AJTC VOICE FO VOICLESS

Alhamisi, 5 Januari 2017

ALHAMISI KATIKA MICHEZO TAEHE 05/01/2017


MKEKA.jpg




Mfumo wa Kocha George Lwandamina umeanza kuwashitua baadhi ya wapinzani wa Yanga katika michuano ya Mapinduzi.
Yanga imekuwa ikitumia pasi ndefu za katikati ya uwanja kutengeneza mabao na inaonekana Thabani Kamusoko na Haruna Niyonzima ndiyo wamepewa jukumu hilo.

Wawili hao, wamekuwa wakipiga pasi ndefu kwa Amissi Tambwe, Donald Ngoma au Simon Msuva ambao wamekuwa wakimalizia pasi hizo.

Taarifa zinaeleza, ndani ya vikosi vya Simba na Azam FC, gumzo la mabao ya Yanga na pasi zinazopigwa limekuwa gumzo.

"Ni kweli, unaona kabisa kuna aina fulani ya kitu kinafundishwa. Tunajua na tunafuatilia. Haina maana tutacheza kama Yanga lakini lazima uwajue wapinzani wako mapema," alisema mmoja ya wahusika ndani ya Simba lakini akaomba kutotajwa jina.

"Kama mwenzako anafanya kazi vizuri, basi lazima ujifunze au uangalie unafanyaje vizuri zaidi yake au unaweza kumshinda."
Lakini upande wa Azam FC, John Bocco ambaye ni nahodha alisema wanaona kila kitu na wanajiandaa.

"Kweli kuna mambo mengi ya kujifunza kila unapocheza. Yanga ni timu kubwa, wamefunga mabao mengi lakini sisi tuna kikosi bora. Kina uwezo wa kupambana na kila mfumo," alisema.

Tayari Yanga imefuzu katika hatua ya mtoano baada ya ushindi mara mbili mfululizo
 



Kiungo mwenye kasi wa Yanga, Simon Msuva wa Yanga, amesema anautaka ufungaji bora na uchezaji bora wa Kombe la Mapinduzi.

Msuva amesema angependa kupata ufungaji bora wa michuano hiyo kwa mara ya pili. Kwa sasa anaongoza kwa kuwa na mabao manne ya kufunga.

“Kweli nataka ufungaji bora, niliwahi kuwa mfungaji bora wa Mapinduzi,” alisema.

“Kwa ushirikiano na wenzangu kwenye timu, ningependa kwua mfungaji bora. Kawaida ushirikiano unamsaidia mtu kuwa bora zaidi,” alisema.


Katika mechi mbili dhidi ya Jamhuri ambayo Yanga ilishinda kwa mabao 6-0 na ule dhidi ya Zimamoto, ikishinda mabao 2-0. Msuva alifunga mabao mawili kila mechi
 

DIAMOND KUTUMBIZA TUZO ZA MWANASOKA BORA AFRIKA LEO ABUJA

Na Mahmoud Zubeiry, DAR E SALAAM MWANAMUZIKI nyota Tanzania, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ na wasanii wengine wakubwa barani, wanatarajiwa kutumbuiza usiku wa leo katika sherehe za tuzo Mwanasoka Bora Afrika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano mjini Abuja, Nigeria. Diamond anaweka rekodi nyingine kubwa katika historia yake ya muziki kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kutumbuiza kwenhye tuzom hizo kubwa barani.  Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borussia Dortmund ya Ujerumani atatetea tuzo yake ya Mwanasoka Bora Afrika dhidi ya Riyad Mahrez wa Algeria na Leicester City na Sadio Mane wa Senegal na Liverpool.
Diamond Platnumz anatumbuiza usiku wa leo katika sherehe za tuzo Mwanasoka Bora Afrika mjini Abuja, Nigeria
Miongoni mwa wanamuziki hao, ni mtoto gwiji wa muziki Afrika, Fela-Anikulapo Kuti, aitwaye Femi Kuti.  Kuti, ambaye alianzisha bendi yake mwenyewe ya Positive Force mwaka 1986 anafahamika kwa muziki wake mzuri.  Amejitambulisha kama gwiji kweli Afro Beat kwa staili yake mwenyewe na moja ya nyimbo zake zinazobamba ni Beng, Beng, Beng. Msanii mwingine anayetarajiwa kutumbuiza usiku wa leo ni dansa, mwandishi wa nyimbo na mtumbuizaji, Chinedu Okoli, maarufu Flavour N’abania wa Nigeria.  Flavour anafahamika barani na nchi nyingine duniani kwa kibao chake cha kuwarusha watu ‘klabu’ kiitwacho Nwa Baby.  Pia watakuwepo Diamond Platinumz mkali wa Bongo Flava kutoka Tanzania ambaye anatamba na kibao chake Salome kwa sasa. Wengine ni Omawumi anayetamba na nyimbo za Megbele na If you ask Me, kundi la Muffinz kutoka Afrika Kusini, Yemi Alade na DJ Jimmy Jatt. Wakati huo huo; Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou aliwasili mjini Abuja jana na kupokewa na Makamu wake wa kwanza, Almamy Kabele Camara; Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Adoum Djibrine, Rais wa Shirikkisho la Soka Nigeria, Amaju Pinnick na Maofisa mbalimbali wa Globacom, wadhamini wa tuzo shughuli hiyo.

Pierre-Emerick Aubameyang anatetea tuzo yake dhidi ya Riyad Mahrez na Sadio Mane
TATU BORA YA TUZO MBALIMBALI LEO Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund) Riyad Mahrez (Algeria & Leicester City) Sadio Mane (Senegal & Liverpool) Mwanasoka Bora wa Mwaka Anayecheza Afrika Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns) Khama Billiat (Zimbabwe & Mamelodi Sundowns) Rainford Kalaba (Zambia & Tp Mazembe) Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Kike Asisat Oshoala (Nigeria & Arsenal Ladies) Elizabeth Addo (Ghana & Kvarnsvedensik) Gabrielle Aboudi Onguene (Cameroon & Rossyanka) Mwanasoka Bora Anayechipukia Elia Meschak (Dr Congo & Tp Mazembe)    Kelechi Iheanacho (Nigeria & Manchester City) Naby Keita (Guinea & Rb Leipzig) Mwanasoka Bora Kijana wa Mwaka Alex Iwobi (Nigeria And Arsenal) Eric Ayiah (Ghana And Charity Fc)         Sandra Owusu-Ansah (Ghana And Supreme Ladies) Kocha Bora wa Mwaka Florent Ibenge (Timu ya taifa DRC) Pitso Mosimane (Mamelodi Sundowns)  Florence Omagbemi (Timu ya taifa ya wanawake ya Nigeria) Klabu Bora ya Mwaka Mamelodi Sundowns  Tp Mazembe      Zesco United Timu Bora ya Taifa ya Mwaka DRC Senegal  Uganda Timu Bora ya Taifa ya Wanawake ya Mwaka Cameroon Nigeria   Afrika Kusini Refa Bora wa Mwaka Bakary Papa Gassama       Ghead Zaglol Grisha      Malang Diedhiou             Kiongozi Bora wa Soka wa Mwaka Manuel Lopes Nascimento Rais wa Shirikisho la Soka Guinea Bissau Tuzo ya Gwiji Laurent Pokou, mchezaji wa zamani wa Ivory Coast Emilienne Mbango, mchezaji wa zamani wa Cameroon

Kipa Denis Onyango wa Uganda anawania Tuzo ya mchezaji Bora Anayecheza Afrika, baada ya kuipa Mamelodi Sundowns taji la Ligi ya Mabingwa
Kikosi Bora wachezaji 11 Kipa: Denis Onyango (Uganda na Mamelodi Sundowns)  Mabeki: Serge Aurier (Ivory Coast na Paris Saint-Germain), Aymen Abdennour (Tunisia na Valencia), Eric Bailly (Ivory Coast & Manchester United), Joyce Lomalisa (DRC na As Vita) Viungo: Khama Billiat (Zimbabwe & Mamelodi Sundowns), Rainford Kalaba (Zambia & Tp Mazembe), Keegan Dolly (Afrika Kusini & Mamelodi Sundowns), Washambuliaji: Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund), Sadio Mane (Senegal & Liverpool), Riyad Mahrez (Algeria & Leicester City)  Wa akiba; Aymen Mathlouthi (Tunisia & Etoile Du Sahel), Kalidou Koulibaly (Senegal & Napoli), Salif Coulibaly (Mali & Tp Mazembe), Islam Slimani (Algeria & Leicester City), Mohamed Salah (Misri & Roma), Kelechi Iheanacho (Nigeria & Manchester City), Alex Iwobi (Nigeria And Arsenal)

Samuel Eto'o wa Cameroon anashikilia rekodi ya kushinda tuzo nyingi za Mwanasoka Bora Afrika 
WALIOWAHI KUWA WANASOKA BORA AFRIKA 1992 Abedi Ayew Pele (Ghana) 1993 Rashidi Yekini (Nigeria) 1994 Emmanuel Amunike (Nigeria) 1995 George Weah (Liberia) 1996 Nwankwo Kanu (Nigeria) 1997 Victor Ikpeba (Nigeria) 1998 Mustapha Hadji (Morocco) 1999 Nwankwo Kanu (Nigeria) 2000 Patrick Mboma (Cameroon) 2001 El-Hadji Diouf (Senegal) 2002 El Hadji Diouf (Senegal) 2003 Samuel Eto'o (Cameroon) 2004 Samuel Eto'o (Cameroon) 2005 Samuel Eto'o (Cameroon) 2006 Didier Drogba (Ivory Coast) 2007 Frederic Kanoute (Mali) 2008 Emmanuel Adebayor (Togo) 2009 Didier Drogba (Ivory Coast) 2010 Samuel Eto'o (Cameroon) 2011 Yaya Toure (Ivory Coast) 2012 Yaya Toure (Ivory Coast) 2013 Yaya Toure (Ivory Coast) 2014 Yaya Toure (Ivory Coast) 2015 Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon) 2016  ?????
 

SIMBA NA URA KATIKA BONGE LA MECHI LEO KOMBE LA MAPINDUZI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM SIMBA SC inakamilisha mechi zake za Kundi A Kombe la Mapinduzi, kwa kumenyana na mabingwa watetezi, URA ya Uganda usiku wa leo. Mchezo huo utakaotanguliwa na mechi nyingine ya kundi hilo kati ya KVZ na Jang'ombe Boys kuanzia Saa 10:00 jioni, itaanza Saa 2:30 usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Simba inayofundishwa na kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog itahitaji ushindi ili kuongoza kundi na kukwepa kukutana na wapinzani wa jadi, Yanga mapema. Lakini hilo litakuwa gumu mbele ya URA ambayo nayo itahitaji zaidi ushindi kwanza kujihakikishia tiketi ya Nusu Fainali.
Simba inaongoza kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na URA, Taifa Jang’ombe na Jang’ombe Boys zenye pointi tatu kila mmoja.’ Maana yake URA haina namna nyingine zaidi ya kushinda ili kuzipiku Taifa na Jang’ombe katika kinyang’anyiro cha tiketi ya Nusu Fainali. Simba kutaka ushindi na URA pia kutaka kushinda lazima kunamaanisha mechi yao leo ni nzuri.   Katika mechi ya Kundi B usiku wa jana, Azam FC ililazimishwa sare ya bila kufungana na Jamhuri ya Pemba Uwanja wa Amaan. Kwa sare hiyo, Azam inafikisha pointi tatu na kuendelea kubaki nafasi ya pili nyuma ya Yanga, yenye pointi sita, ambayo jana jioni iliifunga Zimamoto 2-0. Azam sasa itacheza mechi yake ya mwisho Jumamosi dhidi ya Yanga, mchezo ambao utatanguliwa na mechi kati Zimamoto na Jamhuri. 
CHANZO BIN ZUBERY
SALEHE 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni