaweka rekodi nyingine kubwa katika historia yake ya muziki kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kutumbuiza kwenhye tuzom hizo kubwa barani.  Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borussia Dortmund ya Ujerumani atatetea tuzo yake ya Mwanasoka Bora Afrika dhidi ya Riyad Mahrez wa Algeria na Leicester City na Sadio Mane wa Senegal na Liverpool.
Diamond Platnumz anatumbuiza usiku wa leo katika sherehe za tuzo Mwanasoka Bora Afrika mjini Abuja, Nigeria
Miongoni mwa wanamuziki hao, ni mtoto gwiji wa muziki Afrika, Fela-Anikulapo Kuti, aitwaye Femi Kuti.  Kuti, ambaye alianzisha bendi yake mwenyewe ya Positive Force mwaka 1986 anafahamika kwa muziki wake mzuri.  Amejitambulisha kama gwiji kweli Afro Beat kwa staili yake mwenyewe na moja ya nyimbo zake zinazobamba ni Beng, Beng, Beng. Msanii mwingine anayetarajiwa kutumbuiza usiku wa leo ni dansa, mwandishi wa nyimbo na mtumbuizaji, Chinedu Okoli, maarufu Flavour N’abania wa Nigeria.  Flavour anafahamika barani na nchi nyingine duniani kwa kibao chake cha kuwarusha watu ‘klabu’ kiitwacho Nwa Baby.  Pia watakuwepo Diamond Platinumz mkali wa Bongo Flava kutoka Tanzania ambaye anatamba na kibao chake Salome kwa sasa. Wengine ni Omawumi anayetamba na nyimbo za Megbele na If you ask Me, kundi la Muffinz kutoka Afrika Kusini, Yemi Alade na DJ Jimmy Jatt. Wakati huo huo; Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou aliwasili mjini Abuja jana na kupokewa na Makamu wake wa kwanza, Almamy Kabele Camara; Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Adoum Djibrine, Rais wa Shirikkisho la Soka Nigeria, Amaju Pinnick na Maofisa mbalimbali wa Globacom, wadhamini wa tuzo shughuli hiyo.

Pierre-Emerick Aubameyang anatetea tuzo yake dhidi ya Riyad Mahrez na Sadio Mane
TATU BORA YA TUZO MBALIMBALI LEO Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund) Riyad Mahrez (Algeria & Leicester City) Sadio Mane (Senegal & Liverpool) Mwanasoka Bora wa Mwaka Anayecheza Afrika Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns) Khama Billiat (Zimbabwe & Mamelodi Sundowns) Rainford Kalaba (Zambia & Tp Mazembe) Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Kike Asisat Oshoala (Nigeria & Arsenal Ladies) Elizabeth Addo (Ghana & Kvarnsvedensik) Gabrielle Aboudi Onguene (Cameroon & Rossyanka) Mwanasoka Bora Anayechipukia Elia Meschak (Dr Congo & Tp Mazembe)    Kelechi Iheanacho (Nigeria & Manchester City) Naby Keita (Guinea & Rb Leipzig) Mwanasoka Bora Kijana wa Mwaka Alex Iwobi (Nigeria And Arsenal) Eric Ayiah (Ghana And Charity Fc)         Sandra Owusu-Ansah (Ghana And Supreme Ladies) Kocha Bora wa Mwaka Florent Ibenge (Timu ya taifa DRC) Pitso Mosimane (Mamelodi Sundowns)  Florence Omagbemi (Timu ya taifa ya wanawake ya Nigeria) Klabu Bora ya Mwaka Mamelodi Sundowns  Tp Mazembe      Zesco United Timu Bora ya Taifa ya Mwaka DRC Senegal  Uganda Timu Bora ya Taifa ya Wanawake ya Mwaka Cameroon Nigeria   Afrika Kusini Refa Bora wa Mwaka Bakary Papa Gassama       Ghead Zaglol Grisha      Malang Diedhiou             Kiongozi Bora wa Soka wa Mwaka Manuel Lopes Nascimento Rais wa Shirikisho la Soka Guinea Bissau Tuzo ya Gwiji Laurent Pokou, mchezaji wa zamani wa Ivory Coast Emilienne Mbango, mchezaji wa zamani wa Cameroon

Kipa Denis Onyango wa Uganda anawania Tuzo ya mchezaji Bora Anayecheza Afrika, baada ya kuipa Mamelodi Sundowns taji la Ligi ya Mabingwa
Kikosi Bora wachezaji 11 Kipa: Denis Onyango (Uganda na Mamelodi Sundowns)  Mabeki: Serge Aurier (Ivory Coast na Paris Saint-Germain), Aymen Abdennour (Tunisia na Valencia), Eric Bailly (Ivory Coast & Manchester United), Joyce Lomalisa (DRC na As Vita) Viungo: Khama Billiat (Zimbabwe & Mamelodi Sundowns), Rainford Kalaba (Zambia & Tp Mazembe), Keegan Dolly (Afrika Kusini & Mamelodi Sundowns), Washambuliaji: Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund), Sadio Mane (Senegal & Liverpool), Riyad Mahrez (Algeria & Leicester City)  Wa akiba; Aymen Mathlouthi (Tunisia & Etoile Du Sahel), Kalidou Koulibaly (Senegal & Napoli), Salif Coulibaly (Mali & Tp Mazembe), Islam Slimani (Algeria & Leicester City), Mohamed Salah (Misri & Roma), Kelechi Iheanacho (Nigeria & Manchester City), Alex Iwobi (Nigeria And Arsenal)

Samuel Eto'o wa Cameroon anashikilia rekodi ya kushinda tuzo nyingi za Mwanasoka Bora Afrika 
WALIOWAHI KUWA WANASOKA BORA AFRIKA 1992 Abedi Ayew Pele (Ghana) 1993 Rashidi Yekini (Nigeria) 1994 Emmanuel Amunike (Nigeria) 1995 George Weah (Liberia) 1996 Nwankwo Kanu (Nigeria) 1997 Victor Ikpeba (Nigeria) 1998 Mustapha Hadji (Morocco) 1999 Nwankwo Kanu (Nigeria) 2000 Patrick Mboma (Cameroon) 2001 El-Hadji Diouf (Senegal) 2002 El Hadji Diouf (Senegal) 2003 Samuel Eto'o (Cameroon) 2004 Samuel Eto'o (Cameroon) 2005 Samuel Eto'o (Cameroon) 2006 Didier Drogba (Ivory Coast) 2007 Frederic Kanoute (Mali) 2008 Emmanuel Adebayor (Togo) 2009 Didier Drogba (Ivory Coast) 2010 Samuel Eto'o (Cameroon) 2011 Yaya Toure (Ivory Coast) 2012 Yaya Toure (Ivory Coast) 2013 Yaya Toure (Ivory Coast) 2014 Yaya Toure (Ivory Coast) 2015 Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon) 2016  ?????
 

SIMBA NA URA KATIKA BONGE LA MECHI LEO KOMBE LA MAPINDUZI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM SIMBA SC inakamilisha mechi zake za Kundi A Kombe la Mapinduzi, kwa kumenyana na mabingwa watetezi, URA ya Uganda usiku wa leo. Mchezo huo utakaotanguliwa na mechi nyingine ya kundi hilo kati ya KVZ na Jang'ombe Boys kuanzia Saa 10:00 jioni, itaanza Saa 2:30 usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Simba inayofundishwa na kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog itahitaji ushindi ili kuongoza kundi na kukwepa kukutana na wapinzani wa jadi, Yanga mapema. Lakini hilo litakuwa gumu mbele ya URA ambayo nayo itahitaji zaidi ushindi kwanza kujihakikishia tiketi ya Nusu Fainali.
Simba inaongoza kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na URA, Taifa Jang’ombe na Jang’ombe Boys zenye pointi tatu kila mmoja.’ Maana yake URA haina namna nyingine zaidi ya kushinda ili kuzipiku Taifa na Jang’ombe katika kinyang’anyiro cha tiketi ya Nusu Fainali. Simba kutaka ushindi na URA pia kutaka kushinda lazima kunamaanisha mechi yao leo ni nzuri.   Katika mechi ya Kundi B usiku wa jana, Azam FC ililazimishwa sare ya bila kufungana na Jamhuri ya Pemba Uwanja wa Amaan. Kwa sare hiyo, Azam inafikisha pointi tatu na kuendelea kubaki nafasi ya pili nyuma ya Yanga, yenye pointi sita, ambayo jana jioni iliifunga Zimamoto 2-0. Azam sasa itacheza mechi yake ya mwisho Jumamosi dhidi ya Yanga, mchezo ambao utatanguliwa na mechi kati Zimamoto na Jamhuri. 
CHANZO BIN ZUBERY
SALEHE 

Jumatano, 4 Januari 2017

MICHEZOOO

 

..

...

.

PLAZA.jpg

JEMBE1.jpg

MKEKA.jpg

FARID SASA ANGOJA LESENI TU YA RFEF AANZE KAZI SEGUNDA


WINGA chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Farid Malik Mussa amesema kwamba anasubiri leseni ya Mamlaka ya Shirikisho la Soka Hispania (RFEF) aanze kuchezea klabu yake, Club Deportivo Tenerife. Farid amejiunga na klabu hiyo ya Santa Cruz de Tenerife, Tenerife, visiwa vya Canary mwezi huu kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu kutoka Azam FC ya Dar es Salaam. Na tangu afike wiki iliyopita amekuwa akifanya mazoezi tu na timu hiyo ya Daraja la Kwanza, maarufu kama Segunda Division, inayotumia Uwanja wa Heliodoro Rodriguez Lopez wenye kuchukua mashabiki 23,660.
Farid Mussa Malik akiwa na vifaa vya michezo alivyopatiwa baada ya kuwasili Tenerife
Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online kwa simu jana usiku, Farid alisema anaendelea vizuri tangu afike na amekuwa akifanya mazoezi na wenzake, lakini hajaanza kicheza Ligi kwa sababu ya leseni. “Nadhani leseni itatoka wakati wowote. Sitarajii kama itachelewa,”alisema Farid. Azam FC imemtoa kwa mkopo Farid kwenda CD Tenerife kwa makubaliano maalum baada ya winga huyo kufuzu majaribio katika klabu hiyo Aprili mwaka jana alipokwenda na Mkurugenzi wa klabu yake, Yussuf Bakhresa. Farid alitua Hispania Aprili 21 baada ya kuichezea Azam FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance mjini Tunis, Tunisia ikifungwa 3-0 na kutolewa kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya awali kushinda 2-1 Dar es Salaam. Na ilimchukua wiki moja tu Farid kuwakuna kwa kipaji chake makocha wa Tenerife na kutaka kumnunua, lakini Azam ikakataa na kuamua kumtoa kwa mkopo

SIMBA YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI

Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR SIMBA SC imekwenda Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KVZ usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Ushindi huo uliotokana na bao pekee la kiungo Muzamil Yassin dakika ya 43, unaifanya Simba SC ifikishe pointi sita baada ya kucheza mechi mbili. Sifa zaidi zimuendee beki Abdi Hassan Banda aliyeyafanikiwa kuvunja mtego wa kuotea wa KVZ ma kumchomea pasi nzuri Muzamil aliyekwenda kufunga.
Huu unakuwa ushindi wa pili mfululizo kwa Simba katika michuano hii, baada ya juzi kuilaza Taifa Jang’ombe 2-1. KVZ ilimaliza pungufu mchezo huo baada ya beki wake, Rashid Omar Rashid kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kumkwatua mshambuliaji wa Simba, Pastory Athanas nje kidogo ya boksi akiwa anakwenda kufunga.  Katika mchezo wa Kundi A uliotangulia leo, Jang’ombe Boys iliwalaza mabingwa watetezi, URA ya Uganda 2-1. Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi za Kundi B, kati ya Zimamoto na Yanga kuanzia Saa 10:00 jioni na Jamhuri dhidi ya Azam kuanzia Saa 2:30 usiku. Kikosi cha Simba leo kilikuwa; Daniel Agyei, Janvier Besala Bokungu, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Method Mwanjali, Abdi Banda, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, James Kotei, Athanas Pastory, Juma Luizio na Muzamil Yassin. KVZ; Abdallah Bakari, Saleh Nassor, Makarani Mluchu, Rashid Omar, Said Mohammed, Suleiman Ali, Suleiman Hassan, Suleiman Juma, Sultan Kasikasi, Mohammed Maulid na Masoud Abdllah.

LALA SALAMA LIGI YA WANAWAKE YAANZA KESHO KARUME

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM DURU la Pili la Ligi Kuu soka ya Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatarajiwa kuanza kesho Jumatano Januari 4, 2017 kwa michezo minne itakayofanyika kwenye viwanja mbalimbali. Kwa mujibu wa ratiba, katika kundi ‘A’ pekee litakuwa na mchezo mmoja wakati kundi ‘B’ litakuwa na michezo mitatu kwa siku ya kesho Jumatano. Mchezo pekee wa kesho wa kundi ‘A’ utakuwa kati ya Mburahati Queens ya Kinondoni, Dar es Salaam na Viva Queens ya Mtwara – mchezo utakaofanyika Uwanja wa Karume jijini katika mzunguko wa sita wa ligi hiyo.
Michezo mingine mitatu itakuwa ni ya Kundi B ambako Mejengo FC itacheza na Marsh Academy ya Mwanza kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida wakati Panama ya Iringa inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Sisterz ya Kigoma kwenye Uwanja wa Samora huku Victoria Queens ikiikaribisha Baobab ya Dodoma kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera. Kabla ya michezo ya juma lijalo, upande wa Kundi A michezo yake miwili ya mzunguko wa sita itafanyika Alhamisi Januari 5, mwaka huu ambako Evergreen ya Temeke, Dar es Salaam itacheza na Fair Play ya Tanga kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam. Mlandizi ya Pwani inatarajiwa kuikaribisha JKT Queens ya Dar es Salaam, katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Mabatini.

DILI LA HAJIB MISRI LAINGIWA UKAKASI


BIASHARA ya mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Hajib kwenda Haras El Hodoud ya Misri inaelekea kama kutokamilika kwa sasa. Dirisha la usajili la Misri lilifungwa juzi na Haras El Hodoud hawakuwa wamefanya mawasiliano yoyote na Simba SC hadi jana jioni. Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Hajji Sunday Manara alisema jana katika mazungumzo na Bin Zubeiry Sports - Online kwamba klabu yake haijapokea ofa yoyote kutoka kwa Haras El Hodoud. “Sijui wanategemea nini, maana dirisha la usajili la kwao linafungwa leo (jana). Sasa sijui wana mpango gani,”alisema Manara.
Ibrahim Hajib (kushoto) akiwa na wachezaji wa Haras El Hodoud nchini Misri
Juzi Hajib alisema kwamba amefanya mazungumzo ya awali na Haras El Hodoud na kufikia makubaliano, lakini kwanza wanatakiwa kumalizana na klabu yake ya sasa, Simba SC. “Ninamshukuru Mungu nimefurahia siku zangu chache za kuwa Alexandria, nilikuwa katika klabu nzuri, mazingira mazuri na wachezaji wenzangu kule wamenikubali mapema sana. Sasa baada ya yote, ninawasikilizia wao tu ni jinsi gani watalimalizia hili suala,”alisema. Hajib alirejea nchini juzi na kusema kwamba atajiunga na timu itakayompa ofa nzuri kati ya Haras El Hodoud ya Misri na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini inayomtaka pia. Pamoja na kufuzu majaribio na vipimo vya afya Haras El Hodoud, lakini imeripotiwa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini pia inatamaka mchezaji huyo wa Simba kwa kusaini naye mkataba moja kwa moja bila majaribio. “Ni kweli nimesikia hizo habari, na si Kaizer tu, timu nyingine kama mbili za Afrika Kusini nazo zimetangaza ofa. Kwanza ninamshukuru Mungu. Mungu ni mkubwa, sasa tusubiri haya maneno yawe vitendo ndiyo tufanye maamuzi,” alisema Hajib. Wakala anayeshughulikia mipango ya Hajib nchini Afrika Kusini, Rodgers Mathaba kwa upande wake alikiri juu ya mchezaji huyo kutakiwa na Kaizer Chiefs. “Ni kweli, Kaizer wanamtaka Hajib. Najua alikuwa Misri, nasubiri arejee Dar es Salaam nimpigie simu nizungumze naye. Tayari nimekwishazungumza na kocha Steve Khompela wa Kaizer,”alisema. Hajib alikuwa ana wiki nzuri ya majaribio Haras El Hodoud ikiwemo kufunga bao moja katika ushindi wa 4-0 kwenye mchezo wa kirafiki Ijumaa. Mathaba ndiye aliyempeleka Hajib Afrika Kusini kwa majaribio pia, klabu ya Lamontville Golden Arrows FC ya Ligi Kuu ya ABSA nchini humo na pamoja na kufuzu, wakamtaka arejee Simba kumalizia Mkataba ili baadaye aende kama mchezaji huru. 

YANGA YAANZA NA MOTO KOMBE LA MAPINDUZI, JAMHURI YAFA 6-0


YANGA SC imeanza kwa kishindo michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar baada ya kuichapa mabao 6-0 Jamhuri ya Pemba usiku huu Uwanja wa Amaan. Ushindi huo, unaifanya Yanga iongoze Kundi B, kwa pointi zake tatu sawa na Azam iliyoshinda 1-0 dhidi ya Zimamoto katika mchezo wa kwanza jioni ya leo. Winga Simon Msuva alifungua biashara nzuri dakika ya 19 akiifungia Yanga bao la  kwanza kwa kumalizia kona maridadi ya Nahodha, kiungo Haruna Niyonzima kutoka Rwanda. Mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Ngoma akaifungia Yanga mabao mawili mfululizo daakika ya 23 akimalizia krosi ya Mwinyi Hajji Mngwali na dakika ya 37 baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa, Omary Said kufuatia shuti la Msuva.
Donald Ngoma (kushoto) akikimbia kushangilia baada ya kufunga, huku mabeki wa Jamhuri wakiwa wameduwaa
Msuva tena akawainua vitini mashabiki wa Yanga baada ya kufunga baola nne dakika ya 40 akitumia makosa ya kiopa kutoka langoni bila mahesabu. Baada ya kumaliza kipindi cha kwanza na mtaji wa mabao 4-0, kocha wa Yanga, George Lwandamina akakianza kipindi cha pili kwa mabadiliko, akimpumzisha kiungo Mzambai mwenzake, Justin Zulu na nafasi yake kuchukuliwa na mzalendo, Said Juma ‘Makapu’. Kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko akaifungia Yanga bao la tano dakika ya 59 akimalizia krosi ya Juma Abdul, kabla ya kiungo Juma Mahadhi⁠⁠⁠⁠⁠ aliyetokea benchi pia kipindi cha pili kuhitisha tafrija za mabao kwa kufunga la sita dakika ya 85 kwa shuti la karibu. Katika mchezo huo, nafasi pekee nzuri ambayo Jamhuri walipoteza ilikuwa ni mapema atu dakika ya 13 baada ya krosi ya Ahmed Ali kuokolewa na beki wa Yanga Andrew Vincent ‘Dante’ na  kuwa  kona  iliyochongwa  na Mohamed  omary  ambayo  haikuza  matunda  baada  ya  beki  huyo kuokoa tena. Kikosi cha Yanga kilikuwa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Kelvin Yondan/Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dk72, Vincent Andrew ‘Dante’, Justin Zulu, Simoni Msuva/Geoffrey Mwashiuya dk77, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma/Juma Mahadhi dk66, Haruna Niyonzima/Deus Kaseke dk66 na Emmanuel Martin. Jamhuri: Omary Said, Mohammed Mgau, Mohammed Omary, Mohammed Juma, Yussuf Makame,  Greyson Gerald, Umry Bagaseka, Mbarouk  Suleiman, Mwalimu  Mohammed, Ahmed Ally na  Mussa Mbarouk.

TFF YAACHANA NA MKWASA, MAYANGA KOCHA MPYA STARS


RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtangaza Salum Mayanga kuwa kocha mpya wa muda wa timu ya taifa, Taifa Stars. Malinzi amesema leo kwamba hiyo inafuatia aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa kumaliza Mkataba wake leo. Majukumu ya Mayanga yatakuwa ni kuandaa kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo mechi za awali zitanza mapema mwaka huu. Mayanga atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya mechi za kufuzu CHAN. TFF inamshukuru Kocha Charles Boniface Mkwasa kwa utumishi katika nafasi hiyo ulioanza Julai, 2015 akimrithi Mholanzi, Mart Nooij na kumtakia mafanikio katika mipango yake inayofuata. Katika kipindi chake cha kuwa Taifa Stars, Mkwasa ameiongoza timu katika mechi 13, ikishinda mbili, kufungwa sita na sare tano.

Chini ya Charles Boniface Mkwasa (kulia) Taifa Stars, imeshinda mechi mbili tu kati ya 13, ikifungwa sita na sare tano
REKODI YA MKWASA TAIFA STARS Tanzania 1-1 Uganda (Kufuzu CHAN, Kampala) Tanzania 1-2 Libya (Kirafiki Uturuki) Tanzania 0-0 Nigeria (Kufuzu AFCON Dar) Tanzania 2-0 Malawi (Kufuzu Kombe la Dunia Dar) Tanzania 0-1 Malawi (Kufuzu Kombe la Dunia Blantyre) Tanzania 0-2 Afrika Kusini U23 (Kirafiki Johannesburg) Tanzania 2-2 Afrika Kusini U23 (Kufuzu Kombe la Dunia Dar) Tanzania 2-2 Afrika Kusini U23 (Kufuzu Kombe la Dunia Dar) Algeria 7-0 Tanzania (Kufuzu kombe la Dunia Blida) Tanzania 1-0 Chad (Kufuzu AFCON D’jamena) Tanzania 0-2 Misri (Kufuzu AFCON Taifa) Tanzania 1-1 Kenya (Kirafiki Nairobi) Tanzania 0-3 Zimbabwe (Kirafiki Harare)

AZAM YAANZA VYEMA KOMBE LA MAPINDUZI


BAO pekee la mshambuliaji chipukizi, Shaaban Iddi Chilunda limetosha kuipa Azam FC ya Dar es Salaam ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Zimamoto katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mapinduzi. Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar jioni ya leo, Chilunda alifunga bao hilo dakika ya 79 akimvisha kanzu kipa baada ya kuipokea kiufundi kwa kifua pasi ya juu ya kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’.  Ushindi huo unaifanya Azam FC kuongoza Kundi B ikiwa na pointi tatu, ambapo hivi sasa itasubiria mchezo wa pili wa kundi hilo utakazoihusisha Yanga na Jamhuri ili kujua kama itaendelea kukaa kileleni. Winga wa kushoto wa Azam FC kutoka Ghana, Enock Atta Agyei, alianza kuichezea mechi ya kwanza ya mashindano timu hiyo tokea aliposajiliwa, hii ni baada ya kushindwa kuitumikia kwenye Ligi Kuu kufuatia kutotimiza umri wa miaka 18, ambapo kwenye ligi ataanza kuonekana baada ya kutimiza umri huo Januari 5 mwaka huu.
Shaaban Iddi (katikati) akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga jana
Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii walianza mchezo huo kwa kasi ya chini kabla ya kubadilika dakika 20 za mwisho za kipindi cha pili, ambapo mshambuliaji Samuel Afful, alikaribia kuiandikia bao la uongozi Azam FC dakika ya 30 baada ya kuwatoka mabeki wa Zimamoto lakini shuti alilopiga lilimbabatiza kipa na kuokolewa na mabeki. Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, timu zote ziliweza kutoka nguvu sawa ya bila kufungana, katika dakika 10 za mwanzo za kipindi cha pili Azam FC ilifanya mabadiliko ya kumtoa Afful na kuingia Shaaban ambaye alienda kufunga bao la ushindi. Kabla ya kufunga bao hilo, Shaaban huenda angetangalia kufunga jingine kama angekuwa makini kutumia pasi safi ya Enock Atta Agyei dakika ya 59, lakini aliukosa mpira wakati kiwa kwenye harakati za kuupiga mpira. Azam FC iliweza kuulinda ushindi huo hadi dakika 90 zinamalizika, ambapo itashuka tena dimbani Keshokutwa Jumatano kucheza dhidi ya Jamhuri mchezo utakaofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar saa 2.15 usiku. Kikosi cha Azam FC kilikuwa: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Yakubu Mohammed, Stephan Kingue, Salum Abubakar, Frank Domayo/Mudathir Yahya dk 77, Yahaya Mohammed, Samuel Afful/Shaaban Idd dk 50, Enock Atta/Ramadhan Singano dk 67. 


Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR SIMBA SC imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Taifa Jang’ombe mabao 2-1 katika mchezo wa Kundi A usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.  Hadi mapumziko, Simba walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na wachezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar, Muzamil Yassin na Juma Luizio. Kiungo Muzamil Yassin alianza kuifungia Simba dakika ya 27 baada ya kuwahi mpira uliogonga mwamba na kurudi kufuatia shuti la beki Mzimbabwe, Method Mwanjali ambalo lilimshinda kipa Ahmed Suleiman.
Mshambuliaji Juma Luizio akafunga kwa shuti la umbali wa mita 17 baada ya kuwatoka mabeki wawili wa Taifa, kufuatia pasi ya Muzamil Yassin. Luizio anayecheza kwa mkopo kutoka Zesco United ya Zambia akiichezea kwa mara ya pili Simba leo, alidumu uwanjani kwa dakika 60 tu kabla ya kumpisha Mrundi, Laudit Mavugo.  Beki wa kati wa Simba, Novaty Lufunga akajifunga kwa kichwa katika harakati za kuokoa mpira wa kona uliochongwa na Hassan Bakari dakika ya 76 kuipatia Taifa bao la kufutia machozi. Katika mchezo uliotangulia, URA iliichapa 2-0 KVZ. Simba sasa inalingana kwa pointi na URA na Taifa iliyoifunga Jang’ombe Boys 1-0 katika mchezo wa kwanza Ijumaa. Kikosi cha Simba leo kilikuwa; Daniel Agyei, Hamad Juma, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, James Kotei, Shiza Kichuya/Mwinyi Kazimoto, Muzamil Yassin, Juma Luizio/Laudit Mavgugo dk60, Said Ndemla na Jamal Mnyate/Moses Kitundu dk66. Taifa Jang’ombe; Ahmed Suleiman, Adam Hamad, Saleh Mgeni/Hassan Bakari dk59, Abdallah Shaibu, Samir Yahya, Khatib Simai, Ally Mlanga, Baraka Ushindi/Mohmed Salum ‘Messi’ dk56, Seif Hassan, Adam Ibrahim/Method Apigi dk62 na Yahya Tumbo/Nelson Gabriel dk72.  

SIMBA YAANZA VYEMA KOMBE LA MAPINDUZI, LUIZIO AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO

Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR SIMBA SC imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Taifa Jang’ombe mabao 2-1 katika mchezo wa Kundi A usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.  Hadi mapumziko, Simba walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na wachezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar, Muzamil Yassin na Juma Luizio. Kiungo Muzamil Yassin alianza kuifungia Simba dakika ya 27 baada ya kuwahi mpira uliogonga mwamba na kurudi kufuatia shuti la beki Mzimbabwe, Method Mwanjali ambalo lilimshinda kipa Ahmed Suleiman.
Mshambuliaji Juma Luizio akafunga kwa shuti la umbali wa mita 17 baada ya kuwatoka mabeki wawili wa Taifa, kufuatia pasi ya Muzamil Yassin. Luizio anayecheza kwa mkopo kutoka Zesco United ya Zambia akiichezea kwa mara ya pili Simba leo, alidumu uwanjani kwa dakika 60 tu kabla ya kumpisha Mrundi, Laudit Mavugo.  Beki wa kati wa Simba, Novaty Lufunga akajifunga kwa kichwa katika harakati za kuokoa mpira wa kona uliochongwa na Hassan Bakari dakika ya 76 kuipatia Taifa bao la kufutia machozi. Katika mchezo uliotangulia, URA iliichapa 2-0 KVZ. Simba sasa inalingana kwa pointi na URA na Taifa iliyoifunga Jang’ombe Boys 1-0 katika mchezo wa kwanza Ijumaa. Kikosi cha Simba leo kilikuwa; Daniel Agyei, Hamad Juma, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, James Kotei, Shiza Kichuya/Mwinyi Kazimoto, Muzamil Yassin, Juma Luizio/Laudit Mavgugo dk60, Said Ndemla na Jamal Mnyate/Moses Kitundu dk66. Taifa Jang’ombe; Ahmed Suleiman, Adam Hamad, Saleh Mgeni/Hassan Bakari dk59, Abdallah Shaibu, Samir Yahya, Khatib Simai, Ally Mlanga, Baraka Ushindi/Mohmed Salum ‘Messi’ dk56, Seif Hassan, Adam Ibrahim/Method Apigi dk62 na Yahya Tumbo/Nelson Gabriel dk72.  

KOMBE LA MAPINDUZI, LUIZIO AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO

Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR SIMBA SC imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Taifa Jang’ombe mabao 2-1 katika mchezo wa Kundi A usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.  Hadi mapumziko, Simba walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na wachezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar, Muzamil Yassin na Juma Luizio. Kiungo Muzamil Yassin alianza kuifungia Simba dakika ya 27 baada ya kuwahi mpira uliogonga mwamba na kurudi kufuatia shuti la beki Mzimbabwe, Method Mwanjali ambalo lilimshinda kipa Ahmed Suleiman.
Mshambuliaji Juma Luizio akafunga kwa shuti la umbali wa mita 17 baada ya kuwatoka mabeki wawili wa Taifa, kufuatia pasi ya Muzamil Yassin. Luizio anayecheza kwa mkopo kutoka Zesco United ya Zambia akiichezea kwa mara ya pili Simba leo, alidumu uwanjani kwa dakika 60 tu kabla ya kumpisha Mrundi, Laudit Mavugo.  Beki wa kati wa Simba, Novaty Lufunga akajifunga kwa kichwa katika harakati za kuokoa mpira wa kona uliochongwa na Hassan Bakari dakika ya 76 kuipatia Taifa bao la kufutia machozi. Katika mchezo uliotangulia, URA iliichapa 2-0 KVZ. Simba sasa inalingana kwa pointi na URA na Taifa iliyoifunga Jang’ombe Boys 1-0 katika mchezo wa kwanza Ijumaa. Kikosi cha Simba leo kilikuwa; Daniel Agyei, Hamad Juma, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, James Kotei, Shiza Kichuya/Mwinyi Kazimoto, Muzamil Yassin, Juma Luizio/Laudit Mavgugo dk60, Said Ndemla na Jamal Mnyate/Moses Kitundu dk66. Taifa Jang’ombe; Ahmed Suleiman, Adam Hamad, Saleh Mgeni/Hassan Bakari dk59, Abdallah Shaibu, Samir Yahya, Khatib Simai, Ally Mlanga, Baraka Ushindi/Mohmed Salum ‘Messi’ dk56, Seif Hassan, Adam Ibrahim/Method Apigi dk62 na Yahya Tumbo/Nelson Gabriel dk72.  

Wednesday, January 4, 2017

TUZO ZA CAF KUTOLEWA KESHO.

SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF kesho linatarajia kufanya sherehe ya kutoa tuzo kwa wachezaji mbalimbali wa soka waliofanya vizuri katika kipindi cha mwaka mzima uliopita. Sherehe hizo zinakuwa ni za 25 toka kuanzishwa kwake na zinatarajiwa kufanyika jijini Abuja, Nigeria kwa mara ya pili mfululizo. Kwenye sherehe hizo atapatikana mfalme wa soka Afrika ambapo miongoni mwao ni pamoja na mshindi wa tuzo ya mwaka jana Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon, Riyad Mahrez wa Algeria na Sadio Mane anayetoka Senegal. Kuanzia mwaka 1992 zilipoanzishwa tuzo hizo ambapo ilikwenda kwa nguli wa zamani wa Ghana Abeid Ayew Pele mpaka mwaka jana alipotwaa Aubameyang ni jumla ya wachezaji 15 waliofanikiwa kutwaa hiyo. Nyota wa Cameroon Samuel Eto’o ndio mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo hiyo mara nne mfululizo mwaka 2003, 2004, 2005 na 2010 kabla ya Yaya Toure wa Ivory Coast hajaivunja rekodi hiyo kwa kutwaa kuanzia mwaka 2011 mpaka 2014.
 
 

HULL CITY YAMTIMUA MENEJA WAKE.

KLABU ya Hull City imeamua kumtimua meneja wake Mike Phelan kufuatia kuendelea kuvurunda kwa timu hiyo katika Ligi Kuu. Phelan mwenye umri wa miaka 54 alichukua mikoba kama kocha wa muda kufuatia kuondoka kwa Steve Bruce majira ya kiangazi na kufanikiwa kuteuliwa kuchukua nafasi hiyo moja kwa moja Octoba mwaka jana. Lakini kufuatia Hull City kuburuza mkia katika msimamo wa ligi huku wakiwa wameambulia alama tatu pekee katika mechi tisa za mwisho, klabu imeamua kuachana na kocha huyo. Katika taarifa yake klabu hiyo imedai kuwa kwasasa wanatafuta mbadala wa Phelan na watamtangaza hivi karibuni.

CONTE AWAPASHA WANAOSEMA TIMU YAKE INAPENDELEWA.

MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte amedai kuwa ratiba yao ya msimu wa sikukuu inakosolewa kwasababu wako kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu. Chelsea wana nafasi kubwa ya mapumziko katika ratiba yao kuliko timu yeyote kwenye kipindi hiki huku meneja wa Manchester United Jose Mourinho naye akitoa kauli kuhusiana na faida inayopata klabu yake hiyo ya zamani. Chelsea wameshinda mechi 13 mfululizo katika ligi na wanaweza kufikia rekodi iliyowekwa na Arsenal mwaka 2002 kama wakifanikiwa kuichapa Tottenham Hotspurs baadae leo. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Conte alikiri kuwa ni kweli wana faida kidogo kwani wamepata muda wa kupumzika siku moja zaidi ya wapinzani wao Spurs lakini sio wao waliopanga ratiba. Conte aliendelea kudai kuwa anadhani malalamiko yamekuwa makubwa zaidi kwao kwasababu wanaongoza msimamo wa ligi.

WACHEZAJI WANGU WALIGOMBA KUFUNGWA - WENGER.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kikosi chake kiligoma kupoteza mchezo kufuatia kutoka nyuma wakiwa wamefungwa mabao 3-0 na kutoa sare ya mabao 3-3 dhidi ya Bournemouth. Hiyo ni mara ya kwanza kwa Arsenal kufanikiwa kupata alama baada ya kufungwa mabao matatu katika mchezo wa Ligi Kuu. Akihojiwa Wenger amesema mchezo huo ulikuwa ni jaribio tosha la kimwili na kiakili, lakini mwishoni wamehuzunishwa kwa kutoshinda. Wenger aliendelea kudai kuwa walihitaji kushinda mchezo huo lakini haikuwa rahisi kwani timu kubwa zingine nazo zilipoteza mechi zao kwa Bournemouth ikiwemo Liverpool.

CHAPECOENSE KUSAJILI 20 WAPYA KWA AJILI YA MSIMU MPYA.

MKURUGENZI wa michezo wa Chapecoense, Rui Costa amedai kuwa klabu hiyo inatarajia kusaini wachezaji wapya 20 kwa ajili ya msimu mpya huku fulana mbili za wachezaji walionusurika katika ajali zikituzwa bila kwa matumaini kuwa wanaweza kurejea uwanjani tena. Klabu hiyo ilipoteza karibu wachezaji wote waliofariki katika ajali ya ndege nchini Colombia Novemba 28 mwaka huu. Klabu hiyo ndogo inayotoka kusini wa Brazil ilikuwa njiani kuelekea Medelin kucheza na Atletico Nacional katika mchezo wa fainali ya Copa Sudamericana kabla ya kupata ajali hiyo milimani na kuua watu 71. Mabeki Neto na Alan Ruschel walisalimika katika ajali hiyo sambamba na kipa wa akiba Jackson Follmann ambaye mguu wake umekatwa kutokana na ajali hiyo. Costa amesema wachezaji wote watatu waliopona ajalini bado wana nafasi ya kucheza na hakuna mchezaji yeyote atakayevaa jezi zao na pamoja na kwamba Follmann hataweza lakini anaweza kushiriki kwa upande mwingine. Costa aliendelea kudai kuwa klabu hiyo itasajili wachezaji 18 mpaka 20 wapya kabla ya kuanza kwa msimu Januari 26 kwa mchezo wa nyumbani dhidi ya Joinville.

Monday, January 2, 2017

WENGER ALISIFIA BAO LA GIROUD.


MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amedai kuwa bao murua la Olivier Giroud alilofunga katika ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Crystal Palace ni moja kati ya mabao yake tano bora aliyopata kushuhudia katika kipindi cha miaka 21 akiwa na klabu hiyo.
Mabao ya kina Thierry Henry na Dennis Bergkamp nayo yapo katika orodha yake lakini amesema bao hilo la jana milele litakuwa la Giroud pekee.
Wenger amesema kiufundi sio jambo lisilowezekana lakini unatakiwa na uwezo tofauti kwani mpira wa krosi haukuja kama ilivyotakiwa na Giroud alifanya jambo la kipekee.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amesema ilikuwa kama bahati kwani mpira haukuja kama ilivyotakiwa.

Friday, December 30, 2016

MAPINDUZI CUP YANG'OA NANGA.

Timu zitakazoshiriki kombe la Mapinduzi msimu huu zinatarajiwa kupata asilimia kumi ya mapato ya uwanjani baada ya kulipiwa gharama zote za siku ya mchezo. Kila klabu itapatiwa asilimia hizo 10 baada ya kulipiwa gharama zote ya siku ya mchezo na kinachobakia watapatiwa asilimia hizo. Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa kamati inayosimamia kombe la Mapinduzi Sharifa Khamis amesema msimu huu wanatarajia kuwapatia kila timu asilimia 10 ya mapato ya uwanjani baada ya kulimia gharama zote za mchezo. “Vilabu vimelalamika hasa vya Zanzibar hali zao ni mbaya sana, kwaiyo kwa pamoja tumekubaliana kwa kila timu tutaipatia asilimia 10 ya mapato ya uwanjani baada ya kulimia gharama zote za mchezo.” Aidha kamati ya kombe la Mapinduzi msimu huu imepanga kila timu kuwapatia nafasi 35 kwa wachezaji pamoja na viongozi kuingia bure uwanjani katika mashindano hayo. “Tumekubaliana na vilabu kila timu tutaipatia nafasi 35 za kuingia bure uwanjani kuangalia mashindano hayo.” Pazia la Mashindano ya Kombe la Mapinduzi linatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake Disemba 30, 2016 katika uwanja wa Amaan saa 2:15 Usiku ambapo kutakuwa na mchezo wa Derby ya Jangombe kati ya Taifa ya Jangombe na Jangombe boys ambapo mashindano ya msimu huu yameshirikisha vilabu 9, vitano vikitokea Zanzibar, vitatu Tanzania bara na kimoja kutaka Uganda ambao ndio mabingwa watetezi timu ya URA.


KUNDI A: Simba, URA, KVZ, Taifa ya Jangombe na Jangombe Boys.
KUNDI B: Yanga, Azam, Zimamoto na Jamhuri.




RATIBA KAMILI YA MAPINDUZI CUP

30/12/2016 Taifa ya jang’ombe vs Jang’ombe boys saa 2:30 usiku.
1/1/2017 KVZ VS URA Saa 10:00 alasiri, Simba vs Taifa ya Jang’ombe saa 2:30 usiku.
2/1/2017 Azam vs Zimamoto saa 10:00 alasiri, Yanga vs Jamhuri saa 2:30 usiku.
3/1/2017 Jang’ombe boys vs URA saa 10:00 alasiri, KVZ vs Simba saa 2:30 usiku.
4/1/2017 Zimamoto vs Yanga saa 10:00 alasiri, Jamhuri vs Azam saa 2:30 usiku.
5/1/2017 KVZ vs Jang’ombe boys saa 10:00 alasiri, Simba vs URA saa 2:30 usiku.
6/1/2017 Taifa ya jang’ombe vs KVZ saa 2:30 usiku.
7/1/2017 Jamhuri vs Zimamoto saa 10:00 alasiri, Yanga vs Azam saa 2:30 usiku.
8/1/2017 Simba vs Jang’ombe boys saa 10:00 alasiri ,Taifa ya jang’ombe vs URA 2:30 usiku.
10/1/2017 Saa 10: 00 nusu fainal ya kwanza , Saa 2:30 nusu fainal ya pili.

13/1/2017 FAINAL saa 2: 30 usiku.
 
CHANZO NI BEKI 3
BIN ZUBERY