AJTC VOICE FO VOICLESS

Jumatatu, 9 Januari 2017

JUMATATU 09/01/2017

YANGA KUWAKOSA TAMBWE, NGOMA, ZULU NA CHIRWA KESHO DHIDI YA SIMBA

Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR KOCHA wa Yanga, Mzambia George Lwandamina amesema kwamba ataingia kwenye mchezo wa kesho dhidi ya mahasimu, Simba hali ya kikosi chake ikiwa si nzuri sana. Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online leo, Lwandamina amesema kwamba wachezaji wake wanne tegemeo wote ni majeruhi na hawawezi kucheza kesho. Lwandamina aliwataja wachezaji majeruhi ni Wazambia wenzake, viungo Justin Zulu na Obrey Chirwa na washambuliaji Mrundi Amissi Tambwe na Mzimbabwe Donald Ngoma.
George Lwandamina amesema wachezaji wake tegemeo wanne ni majeruhi kuelekea mchezo wa kesho
Pamoja na hao, Lwandamina alisema beki Pato Ngonyani na mshambuliaji Matheo Anthony nao wote ni wagonjwa na hawana uhakika wa kucheza kesho. Kwa ujumla Lwandamina ambaye timu yake ilifungwa 4-0 na Azam FC Jumamosi kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi A, alisema ataingia kwenye mchezo wa kesho katika mazingira magumu ya kukatisha tamaa. “Lakini hatuna namna nyingine, lazima tuingize timu tukapambane,”alisema. Yanga inakutana na mahasimu, Simba katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku wa leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
 
 

MKUDE: MECHI NA YANGA ITAKUWA NGUMU KESHO

Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR NAHODHA wa Simba, Jonas Mkude amesema kwamba mechi dhidi ya Yanga itakuwa ngumu kwa sababu kila timu imejiandaa vizuri. Akizugumza jana baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Jang’ombe Boys kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi A, Mkude alisema kwamba hawana wasiwasi wowote kuelekea Nusu Fainali dhidi ya mahasimu, Yanga. “Sisi tumejiandaa vizuri, ni matumaini yetu na wao wamejiandaa vizuri, mchezo wa mpira wa miguu ni maandalizi, baada ya maandalizi tutakutana tutacheza, utakuwa mchezo mzuri, kipimo kizuri kwetu na kwao, dakika 90 zitaamua,”.
Jonas Mkude (kushoto) amesema mechi dhidi ya Yanga itakuwa ngumu kesho
Simba na Yanga zitakutana katika Nusu Fainali ya Pili ya Kombe la Mapinduzi kesho Saa 2:15 usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar.  Hiyo inafuatia Simba kumaliza kileleni mwa Kundi A kwa pointi zake 10, ikifuatiwa na Taifa Jang’ombe pointi tisa, Jang’ombe Boys pointi sita na URA pointi nne.  Ikumbukwe Yanga imeshika nafasi ya pili Kundi B nyuma ya Azam walioongoza kwa wastani wa mabao baada ya kufungana kwa pinti saba kila timu. Mabao yote ya Simba SC jana yalifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo moja kila kipindi. Nusu Fainali ya kwanza kesho itazikutanisha Azam FC na Taifa Jang’ombe Saa 10:30 jioni. Hiyo inafuatia Taifa kuwalaza waliokuwa mabingwa watetezi, URA ya Uganda 1-0 katika mchezo wa mwisho wa Kundi A usiku wa jana Uwanja wa Amaan. Bao pekee la Taifa Jang’ombe limefungwa na Mohammed Said kwa penalti, baada ya Ally Badru kuangushwa kwenye boksi. Mapema URA nao walipoteza penalti baada ya Bogota Labama kuangushwa kwene boksi.
 
 

MA DJ WA SAUZI WAUFAGILIA MUZIKI WA BONGO

Na Mwandishi Wetu,  DAR ES SALAAM WACHEZESHA disko ‘ma DJ’ maarufu Afrika Kusini Siyabonga Sibeko ‘DJ Capital’ na Lutendo Kungoane ‘Dj Sliqe’ wamesema kwamba muziki wa Tanzania uko juu kwa sasa. Wakizungumza na Waandishi wa Habari jana katika hoteli ya New Africa, Dar es Salaam ma DJ hao wa Redio na Telesheni nchini Afrika Kusini walisema Tanzania imepiga hatua kubwa kimuziki. “Kwa sasa huwezi kuzungumzia nchi zinazofanya vizuri kwa kiwango cha juu kimuziki Afrika bila kuitaja


Tanzanja,”alisema Dj Capital na kuongeza; “Afrika Kusini, Nigeria, Ghana, Tanzania na Kenya hizo ndizo nchi za Afrika zinazofanya vizuri katika muziki wa kisasa,”alisema. Kwa upande wake DJ Sliqe’ alisema kwamba anavutiwa zaidi na wasanii wawili wa Tanzania kwa sasa, ambao ni Diamond Platnumz na Vanessa Mdee. “Ni wasanii wengi wa Tanzania wanaofanya vizuri kwa sasa, lakini mimi upande wangu nawapenda zaidi hao wawili,”alisema.  Wawili hao, wote ni Ma DJ wa kituo cha Redio cha Touch Central cha Johannesburg, Afrika Kusini wakati DJ Capital pia anafanya kipindi cha Club 808 cha Televisheni ya ETV nchini humo. Wawili ambao wamekuja nchini kwa ziara ya wiki moja kujifunza zaidi kuhusu muziki wa Tanzania, pia ni Ma DJ wa kumbi za disko nchin kwao.  “Tumekuja hapa kujigunza na kukutana na wasnaii kwa sababu sisi pia ni watayarishaji wa muziki,”alisema Capital.
 

AZAM KUMENYANA NA TAIFA JANG’OMBE NUSU FAINALI MAPINDUZI

Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR TIMU ya Azam FC itamenyana na Taifa Jang’ombe katika Nusu Fainali ya kwanza Kombe la Mapinduzi Jumanne jioni Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Hiyo inafuatia Taifa kuwalaza waliokuwa mabingwa watetezi, URA ya Uganda 1-0 katika mchezo wa mwisho wa Kundi A usiku huu Uwanja wa Amaan. Bao pekee la Taifa Jang’ombe limefungwa na Mohammed Said kwa penalti, baada ya Ally Badru kuangushwa kwenye boksi. Mapema URA nao walipoteza penalti baada ya Bogota Labama kuangushwa kwene boksi.

Nusu Fainali ya Pili itawakutanisha watani wa jadi, Simba na Yanga Jumanne Saa 2:15 usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar.  Hiyo inafuatia Simba SC kushinda 2-0 dhidi ya Jang’ombe Boys jioni ya leo katika mchezo wa mwingine wa Kundi A. Matokeo hayo yanaifanya Simba imalize kileleni mwa Kundi A kwa pointi zake 10, ikifuatiwa na Taifa Jang’ombe pointi tisa, Jang’ombe Boys pointi sita na URA pointi nne.  Ikumbukwe Yanga imeshika nafasi ya pili Kundi B nyuma ya Azam walioongoza kwa wastani wa mabao baada ya kufungana kwa pinti saba kila timu. Mabao yote ya Simba SC leo yamefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo moja kila kipindi.
 

FA CUP: DROO YA RAUNDI YA 4 LEO, MABINGWA MAN UNITED KUWAKWAA NANI?


DROO YA RAUNDI YA 4 ya EMIRATES FA CUP itafanyika Leo Usiku kabla kuanza kwa Mechi ya mwisho ya Raundi ya 3 kati ya Cambridge and Leeds United.
Droo hiyo itafanyika huko BT Tower Mjini London na kuendeshwa na Wachezaji wa zamani wa Kimataifa wa England Michael Owen na Martin Keown.
Mechi 16 za Raundi ya 4 zitapangwa na kutakiwa kuchezwa Wikiendi ya Januari 28 na 29.
++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-FA CUP 2016/17, ambalo pia hujulikana kama FA Challenge Cup, ni mara ya 136 kushindaniwa kila Mwaka tangu lilipoanzishwe na linatambuliwa kama ndio Mashindano ya kale kupita yote Duniani.
-Kombe hili linadhaminiwa na Kampuni ya Ndege8k ya Emirates na kwa sababu za kiudhamini linaitwa Emirates FA Cup.
-Timu 736 zilikubaliwa kushiriki Mashindano haya Msimu huu na yalianza kwa Raundi ya Awali na yatafikia Tamati kwa Fainali itakayochezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Mei 27, 2017.
-Mshindi wa FA CUP ataingizwa Hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI Msimu wa 2017/18.
-Bingwa Mtetezi ni Manchester United.
+++++++++++++++++++
Mabingwa Watetezi Manchester United wamepewa Kipira Namba 3 ambacho kitawekwa ndani ya Mtungi pamoja na Vipira vingine 31ambavyo vitatolewa Mtungini na Owen na Keown kupambanisha Timu.
 NAMBA ZA VIPIRA KWA KILA TIMU:
1 Ipswich Town au Lincoln City
2 Rochdale
3 Manchester United 
4 Hull City 
5 Sunderland au Burnley
6 Blackburn Rovers
7 Millwall
8 Manchester City
9 Brighton & Hove Albion
10 Blackpool au Barnsley
11 Wigan Athletic au Nottingham Forest
12 Birmingham City au Newcastle United
13 Chelsea 
14 Middlesbrough 
15 Derby County 
16 Leicester City 
17 Liverpool au Plymouth Argyle 
18 Wycombe Wanderers
19 Watford
20 Arsenal
21 Fulham
22 Wolverhampton Wanderers
23 Cambridge United au Leeds United 
24 Bristol City au Fleetwood Town
25 Huddersfield Town
26 Tottenham Hotspur
27 Brentford
28 Bolton Wanderers au Crystal Palace
29 Norwich City au Southampton
30 Sutton United au AFC Wimbledon
31 Accrington Stanley
32 Oxford United
 

EFL CUP - NUSU FAINALI: JUMANNE KUANZA OLD TRAFFORD MAN UNITED v HULL CITY!


EFL CUP
Nusu Fainali
**Saa za Bongo
Jumanne Januari 10
2300 Manchester United v Hull City
Jumatano Januari 11
2245 Southampton V Liverpool
=============================
IMG-20170109-WA0000NUSU FAINALI za Kombe la Ligi hukoEngland ambalo sasa huitwa EFL CUP (English Football League Cup) zitaanza Jumanne Januari 10 huko Old Trafford kwa Manchester
 United kucheza na Hull City.
Siku ya Pili, Jumatano Januari 11, itachezwa Nusu Fainali ya Pili huko Saint Mary kwa Southampton kucheza na Liverpool.
Nusu Fainali hizi huchezwa kwa Mikondo Miwili ya Nyumbani na Ugenini na hivyo Marudiano ya Mechi hizi yatakuwa hapo Januari 25 na 26 huko Anfield na KCOM Stadium.
Kwenye Mechi ya Old Trafford, Meneja wa Man United Jose Mourinho amedokeza atabadili Kikosi chake toka kile kilichoichapa Reading 4-0 Jumamosi katika Raundi ya 3 ya FA CUP.
Akiongea baada ya Mechi hiyo, Mourinho alieleza: "Jumamosi tumecheza na Wachezaji freshi. Ila sitaki ieleweke tuna Timu ya Kwanza au ya Pili! Wachezaji ambao hawakucheza Mechi hii watacheza na Hull..hivyo ni rahisi kujua Zlatan, Pogba, Herrera, Valencia watarudi Mechi na Hull."
+++++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-Msimu huu hili Kombe la Ligi halina Mdhamini na limebatizwa English Football League Cup, EFL CUP.
-Huko nyuma Kombe la Ligi, kwa sababu za kiudhamini, liliwahi kubatizwa Coca-Cola Cup, Worthington Cup, Carling Cup na Capital One Cup.
+++++++++++++++++
Hull City, chini ya Meneja Mpya Marco Silva kutoka Ureno alietwaa mikoba ya Mike Phelan alietimuliwa Wiki iliyopita, itatinga Old Trafford ikiwa na Difensi ya kuungaunga kutokana na Majeruhi kadhaa.
Sentahafu wao Michael Dawson aliumia na kutolewa Kipindi cha Pili Juzi kwenye FA CUP walipoifunga Swansea City na nafasi hiyo kushikwa na Kiungo Tom Huddlestone alishirikiana na Kiungo mwingine Jake Livermore.
Beki mwingine Majeruhi wa Hull ni Curtis Davis na hivyo kuwaacha Hull kutumia Viungo Watatu kwenye Nafasi 4 za Difensi yao.
Nafasi ya Fulbeki wa Kulia imelazimika kuzibwa na David Meyler baada kumpoteza Ahmed Elmohamady ambae ameenda Egypt kujiunga na Timu ya Taifa kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2017, yanayoanza huko Gabon Januari 14.
EFL CUP
Nusu Fainali
MARUDIANO
**Saa za Bongo
Jumatano Januari 25
2300 Liverpool v Southampton
Alhamisi Januari 26
2245 Hull City v Manchester United

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni